Tujiandae na Vita ya Tatu ya Dunia

Tujiandae na Vita ya Tatu ya Dunia

Ni muda mrefu sasa tangu vita ya pili ya dunia ilipoisha mataifa yaliheshimiana kwa muda sasa wanadhani heshima imepungua tena. Wange weka vipindi kila baada ya mika 50 tunachapana tena, heshima inge kuwa inakuwepo kwa muda mrefu.

Kuna watu tutakufa ama kwa maradhi, njaa, au vita yenyewe lakini watakao baki wataheshimiana. Kizazi hiki hakina kumbukumbu ndio maana unaoana yoote haya.

Vita ni nzuri sana ukiwa unaangalia movie na kusikia kwenye redio, na kuangalia kwenye television kama hivi sasa. lakini timbwili likiwa mlangoni kwako, hutotamani vita milele.

Mimi naunga mkono vita ya Hamas na IDF kwasababu nafahamu eneo lile Diplomasia iliisha fail, kilichobaki ni tumpate mbabe wa kivita, na huyo atawale eneo lote. Watanuna na kulia lakini hiyo pekee ndiyo suluhu iliyopo pale.

Palestine wana taka Israel aondoke, na Israel anapigania existance yake. Kuna vi-siasa viingi lakini bottom ni hilo. Na kwakuwa hakuna suluhu ya mezani inayokubalika kwa pande zote mbili mi naomaba waendelee kutwangana tu.
Atakayeshinda ajitwalie lote.
 
Lile bomu la nyuklia la hiroshima lilipokuwa likishuka lilitua kwny kichwa cha jamaa anaitwa Gemba Minamata akiwa anaoga bafuni akafanyiwa kitu kwenye chemistry inaitwa SUBLIMATION yaani direct change from solid to gas or viceversa huko hatuwezi kurudi
 
Kila dalili zinaonesha tunaelekea kwenye vita kuu ya tatu ya dunia. Haya yatatukia kabla kizazi hiki hakijapita

Safari hii, Afrika ndiyo uwanja wa mapambano. Kutakuwa na block 2 zitakazopambania maslahi yao.

Block ya kwanza: NATO na washirika wote wa magharibi.

Block ya pili: Urusi + China + Iran + baadhi ya members wa BRICKS

SABABU ZA VITA
Shamba la bibi la malighafi ambalo ni AFRIKA.

Hakuna atakayejali ustawi wala maslahi ya manamba wa shamba hilo (Afrika). Ikumbukwe kwamba Afrika haijavumbuliwa vya kutosha. Maisha ya ulimwengu yanategemea uwepo wa bara hili jeusi

Ole wao kwa watakaokuwa na tumbo la utungu siku hizo.

Tumuombe Mungu aepushe kikombe hiki.
 
Marekan ili aendelee ku maintain hegemony yake globally anahitaji Vita ya Tatu ya Dunia.

Ukiona chokochoko zoote kuanzia UCHINA na Taiwan, URUSI -Ukraine , zote hizi ni Kwa sababu anahitaji Vita

Kwa Marekan Vita, humneesha Kiuchumi na Kiutawala.
 
Kila dalili zinaonesha tunaelekea kwenye vita kuu ya tatu ya dunia. Haya yatatukia kabla kizazi hiki hakijapita

Safari hii, Afrika ndiyo uwanja wa mapambano. Kutakuwa na block 2 zitakazopambania maslahi yao.

Block ya kwanza: NATO na washirika wote wa magharibi.

Block ya pili: Urusi + China + Iran + baadhi ya members wa BRICKS

SABABU ZA VITA
Shamba la bibi la malighafi ambalo ni AFRIKA.

Hakuna atakayejali ustawi wala maslahi ya manamba wa shamba hilo (Afrika). Ikumbukwe kwamba Afrika haijavumbuliwa vya kutosha. Maisha ya ulimwengu yanategemea uwepo wa bara hili jeusi

Ole wao kwa watakaokuwa na tumbo la utungu siku hizo.

Tumuombe Mungu aepushe kikombe hiki.
Sidhani kama hii itawafanya wapigane vita maana wanaitafuna hata bila vita
 
Marekan ili aendelee ku maintain hegemony yake globally anahitaji Vita ya Tatu ya Dunia.

Ukiona chokochoko zoote kuanzia UCHINA na Taiwan, URUSI -Ukraine , zote hizi ni Kwa sababu anahitaji Vita

Kwa Marekan Vita, humneesha Kiuchumi na Kiutawala.
Olympus must fall this time
 
Habari wakuu zangu,

Kuna msemo unasema "Jela hakuna mateso ila wanao leta mateso jela ni wajelajela wenyewe."

Hivyo hivyo duniani ni mahala salama, pana maji, vyakula ardhi nzuri, na vyote Mungu alitoa bure. Yaani ule bure, unywe bure, ujenge popote bure, uwinde bure, uvue samaki was baharini bure nk.

Vyoote Mungu alitoa bure kabisa kusudi maisha yawe rahisi na yenye fraha duniani kote, lakini kuna watu wachache walio barikiwa roho za kibinafsi, makatiri, wasiyoipenda katu furaha wala amani wasio iwazia mema dunia yetu nzuri, wala uzao wake wa asili.

Wakajimilikisha mito na maziwa ili wauze maji na kuwalipisha ushuru wavua samaki na wapita na meli juu ya bahari mito na maziwa.

Wakajimilikisha aldhi ili wawalipishe ushuru wakulima walimao juu ya nchi na kuwauzia ardhi wale watakao kujenga na kuishi na wale wafugaji na hata wale wachimbaji wa madini ardhini kama dhahabu, chuma, nk.

Wakajimilikisha anga ili walipwe ushuru kwa wale wapitao na vyombo vya angani. Hawakuishia hapo, wakafikia hatua mpaka ya kutaka ushuru kwa wale walitangazao neno la Mungu, Mungu muumba mbingu na nchi!

Kwa matendo yao wakaipandisha pesa thamani, pesa ikawa na nguvu kuliko utu, pesa ikatawala ikazisimamisha na kuziangusha tawala, ikawasimamisha na kuwaangusha wafalme.

Pesa ikaharibu kabisa nguvu ya upendo kwa dunia yetu pendwa. Wasio na pesa wakakosa ardhi, wasio napesa wakakosa Uhuru, wasio na pesa wakakosa maji, wasio na pesa wakakosa chakula, paku lala, elimu, mavazi, nk, watu wakaitambua thamani ya pesa, wakapania kuitafuta kwa njia yoyote ili wapate heshima, makazi, chakula, maji, mavazi nk.

Kadri watu walivyotafuta pesa kwa nguvu na kwa akili zao zote, wale walioumiliki utajiri wote wa dunia pesa zote za inchi wakapata hofu wakaanza kuwaita; majambazi, matapeli, wakabaji, ombaomba, maskini, mafukara, wadangaji, ma bar maid, wapasua mbao, makapuku wanuka kwapa.

Hawakuishia hapo wakawaita magaidi wakawaua kwa risasi, mabomu, visu, mafuta, magonjwa ya zinaa, nyuklia nk, hawakujipa muda kujiuliza kwanini ujambazi umeshamili, kwanini ngono zimeshamili, kwanini wa watu wanauwana, kwanini migogoro ya ardhi imeshamili!

Hawa kuwa na muda huo, walichojari ni kuongeza ulinzi juu ya mali zao, familia zao, pesa zao, na kuongeza ufanisi katika kutengeneza silaha nzito kwa ajili ya kulinda maslahi yao na utajiri wao.

Leo hii dunia imekuwa uwanja wa vita, magonjwa, visasi, shida, dhiki, ukame, japo maji yapo, kwani hawako tayari kuhakikisha maji yanapatikana kila mahari kwa kuhofia watashindwa kuuza maji ya chupa, wala hawako taya rikuhakikisha kila mmoja ana nyumba ya kulala kwa kuhofia watapoteza mapato kwenye nyumba za kupanga.

Wala hawako tayari kuzalisha umeme wa kutosha kwa kuhofia watashindwa kuuza magenerator, pesa imetufikisha pabaya tumekuwa wanyama! Natokwa na machozi nikiitazama Sudan, Congo, Ukraine, leo hii Palestina na Israel.

Naona kuna mama, watoto, na wazee, wakati wanaoupitia ni mgumu sana na hauelezeki. Yote haya yanatokea kwa sababu ya ubinafsi wa watu wachache ili wauze silaha zao na kuzitangaza biashara zao. Mambo haya yanatupeleka kuelekea Vita ya Tatu ya Dunia kwani nvita zote msingi wake ni ubinafsi.

Vita hii itaanzia pale Irani itakapoingilia kati, bila shaka Mmisri hatasita na vipi nchi nyingine za kiislamu kama Saudi Arabia, nk, na huku pembeni Muingereza na Mjerumani na washirika wengine hawatakaa kimya.

Kwahiyo tujiandae gharama za maisha kupanda zaidi.
Maneno mengi pumba tupu
 
Mbona sijakuelewa vizuri kiongozi!! Haya mamno ya kui- equate uwwzo wa kiuchumi na masuala ya kushinda vita ndio huwa siuelewi, kila siku huwa nawahoji hivi GDP ya Merikani wakati alipo vamia/jiingiza kwenye vita na VietNam ya Kasikazini GDP ya North VietNam ilikuwa ya kiwango gani???

Bottom line is: kuwa na Uchumi mkubwa sio passport ya kushinda vita - tulishuhudia jinsi Meeikani ilivyo dhalilishwa na Taifa dogo la VietNam Kaskazini sasa hizo zillion USD ya uchumi wa Merikani na zana za kivita ziliwasaidia nini?? Kuhusu Ukraine, Urusi ilisha jipanga kwa muaka mingi jinsi ya lu-deal na njama za kutaka kuitumia Ukraine ili wadhoofishe kijeshi, lakini wawahakikisheni nja hizo hazitafamikiwa Urusi itahibuka kidedea wayakaopata shida na taabu ni nchi za Ulaya zilizokuwa zina msupport Zelesky kwa niaba ya Merikani.
hawa nchi za magharibi ni kuwanyima gesi tuu wafe na baridi
 
"Sheikh mmja alikuwa anasema,"Kila mara tunasikia ,'Watoto wa siku hizi walevi,watoto wa siku hizi wanavuta bangi'"
Sasa,yule Sheikh akauliza,"Huyu 'Siku Hizi' ana watoto wangapi? Kwa sababu kila mtaa unaopita unasikia kuhusu watoto wa Siku Hizi".
Watoto wa Siku Hizi wapo wengi na sasa miaka mingi imepita na watoto wa Siku Hizi wamekuwa mawaziri,wamekuwa wakuu wa mikoa,wamekuwa wakuu wa wilaya( duniani kote).
Kwa hiyo upo uwezekano wa kutokea ww111.
 
Back
Top Bottom