Tujifunze kitu kwa misiba ya vigogo hawa na idadi ya watoto

Tujifunze kitu kwa misiba ya vigogo hawa na idadi ya watoto

Vijana wanajiamini wapo vizuri katika lugha n.k natumai watoto wangu pia nitahakikisha wanapata Elimu Bora Nje ya Nchi pia ..

Watanzania tunakosa Nafasi nzuri sababu ya Lugha
Kwenye lugha hapo nimekuelewa.viongozi wa Tanzania wanasisitiza kiswahili kifundishwe darasa la kwanza Hadi chuo kikuu lakini watoto wao wanaowapeleka international ambako lugha za kimataifa ni lazima
 
Kwani ukilia kwa kuzimia ndo nini yaani? Walishalia kidogo inatosha.
Sio lazima ulie mimi sijasema lia nimesema kwenye msiba hata chozi lisipotoka sura yako haiwezi kuficha huzuni hawa utasema kitu cha kawaida tu bado watoto hawa ndio kujizuia ngumu mtu mzima unaweza kujikaza.
 
Tahadhari kwa wazazi uzungu ukizidi sana ndio haya matokeo, ujasiri unaotoa wapi mtoto mdogo unamzika Baba yako uneongelea mziki wa Prof J, sisemi alie agalegale hapana ila sisi wa Africa wazazi tukipoteza ni pigo haijalishi wewe ni nani ila wenzetu naona mpaka tabia wanaiga za huko tuliona hata kwenye msiba wa Mafuru sijui labda ndio watoto wa kileo lakini mimi nilimzika mzazi wangu kwa uchungu hata kama sikulia hadharani lakini sura yangu sikuweza kuficha dhoruba.
Kule kwetu kusini usipolia msibabi unaitwa mchawi. Na watoto na mke mpaka wanashikiliwa kabisa. Hao pesa za baba yao zimewavuruga. Hawawazi msiba wanawaza kumiliki.
 
LAKINI nahisi masikini kuzaa watoto wengi inaweza kuwa sawa.... yaani, sio kitu kibaya moja kwa moja

kujenga hoja ndo ngumu sasa
Haya tufanye maskini kapanga chumba kimoja na sebule, ana watoto sita, anafanya kazi kiwandani analipwa elfu7 kwa siku, hapo hata kiwanja Hana, HUJAONA tuu shida hapo?
 
Nipo nacheki hapa msiba WA Ndugulile, kuacha watoto wawili tuu, pamoja alikua na uwezo WA kipesa na cheo lakini kaishia kwenye watoto wawili, watoto wawili hawa naona kawakuza na kuwasomesha kwenye shule za gharama inawezekana nnje ya nchi maana hata Kiswahili Chao NI broken Sana wanakua kama sio watanzania.

Lawrence mafuru nae nadhani aliacha watoto wawili tuu.

Swali kwa makapuku wenzangu, hivi Sisi maskini tunazaa watoto wengi ili iweje? na utakuta pengne hata uwezo wa kuwahudumia tuu kikamilifu kwenye elimu na gharama za kila siku hatuwezi, nini maana ya hii?

Nahis NI vizuri kuzaa watoto kulingana na kipato chako, ambao utawamudu vizuri, utakaowapa elimu ya uhakika sio hii ya kuunga unga.

Sisi maskini tunawaza eti tukizaa watoto wengi ndio hao badae watatusaidia, wewe mzazi somesha mtoto, hudumia kwa kadiri ya uwezo wako maana NI jukumu lako, badae akipata maisha mazuri NI yeye sasa atajua atakusaidiaje, ndio ile utakuta wazazi wananunia wakwe zao wanaona kama wao ndio wanafanya wasipewe pesa na mtoto wao.

Tuzae Kwa mahesabu, utakuta mtu ana watoto wanne, halafu kapanga chumba na sebule, sasa jiulize hapo ndani wanaishije, tuwekeze nguvu kwenye kujenga uchumi Kwanza na kuzaa kwa akili.

View attachment 3167382
Tajiri kikwete anawatoto wangapi?
 
Sio lazima ulie mimi sijasema lia nimesema kwenye msiba hata chozi lisipotoka sura yako haiwezi kuficha huzuni hawa utasema kitu cha kawaida tu bado watoto hawa ndio kujizuia ngumu mtu mzima unaweza kujikaza.
Unadhani ni kwanini wapo hivyo?
 
Back
Top Bottom