Tujenge utamaduni wa kupendeza (kujipenda), kutoka out na kula vizuri

Tujenge utamaduni wa kupendeza (kujipenda), kutoka out na kula vizuri

Sikukuu haiwezi kuwa sawa na siku za kawaida hata nchi zilizoendelea wana majira yao ambayo wananchi wake wanasherekea na huwezi kufananisha na siku za kawaida. Na kila mmoja anakuwa na namna ya kusherekea kwake kwa namna yake.
 
Nimekupenda bure Mideko
 
........jf bana saa zingine!! sijui mleta mada hajaeleweka au ni vipi, watu wamekomaa kumuatack personally kwamba ana wivu na bodaboda!!!, wakati boda kamtolea mfano kuwa kang'aa siku hiyo na anataka kuchinja kuku......
........mkuu kashauri vema kabisa kuwa watu wasiishie kupendeza nakula vizuri siku za sikukuu pekee, watu wajitahidi kuwa nadhifu, kujipenda,kujijali na kula vizuri japo siku mojomoja.....
......na hili la kuwatoa watoto na familia out na kuwanunulia nguo au zawadi ni muhimu sana especially kwa watoto wa kike kama unao, inapunguza ulimbukeni wa mambo hayo, inakuwa sio rahisi sana kuhadaika na wanaume wahongaji, eg hawezi kushawishika kirahisi eti kwa kupelekwa beach coz familia yake wanatoka may be kila baada ya miezi miwili mitatu......
......kuna siku nilisikitika sana nilimtembelea Jamaa yangu mmoja anaishi uswahili kidogo, zile nyumba ukiwasha TV watoto wanajaa dirishani kuchungulia, sasa shemeji aliandaa pilau na lilinukia haswaa, Sasa wale watoto dirishani wakaanza kuulizana 'eti we mwanakombo kwani leo kwa kina Themeni kuna arusi!?', kengine kakadakia 'kwani thatha we huoni thi wamepika pilau afu nilimuona Themeni ameshika thoda'......kwa kweli nilijisikia vibaya, ila nilijifinza kitu.......
 
Heri ya Pasaka.

Iko hivi, imekuwa kama tamaduni kwetu kuwa siku za sikukuu ndio mtu atavaa vizuri, atakula vizuri na atatoka out.

Jana wakati natoka kwenye mishe zangu nikamuita boda wangu anipeleke home nikaangalie chama langu Liverpool likimenyana na Arsenal.

Jamaa kafika asee alikuwa amevaa amependeza nguo mpya mpya (sio kawaida yake huwa sio msafi sana namtumia tu kwakuwa ni mwaminifu).

Jana yake usiku (juzi) alinipigia kuniomba nimtumie namba ya jamaa yangu ambae huwa ananiuzia kuku wa kienyeji. Akaniambia "bro naomba namba ya yule jamaa wa kuku nimeipoteza nataka home nao wale kuku hii sikukuu"

Sasa jana wakati ananipeleka home njiani ikawa kero kwa kuwa watoto wanakimbia kimbia hovyo barabarani na watu wazima wamejaa sio kawaida. Nikajua tu shida ni hii sikukuu.

Nadhani tuwe na utamaduni wa kujipenda, kula vizuri na kutoka mara kwa mara siku zisizo za sikukuu.

Mimi jana nimerudi zangu home nikala matunda yangu na kulala lakini hizi siku kuna watu wanazichukulia ndio siku za kulewa, kutoka, kufanya ngono na kuvaa vizuri jambo ambalo mimi naona sio sawa kabisa.

Hizi siku huwa ndio siku zenye vurugu nyingi. Ambae hajawahi kunywa atakunywa, wasiotoka watatoka kwahiyo kero ni nyingi. Lakini yote husabaishwa na utamaaduni mbovu kuwa siku za sikukuu ndio za kunywa, kutoka, kuvaa vizuri na kula kuku, nyama na pilau.

Sio sawa.
Out huwa natoka lskini naishia kubarazani.
 
........jf bana saa zingine!! sijui mleta mada hajaeleweka au ni vipi, watu wamekomaa kumuatack personally kwamba ana wivu na bodaboda!!!, wakati boda kamtolea mfano kuwa kang'aa siku hiyo na anataka kuchinja kuku......
........mkuu kashauri vema kabisa kuwa watu wasiishie kupendeza nakula vizuri siku za sikukuu pekee, watu wajitahidi kuwa nadhifu, kujipenda,kujijali na kula vizuri japo siku mojomoja.....
......na hili la kuwatoa watoto na familia out na kuwanunulia nguo au zawadi ni muhimu sana especially kwa watoto wa kike kama unao, inapunguza ulimbukeni wa mambo hayo, inakuwa sio rahisi sana kuhadaika na wanaume wahongaji, eg hawezi kushawishika kirahisi eti kwa kupelekwa beach coz familia yake wanatoka may be kila baada ya miezi miwili mitatu......
......kuna siku nilisikitika sana nilimtembelea Jamaa yangu mmoja anaishi uswahili kidogo, zile nyumba ukiwasha TV watoto wanajaa dirishani kuchungulia, sasa shemeji aliandaa pilau na lilinukia haswaa, Sasa wale watoto dirishani wakaanza kuulizana 'eti we mwanakombo kwani leo kwa kina Themeni kuna arusi!?', kengine kakadakia 'kwani thatha we huoni thi wamepika pilau afu nilimuona Themeni ameshika thoda'......kwa kweli nilijisikia vibaya, ila nilijifinza kitu.......
JF wajuaji wengi, mimi nimesema watu wajipende. Nikatoa mfano boda wangu huwa sio msafi sana na mtaani sionagi watu ila siku za sikukuu tu na hata ninampomtuma kuku huwa yeye hachukui bali ilipofika sikukuu tu ndio akaomba namba na yeye achukue.

Watu wanasema naona wivu sijui shida ni nini. Tumeshajenga utamaduni mbovu sana na wa hovyo.

Mimi sijasema watu wasile vizuri siku za sikukuu au wasitoke au wasivae vizuri. Ila naona kuna shida pale unapoona watu wamejizoesha kula, kutoka na kuvaa vuzuri siku za sikukuu tu na sio utaratibu wa kila siku.
 
Wewe unapenda kupangiwa utaratibu wako wa maisha?
 
Nd umtolee mfn boda boda wako kwel mtu unaye mwamin na anakuamin af wew unakuja ku msnich huku daah uamimif gan siri hakun
 
Tatizo pesa 90% ya watanzania wanaishi kwenye umasikini kutoka out bila unawezaje mkuu try to trade their minds.
 
Kuna haja gani ya kuyokufurahia maisha mpaka siku fulani?
Hayo ndio maisha yao na kakuambia nani kutoka au kuvaa vizuri tu ndio kufurahia maisha. Mtazamo wako ni wakwako pekeako ingekua hawapo sahihi wasingefanya hivyo. Ww kama unajiweza kawaveshe vizuri watoe kila siku sio kukaa sebuleni kwa shemeji na kuleta imagination za ajabu ajabu kisa kila weekend dada ako anatolewa kila weekend basi unahisi kila mtu anaweza
 
Mi Jana nimelala na kushinda JF...Leo nitazurura mpaka miguu ijute kuwepo mwilini mwangu
Uzuri wa jf unaweza kushnda humu na Hali zote ukaziptia hyo siku utafurah,utakasirika,utahuzunika na mwisho kabisa unahitimisha siku yko kw kuipongeza jf
 
Kwanza ndio maana ikaitwa SIKU KUU, usipopendeza sikukuu na kula vizuri utafanya hayo siku gani?

Kumbuka kwenye sikukuu pia watu hutembeleana na kubadilishana zawadi na vyakula kiufupi ni siku ya kufurahii wewe muombe tu Mungu akuondolee upweke wako uwe na mtu/watu wa kufurahi nao Sikukuu.
Kwa kweli, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kila mtu afanye atakalo.

Mkuu una gubu sana kisa boda boda wako alipendeza kukuzidi na pilau kala kuku sikukuu wakati boss umeishia kula matunda
Ndio maana comment yako inepata likes nyingi kuliko ya mtoa mada
 
Back
Top Bottom