TUJIKUMBUSHE: Timu Maarufu za Ndondo kutoka mitaa yetu

Jamal Mnyate tulicheza naye sana. Kuna kipindi alikuwa anasoma Jabal Hila Sekondari. Mvumi naikumbuka sana hiyo.
Kilosa Boys ya kina Juma Luizio,Mwaikimba,Malima na Mzamiru Yassin ulipata kusikia habari zake ilivyosumbua wilaya ya kilosa na ligi za ndondo Kilosa.

Mzamiru alimpiga Chenga Maduba wa Orlando siku ya fainali mpaka mkongwe Maduba akakaa chini,Goli ya ushindi ilifungwa na Juma Luizio bonge la shuti nje ya 18 Uwanja wa shule ya msingi Ludewa Batini
 
Kajima Rangers SC Ubungo Riverside miaka 2006.
Captain Salehe Ibrahim Tendega ( Transit Camp 2021-R.I.P) Ndani kulikuwa na vijana wa kipingu wengi mno kama kina Beka, Haruna, Pompi, Lameki mdudu, Yohana Nginja nginja, Mika Mwamba (Mzee wa Mawe).
 
Sikuwa naifahamu hiyo bro. Ndondo ilikuwa ina wachezaji bora sana kwa kweli.
 
Kajima Rangers SC Ubungo Riverside miaka 2006.
Captain Salehe Ibrahim Tendega ( Transit Camp 2021-R.I.P) Ndani kulikuwa na vijana wa kipingu wengi mno kama kina Beka, Haruna, Pompi, Lameki mdudu, Yohana Nginja nginja, Mika Mwamba (Mzee wa Mawe).
Mzee wa Mawe inamaanisha alikuwa anapiga makiki kama mawe. Yeye anakandamiza mawe tu. Kuna mmoja alikuwa anaitwa krosi dongo. Yeye hajui kupiga krosi taratibu ila yeye kila krosi ni dongo tu. Yaani jamaa anakandamiza mawe tu.
 
Akiweka Krosi tukiweka kichwa lazima uugulie.
Yeah huyo mwamba alikuwa akipokea mpira mita 28 kutoka Goli lilipo kipa akague kasimamia wapi anapiga balaa.
 
Akiweka Krosi tukiweka kichwa lazima uugulie.
Yeah huyo mwamba alikuwa akipokea mpira mita 28 kutoka Goli lilipo kipa akague kasimamia wapi anapiga balaa.
Hahaaaa kuna mmoja tulicheza naye akitokea Town Stars ya Pale Wami Dakawa yeye alikuwa anaitwa Salum "Kona Goli" yeye alikuwa anatumia mguu wa kulia. Kila akienda kupiga kona upande wa Kushoto ujue ni Goli. Mimi nilikuwa napiga free kiki matata sana. Hata ukuta ukae hatua tano au sita nilikuwa nauvusha mpira juu ya ukuta na ni lazima iwepo kunyavu. Huwa naangalia timu zetu zinavyopoteza nafasi za magoli kwa free kiki huwa nawaambia wanangu, ningekuwa mimi hizi nafasi zote ni magoli.
 
Kwa nini hukuendelea kusukuma gozi la ng'ombe?
 
Free kick kama penati.... Ni Moja la eneo langu pendwa hilo la mpira iliyokufa ila Tz masters wa setpiecez wachache mno.
 
Kagera rangers, faru dume, Sinza stars, Linea Messina, afc leopard, nyarugusu, milambo ya Mburahati, Oman,
 
Huwaga nasikitika sana nikiona Ki, Chama na yule jamaa wa Azam wanapoteza hizo nafasi huwa nasikitika sana.
Wapiga free kick wazuri Huwa Wana accuracy kubwa za pasi ndefu.
Huku kwetu wanabahatisha na kila siku wakilala wakiamka kazi ni hy hy mpira tu ila bado quality duni.
 
Boom FC. Ilala moja.miaka imeenda sana. Walikua na Derby yao hawa jamaa na Ashanti. Hatari sanaKarume hiyo.
 
David Izengo alikuwa mtu haswaa, mimi binafsi sijaona hadi leo mtu alikuwa na kipaji kama yule jamaa, sema muda haukuwa rafiki kwake na nafikiri akishatangulia mbele ya haki
Pia ana mdogo wake anaitwa Denis Izengo nae alikuwa moto sanaa, alisomaga Dumila sec
Hawa wote walikuwa na vipaji vikubwa sana aisee, muda ukawakatili
Vp unamkumbuka ombopaa?
 
Hahaaaaa, unawafahamu hao. David kwangu mimi ni mchezaji bora kuwahi kumuona kwa macho yangu nchini Tanzania. Denis alikipigaga Under 18 ya Azam FC.
 
Hapana David Hajatangulia bro mbele ya haki bro. Mbona sijasikia hilo na huwa nawasiliana na Denis. Nafahamu aliyetangulia ni mdogo wake alikuwa anaitwa Robert Izengo aliyemfuatia David na wa mwisho ni Denis. Ngoja nimuulizie Denis
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…