Je, wafahamu ni kipindi gani hali ya kupoteza nguvu na kuanguka kwa dini ulaya kilianza miaka ipi na karne gani ?
Simple fact:
Tujifunze, wenda hali hii ya sasa ya mataifa mengi ya ulaya kuteteleka katika mambo ya imani na dini yakushanganza na kujenga maswali mengi katika ufahamu wako kuhusu sababu nini na lini hali hii ilianza.
AGE OF REASON
Hiki ndicho kipindi ulaya ili shuhudia mabadiliko makubwa ya kiimani pia kiutawala.
Kipi hiki imani na dini zilipitia wakati mgumu uliopelekea kuanguka kwa kiasi kikubwa katika mataifa mbalimbali ya ulaya tofauti na nguvu iliyokuwa nayo mwanzo
Kipindi hiki kilianza mwanzo mwa karne ya 17 kwenda karne ya 18. Kipindi hiki kilisisitiza matumizi ya akili katika kuchambua masuala ya kidini na kuepesha matumizi ya Imani kwa kiwango kikubwa.
Hiki ndicho kipindi sayansi na utumizi wa falsafa ulichipukia kwa kasi sana ndani ya ulaya. Sayansi na falsafa za kimaisha ziliathiri dini na imani kwa kiwango kikubwa ulaya.
Mapinduzi ya sayansi na teknolojia na uhuru binafsi ulichukua nafasi kubwa kipindi hiki, wanasayansi wengi wakubwa ulaya na duniani walianza kuonekana katika kipindi hiki.
Somo fupi la leo.