Tujenge utamaduni wa kupendeza (kujipenda), kutoka out na kula vizuri

Kwamba kwa kuwa siku zingne unakulaga poa,unavaa poa na kujivinjari basi sikukuu ule ugali matembere?....SIKU~KUU itabak kuwa special day tu hata ukifanya hayo kila siku!
Hapana sina maana hiyo. Wengi wanajitesa ku save kwaajili ya sikukuu ndio waonekane
 
Sijasema utamaduni ni mbaya nadhani hapo umekurupuka. Kuhusu kubadilika ni kutokana na mabadiliko ya hali ya kimaisha hayo mambo upende usipende yatabadilika tu sijui kutunza vyombo kwa ajili ya wageni, kununua nguo za sikukuu wewe mwenyewe unajua hilo.

Mara ya mwisho kumnunulia mtoto wako nguo ya sikukuu ni lini?
Jana kwenye sikukuu ya Pasaka na Eid pia nishamuandalia nguo 3 me mwenyewe ninazo 3 pia kwa ajili ya Eid,

Utamaduni wa nguo mpya, pilau na biriyani, vyombo vizuri hauwezi kuisha sijui kama unasemea familia za wapi huko
 
Hahahahaha kaumia kuona Boda kala kuku wa kienyeji halafu yeye kala matunda ya buku jero na bado buku ya nauli kamuachia
Huyu boda wangu ananiletea kuku wawili wa kienyeji (20000 kila mmoja) kila baada ya week mbili. Simuonei wivu mkuu kwakuwa mimi sio hohehahe
 
Kwanza ndio maana ikaitwa SIKU KUU, usipopendeza sikukuu na kula vizuri utafanya hayo siku gani?

Kumbuka kwenye sikukuu pia watu hutembeleana na kubadilishana zawadi na vyakula kiufupi ni siku ya kufurahii wewe muombe tu Mungu akuondolee upweke wako uwe na mtu/watu wa kufurahi nao Sikukuu.
Tutembeleane kila siku sio siku kuu tu. Unajua wewe mantiki ya mada yangu hujaelewa vizuri.

Tufanye haya yote siku yoyote sio kusubiri sikukuu.
 
Kila mtu afanye atakalo.

Mkuu una gubu sana kisa boda boda wako alipendeza kukuzidi na pilau kala kuku sikukuu wakati boss umeishia kula matunda
Daaahh nimecheka sana, sijui huwa unafikiria nini 😂😂😂😂🙌🏾🙌🏾
 
......kuna watu wengine siku za za sikukuu ndo hawataki kabisa kufanya mitoko......wanasema zinakua zimekaa kishamba coz siku hizo utaona kila mtu kaenda disco, bar, beach etc.......wanasema ukienda huko na wewe unaonekana ni walewale wa sikukuu, wanasema hukawii kukutana na watoto maeneo hayo au hata watu usiowategemea kama vile mamamkwe na mashemeji zako.......Sasa hilo linawaboa wengi so huamua kushinda nyumbani na kuziacha familia au watoto ndo watoke, wao mitoko yao ni siku za kawaida au siku ya pili yake,boxing days, sasa sijui kama ni wengi wenye mtazamo huo au ni vipi.........
Ni kweli mkuu. Mimi ni mmoja wao.
 
Heri ya Pasaka.

Iko hivi, imekuwa kama tamaduni kwetu kuwa siku za sikukuu ndio mtu atavaa vizuri, atakula vizuri na atatoka out.

Jana wakati natoka kwenye mishe zangu nikamuita boda wangu anipeleke home nikaangalie chama langu Liverpool likimenyana na Arsenal.

Jamaa kafika asee alikuwa amevaa amependeza nguo mpya mpya (sio kawaida yake huwa sio msafi sana namtumia tu kwakuwa ni mwaminifu).

Jana yake usiku (juzi) alinipigia kuniomba nimtumie namba ya jamaa yangu ambae huwa ananiuzia kuku wa kienyeji. Akaniambia "bro naomba namba ya yule jamaa wa kuku nimeipoteza nataka home nao wale kuku hii sikukuu"

Sasa jana wakati ananipeleka home njiani ikawa kero kwa kuwa watoto wanakimbia kimbia hovyo barabarani na watu wazima wamejaa sio kawaida. Nikajua tu shida ni hii sikukuu.

Nadhani tuwe na utamaduni wa kujipenda, kula vizuri na kutoka mara kwa mara siku zisizo za sikukuu.

Mimi jana nimerudi zangu home nikala matunda yangu na kulala lakini hizi siku kuna watu wanazichukulia ndio siku za kulewa, kutoka, kufanya ngono na kuvaa vizuri jambo ambalo mimi naona sio sawa kabisa.

Hizi siku huwa ndio siku zenye vurugu nyingi. Ambae hajawahi kunywa atakunywa, wasiotoka watatoka kwahiyo kero ni nyingi. Lakini yote husabaishwa na utamaaduni mbovu kuwa siku za sikukuu ndio zakunywa, kutoka, kuvaa vizuri na kula kuku, nyama na pilau.

Sio sawa.
Nikuulize: siku kuu na siku ya kawaida wewe unaona ziko sawa? Kama zingekuwa sawa hizo zingine zisingeitwa siku kuu. Hata kwenye nyumba za ibada kuna tofauti ya ibada siku za kawaida na siku kuu za matukio ya kidini.

Tofauti lazima iwepo.
 
Daaahh nimecheka sana, sijui huwa unafikiria nini 😂😂😂😂🙌🏾🙌🏾
Hajafikiria bali umependa kwakuwa una personal interest labda na yeye mtoa comment au na wewe ndio unapendeza siku ya sikukuu.
 
Jana kwenye sikukuu ya Pasaka na Eid pia nishamuandalia nguo 3 me mwenyewe ninazo 3 pia kwa ajili ya Eid,

Utamaduni wa nguo mpya, pilau na biriyani, vyombo vizuri hauwezi kuisha sijui kama unasemea familia za wapi huko
Then ni swala la muda tu. Wala sio utamaduni mbaya ila sasa hivi tuko busy sana na mambo mengine mambo ya kuzingatia sikukuu na vikorombwezo vyake mtabaki nayo wanawake na itafika kipindi mtayaacha
 
Nikuulize: siku kuu na siku ya kawaida wewe unaona ziko sawa? Kama zingekuwa sawa hizo zingine zisingeitwa siku kuu. Hata kwenye nyumba za ibada kuna tofauti ya ibada siku za kawaida na siku kuu za matukio ya kidini.

Tofauti lazima iwepo.
Ziko sawa mkuu, jua huchomoza asubuhi na kuzama jioni, masaa ni yale yale. Je unawezaje kusema haziko sawa?
 
Heri ya Pasaka.

Iko hivi, imekuwa kama tamaduni kwetu kuwa siku za sikukuu ndio mtu atavaa vizuri, atakula vizuri na atatoka out.

Jana wakati natoka kwenye mishe zangu nikamuita boda wangu anipeleke home nikaangalie chama langu Liverpool likimenyana na Arsenal.

Jamaa kafika asee alikuwa amevaa amependeza nguo mpya mpya (sio kawaida yake huwa sio msafi sana namtumia tu kwakuwa ni mwaminifu).

Jana yake usiku (juzi) alinipigia kuniomba nimtumie namba ya jamaa yangu ambae huwa ananiuzia kuku wa kienyeji. Akaniambia "bro naomba namba ya yule jamaa wa kuku nimeipoteza nataka home nao wale kuku hii sikukuu"

Sasa jana wakati ananipeleka home njiani ikawa kero kwa kuwa watoto wanakimbia kimbia hovyo barabarani na watu wazima wamejaa sio kawaida. Nikajua tu shida ni hii sikukuu.

Nadhani tuwe na utamaduni wa kujipenda, kula vizuri na kutoka mara kwa mara siku zisizo za sikukuu.

Mimi jana nimerudi zangu home nikala matunda yangu na kulala lakini hizi siku kuna watu wanazichukulia ndio siku za kulewa, kutoka, kufanya ngono na kuvaa vizuri jambo ambalo mimi naona sio sawa kabisa.

Hizi siku huwa ndio siku zenye vurugu nyingi. Ambae hajawahi kunywa atakunywa, wasiotoka watatoka kwahiyo kero ni nyingi. Lakini yote husabaishwa na utamaaduni mbovu kuwa siku za sikukuu ndio zakunywa, kutoka, kuvaa vizuri na kula kuku, nyama na pilau.

Sio sawa.
Kufanya hivyo sio kwamba watu wameamua bali kunasababishwa na hali ya umasikini....
Watu hawana uwezo wa kupanga hayo matukio ya kutoka mara kwa mara.
Uchumi wetu bado upo chini sana na hata watu ulio watolea mifano wote wana uchumi mdogo
Ukipata nafasi soma " Maslow's Hierarchy of Needs" utaelewa ninachosema
Siku uchumi wa mtu ukitengemaa, hata akienda kwenye Sherehe ya harusi wala hatawazia kula/ kunywa; hata akipata maji nusu lita ya bakhresa ataona yanatosha sana; na ni kwa sababu ana uwezo wa kula anachotaka na sio kula anachopata. Unakuta Harusi wamepika buffet (bufee) wakati wewe unawazia Pizza ambayo unauwezo wa kuinunua ukitoka hapo
 
Kuichukulia sikukuu kama ni siku ya kawaida si sawa kwa sababu ni siku ambayo imetengwa kwa kusherehekea kitu flani lakini pia kila mtu anakuwa free hivyo, kujumuika ndugu, familia na marafiki ni jambo zuri..

Kuna watu kweli mwaka mzima anakuwa busy na holliday season anakuwa free, hakuna ubaya wa kufanya vitu ambavyo huwa hawafanyi

Labda hiyo ya kununua nguo mota kwa mtu mzima 😂😂
 
Then ni swala la muda tu. Wala sio utamaduni mbaya ila sasa hivi tuko busy sana na mambo mengine mambo ya kuzingatia sikukuu na vikorombwezo vyake mtabaki nayo wanawake na itafika kipindi mtayaacha
Hata miaka ya zamani wakina Mama ndio walikua busy na mambo ya sikukuu na wakina Baba walitafuta kuleta nyumbani,
Sijajua wanaume wa siku hizi mna shida gani katika suala la kuhudumia familia tena chache tu mnakimbilia ubusy utakua busy bila kurudisha huduma nyumbani watoto wakavaa nguo mpya, wakala pilau kuku na soda na mama zao wakavaa vitenge vya Wax!
 
Jana kwenye sikukuu ya Pasaka na Eid pia nishamuandalia nguo 3 me mwenyewe ninazo 3 pia kwa ajili ya Eid,

Utamaduni wa nguo mpya, pilau na biriyani, vyombo vizuri hauwezi kuisha sijui kama unasemea familia za wapi huko
Huo ni ulimbukeni, kujipenda siku za sikukuu ambazo kwa mwaka ni chini ya siku tano au sita na kuishi kwa shida siku nyingine zote ni tatizo.
 
Ziko sawa mkuu, jua huchomoza asubuhi na kuzama jioni, masaa ni yale yale. Je unawezaje kusema haziko sawa?
Kwa jibu hili ni wazi unasumbuliwa na upweke au maisha bado hayajakaa sawa, piga kazi mwanaume acha kulia lia
 
Kuichukulia sikukuu kama ni siku ya kawaida si sawa kwa sababu ni siku ambayo imetengwa kwa kusherehekea kitu flani lakini pia kila mtu anakuwa free hivyo, kujumuika ndugu, familia na marafiki ni jambo zuri..

Kuna watu kweli mwaka mzima anakuwa busy na holliday season anakuwa free, hakuna ubaya wa kufanya vitu ambavyo huwa hawafanyi

Labda hiyo ya kununua nguo mota kwa mtu mzima 😂😂
Inategemea hiyo siku ni siku ya nini. Sasa siku ya kuzaliwa Mtume au Yesu inawezaje kufanywa siku ya kula vizuri na kula vizuri na kutoka out na kufanya ngono?
 
Hajafikiria bali umependa kwakuwa una personal interest labda na yeye mtoa comment au na wewe ndio unapendeza siku ya sikukuu.
Kaka no hard feelings, Mimi nimecomment tu 😁

Sometimes kuwaamulia watu namna ya kuishi inaweza isiwe sawa. Imagine boda wako labda siku zote anaipa familia kuku wa kisasa kutokana na kipato Ila jana kaamua kuwafanyia kitu special

Kwa nini usiichukulie kama baba wa familia anaeonesha upendo kwa familia yake kuliko kumtwika jukumu la kufanya unayoyafanya wakati kipato ni tofauti
 
Kwa jibu hili ni wazi unasumbuliwa na upweke au maisha bado hayajakaa sawa, piga kazi mwanaume acha kulia lia
Kuhusu mimi hunifahamu lakini naomba tujikite kwenye hoja ya msingi. Usianze ku commit logical fallacies (ad hominem)
 
Back
Top Bottom