Tujenge utamaduni wa kupendeza (kujipenda), kutoka out na kula vizuri

Kwamba kwa kuwa siku zingne unakulaga poa,unavaa poa na kujivinjari basi sikukuu ule ugali matembere?....SIKU~KUU itabak kuwa special day tu hata ukifanya hayo kila siku!
Hapana sina maana hiyo. Wengi wanajitesa ku save kwaajili ya sikukuu ndio waonekane
 
Jana kwenye sikukuu ya Pasaka na Eid pia nishamuandalia nguo 3 me mwenyewe ninazo 3 pia kwa ajili ya Eid,

Utamaduni wa nguo mpya, pilau na biriyani, vyombo vizuri hauwezi kuisha sijui kama unasemea familia za wapi huko
 
Hahahahaha kaumia kuona Boda kala kuku wa kienyeji halafu yeye kala matunda ya buku jero na bado buku ya nauli kamuachia
Huyu boda wangu ananiletea kuku wawili wa kienyeji (20000 kila mmoja) kila baada ya week mbili. Simuonei wivu mkuu kwakuwa mimi sio hohehahe
 
Tutembeleane kila siku sio siku kuu tu. Unajua wewe mantiki ya mada yangu hujaelewa vizuri.

Tufanye haya yote siku yoyote sio kusubiri sikukuu.
 
Kila mtu afanye atakalo.

Mkuu una gubu sana kisa boda boda wako alipendeza kukuzidi na pilau kala kuku sikukuu wakati boss umeishia kula matunda
Daaahh nimecheka sana, sijui huwa unafikiria nini πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎ
 
Ni kweli mkuu. Mimi ni mmoja wao.
 
Nikuulize: siku kuu na siku ya kawaida wewe unaona ziko sawa? Kama zingekuwa sawa hizo zingine zisingeitwa siku kuu. Hata kwenye nyumba za ibada kuna tofauti ya ibada siku za kawaida na siku kuu za matukio ya kidini.

Tofauti lazima iwepo.
 
Daaahh nimecheka sana, sijui huwa unafikiria nini πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ™ŒπŸΎπŸ™ŒπŸΎ
Hajafikiria bali umependa kwakuwa una personal interest labda na yeye mtoa comment au na wewe ndio unapendeza siku ya sikukuu.
 
Jana kwenye sikukuu ya Pasaka na Eid pia nishamuandalia nguo 3 me mwenyewe ninazo 3 pia kwa ajili ya Eid,

Utamaduni wa nguo mpya, pilau na biriyani, vyombo vizuri hauwezi kuisha sijui kama unasemea familia za wapi huko
Then ni swala la muda tu. Wala sio utamaduni mbaya ila sasa hivi tuko busy sana na mambo mengine mambo ya kuzingatia sikukuu na vikorombwezo vyake mtabaki nayo wanawake na itafika kipindi mtayaacha
 
Nikuulize: siku kuu na siku ya kawaida wewe unaona ziko sawa? Kama zingekuwa sawa hizo zingine zisingeitwa siku kuu. Hata kwenye nyumba za ibada kuna tofauti ya ibada siku za kawaida na siku kuu za matukio ya kidini.

Tofauti lazima iwepo.
Ziko sawa mkuu, jua huchomoza asubuhi na kuzama jioni, masaa ni yale yale. Je unawezaje kusema haziko sawa?
 
Kufanya hivyo sio kwamba watu wameamua bali kunasababishwa na hali ya umasikini....
Watu hawana uwezo wa kupanga hayo matukio ya kutoka mara kwa mara.
Uchumi wetu bado upo chini sana na hata watu ulio watolea mifano wote wana uchumi mdogo
Ukipata nafasi soma " Maslow's Hierarchy of Needs" utaelewa ninachosema
Siku uchumi wa mtu ukitengemaa, hata akienda kwenye Sherehe ya harusi wala hatawazia kula/ kunywa; hata akipata maji nusu lita ya bakhresa ataona yanatosha sana; na ni kwa sababu ana uwezo wa kula anachotaka na sio kula anachopata. Unakuta Harusi wamepika buffet (bufee) wakati wewe unawazia Pizza ambayo unauwezo wa kuinunua ukitoka hapo
 
Kuichukulia sikukuu kama ni siku ya kawaida si sawa kwa sababu ni siku ambayo imetengwa kwa kusherehekea kitu flani lakini pia kila mtu anakuwa free hivyo, kujumuika ndugu, familia na marafiki ni jambo zuri..

Kuna watu kweli mwaka mzima anakuwa busy na holliday season anakuwa free, hakuna ubaya wa kufanya vitu ambavyo huwa hawafanyi

Labda hiyo ya kununua nguo mota kwa mtu mzima πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Then ni swala la muda tu. Wala sio utamaduni mbaya ila sasa hivi tuko busy sana na mambo mengine mambo ya kuzingatia sikukuu na vikorombwezo vyake mtabaki nayo wanawake na itafika kipindi mtayaacha
Hata miaka ya zamani wakina Mama ndio walikua busy na mambo ya sikukuu na wakina Baba walitafuta kuleta nyumbani,
Sijajua wanaume wa siku hizi mna shida gani katika suala la kuhudumia familia tena chache tu mnakimbilia ubusy utakua busy bila kurudisha huduma nyumbani watoto wakavaa nguo mpya, wakala pilau kuku na soda na mama zao wakavaa vitenge vya Wax!
 
Jana kwenye sikukuu ya Pasaka na Eid pia nishamuandalia nguo 3 me mwenyewe ninazo 3 pia kwa ajili ya Eid,

Utamaduni wa nguo mpya, pilau na biriyani, vyombo vizuri hauwezi kuisha sijui kama unasemea familia za wapi huko
Huo ni ulimbukeni, kujipenda siku za sikukuu ambazo kwa mwaka ni chini ya siku tano au sita na kuishi kwa shida siku nyingine zote ni tatizo.
 
Ziko sawa mkuu, jua huchomoza asubuhi na kuzama jioni, masaa ni yale yale. Je unawezaje kusema haziko sawa?
Kwa jibu hili ni wazi unasumbuliwa na upweke au maisha bado hayajakaa sawa, piga kazi mwanaume acha kulia lia
 
Inategemea hiyo siku ni siku ya nini. Sasa siku ya kuzaliwa Mtume au Yesu inawezaje kufanywa siku ya kula vizuri na kula vizuri na kutoka out na kufanya ngono?
 
Hajafikiria bali umependa kwakuwa una personal interest labda na yeye mtoa comment au na wewe ndio unapendeza siku ya sikukuu.
Kaka no hard feelings, Mimi nimecomment tu 😁

Sometimes kuwaamulia watu namna ya kuishi inaweza isiwe sawa. Imagine boda wako labda siku zote anaipa familia kuku wa kisasa kutokana na kipato Ila jana kaamua kuwafanyia kitu special

Kwa nini usiichukulie kama baba wa familia anaeonesha upendo kwa familia yake kuliko kumtwika jukumu la kufanya unayoyafanya wakati kipato ni tofauti
 
Kwa jibu hili ni wazi unasumbuliwa na upweke au maisha bado hayajakaa sawa, piga kazi mwanaume acha kulia lia
Kuhusu mimi hunifahamu lakini naomba tujikite kwenye hoja ya msingi. Usianze ku commit logical fallacies (ad hominem)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…