Tujenge utamaduni wa kupendeza (kujipenda), kutoka out na kula vizuri

Huo ni ulimbukeni, kujipenda siku za sikukuu ambazo kwa mwaka ni chini ya siku tano au sita na kuishi kwa shida siku nyingine zote ni tatizo.
Tafuta pesa bro,
Utafurahi sikukuu ndio maana ikaitwa sikukuu [emoji3]
Yaani Mtu afunge siku 40 au mwingine siku 30 halafu unataka sikukuu ale matunda alale weee hebu kua na aibu kidogo,

Jana tu mwenye nyumba wangu katuchinjia kuku wa kienyeji watatu, ujue sikukuu ilivyo na raha na furaha, eid tutachinja Mbuzi wawili na Kuku kadhaa nitakualika [emoji1787][emoji1787]
 
Pesa naitafuta mkuu ndio maana jana nikaenda kwenye mishe zangu kuingiza hela
 
Mimi mwenyewe jana na leo kwangu wamekula mikuku na minyama ya mbuzi .Ila kuanzia kesho na kuendelea nimewaambia kabisa wafunge mikanda budget ya vitafunwa kwa kuanzia nimeifuta watakunywa uji bila kitafunwa chochote na nimewaambia sitaishia hapo.
 
Kadhani Boda kununua Kuku jana basi siku zote familia ya Boda wanakula matembele,
tena sio Kuku wa kisasa huenda hiyo jana sehemu ambayo huchukua kuku wa kienyeji waliisha ndio maana akampigia yeye ampe namba ya huyo mtu mwingine,

Huyu mtoa mada sio tu mpweke ana kiroho cha korosho pia.
 
Si kila mtu afanye kinachompendeza [emoji2368]
 
Pesa naitafuta mkuu ndio maana jana nikaenda kwenye mishe zangu kuingiza hela
Pesa ulivyoipata ukala matunda ukalala,
Huzikwi nazo Bro we tumiaaaaaaaa,
Mada yako inafaa ikurudie wewe, jipende, jitoe out [emoji38]
 
Huyu boda wangu ananiletea kuku wawili wa kienyeji (20000 kila mmoja) kila baada ya week mbili. Simuonei wivu mkuu kwakuwa mimi sio hohehahe

Yaani unakula kuku wa kienyeji wanne kwa mwezi[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Wakati kuku wa kienyeji ni mboga Kama maharage tu
Unaweza kula daily
 
Msimsagie kunguni sana πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Familia inahudumiea wakati wote ila ikifika sikukuu kwakua mnapenda makubwa mnasema haihudumiwi lakini siku nyingine watoto wanaenda shule wamevaa vizuri na mahitaji yote ya muhimu ila ikifika sikukuu hela ikipungua kidogo zinakuja kauli baba fulani hahudumii familia yake
 
Mimi nafikiri hiyo inatoka na umri na exposure ya mtu Mimi Jana nmelala the whole day na ata sijatoka nmechukulia siku ya Kawaida mpaka kuna muda nilikuwa nasahau kama Jana ni pasaka kila siku Mimi kwangu ni sikukuu siku najiwenga natoka zangu nafanya vurugu

Sent from my Nokia C2 using JamiiForums mobile app
 
Yaani unakula kuku wa kienyeji wanne kwa mwezi[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Wakati kuku wa kienyeji ni mboga Kama maharage tu
Unaweza kula daily
Nakula na vitu vingine mkuu. Sio sifa kula kuku kila siku, kuna samaki, maharage, mbuzi, ng'ombe' maini. Halafu mimi ni bachelor na sipiki kila siku
 
Pesa ulivyoipata ukala matunda ukalala,
Huzikwi nazo Bro we tumiaaaaaaaa,
Mada yako inafaa ikurudie wewe, jipende, jitoe out [emoji38]
Mimi najipenda sana. Nakula vizuri sana. Jana nimekula matunda kwakuwa nimechelewa kutoka kwenye mishe nikafikia home moja kwa moja nikakata tikiti nanasi papai na parachichi nikala nikalala. Ningewahi kutoka ningepika chakula kama kawaida yangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…