La Quica
JF-Expert Member
- Dec 19, 2017
- 1,009
- 2,315
Heri ya Pasaka.
Iko hivi, imekuwa kama tamaduni kwetu kuwa siku za sikukuu ndio mtu atavaa vizuri, atakula vizuri na atatoka out.
Jana wakati natoka kwenye mishe zangu nikamuita boda wangu anipeleke home nikaangalie chama langu Liverpool likimenyana na Arsenal.
Jamaa kafika asee alikuwa amevaa amependeza nguo mpya mpya (sio kawaida yake huwa sio msafi sana namtumia tu kwakuwa ni mwaminifu).
Jana yake usiku (juzi) alinipigia kuniomba nimtumie namba ya jamaa yangu ambae huwa ananiuzia kuku wa kienyeji. Akaniambia "bro naomba namba ya yule jamaa wa kuku nimeipoteza nataka home nao wale kuku hii sikukuu"
Sasa jana wakati ananipeleka home njiani ikawa kero kwa kuwa watoto wanakimbia kimbia hovyo barabarani na watu wazima wamejaa sio kawaida. Nikajua tu shida ni hii sikukuu.
Nadhani tuwe na utamaduni wa kujipenda, kula vizuri na kutoka mara kwa mara siku zisizo za sikukuu.
Mimi jana nimerudi zangu home nikala matunda yangu na kulala lakini hizi siku kuna watu wanazichukulia ndio siku za kulewa, kutoka, kufanya ngono na kuvaa vizuri jambo ambalo mimi naona sio sawa kabisa.
Hizi siku huwa ndio siku zenye vurugu nyingi. Ambae hajawahi kunywa atakunywa, wasiotoka watatoka kwahiyo kero ni nyingi. Lakini yote husabaishwa na utamaaduni mbovu kuwa siku za sikukuu ndio za kunywa, kutoka, kuvaa vizuri na kula kuku, nyama na pilau.
Sio sawa.