Tujikumbushe vifo vilivyotokea Morogoro, JB na wenzake walipopigwa risasi na kufa papo hapo

Tujikumbushe vifo vilivyotokea Morogoro, JB na wenzake walipopigwa risasi na kufa papo hapo

Kama miaka kumi iliyopita kuna wafanyabiashara wa madini walikuwa nane walikuwa wanaenda Mahenge walipofika nanenane walimiminiwa risasi na Polisi wakidhaniwa ni majambazi akiwemo aliyekuoa mfadhili wa bendi nyingi za muziki mjini Darisalama aliyeitwa JB

Mnaokumbuka vizuri tukio hili mtukumbushe.
Kww hiyo wapipolambwa risasi dhahabu zao nani alizichukua?
 
Huyu mtoa mada katoa taarifa zisizo za kweli, JB na wenzake walikuwa majambazi kweli na waliwekewa mtego palepale Moro walipotaka kuiba sehemu. Hawakutokea Mahenge
Nakumbuka taarifa ya polisi ilisema walikuwa majambazi.
 
Jb alikuwa jambazi na tapeli ,ila polisi siku ile hawakuwa na huruma walipiga wote risasi nilishuhudia mpaka maiti mwanamke imetandikwa risasi za kutosha
Huyo mwanamke alikuwa mshenzi sana na alitafutwa muda mrefu . Enzi Ile majambazi wengi walikuwa maskani yao Morogoro, wakijificha vijijini ni ngumu kuwajua na ni karibu na town kwa hiyo wanakuja dar na kwengineko wanapiga tukio then wanakimbilia Moro.

Huyo mwanamke nadhani alitandikwa Shaba na Afande Sabasita huyu aliyejijengea kaburi maana nae alikuwa sniper mzuri sana kwa kutumia pistol maana huyo mwanamke alikuwa hawampati.
 
Jb alikuwa jambazi na tapeli ,ila polisi siku ile hawakuwa na huruma walipiga wote risasi nilishuhudia mpaka maiti mwanamke imetandikwa risasi za kutosha
Tukio la JB, huyo mwanamke jambazi na wenzao kuuawa mwaka huo linanikumbusha yafuatayo:
1. Onyesho la muziki lililoitwa BUWASHIBA likiwahusisha Bushoke, WASHIKAJI (kama kundi likiwahusisha Ismail ambaye kama sikosei kwa sasa yupo kwenye band ya Mrisho Mpoto na kijana mwingine jina limenitoka) na Banana Zoro. Onyesho hili lilifanyika ukumbi fulani uliokuwa pale Dar maeneo ya Sayansi ambao kama sikosei ulikuwa ukimilikiwa na mmiliki wa Clouds FM. Jina au neno BUWASHIBA liliwakilisha herufi za mwanzo za majina ya wanamuziki hao.
2. Tukio la ujambazi wa kutumia silaha kwenye maduka ya simu pale Mwenge ambapo ilidaiwa kiongozi wa majambazi hayo alikuwa ni mwanamke akitembeza njugu mawe kwa bunduki yake mithili ya komandoo.
3. Siku chache baadae JB, huyo mwanamke niliyemwelezea katika tukio la pili hapo juu na majambazi mengine yakaripotiwa kuuawa na polisi huko Morogoro. Picha ya huyo jambazi mwanamke aliyeuawa iliwekwa kwenye baadhi ya magazeti na mmoja wa watu wangu wa karibu sana akanieleza jinsi huyo mwanamke alivyomwendea bila kumfahamu na kutaka kumuuzia moja ya simu nyingi kali alizokuwa nazo kwenye begi tena kwa bei ya chee na hiyo ikiwa ni ndani ya wiki moja tu baada ya tukio la ujambazi kwenye maduka ya simu pale Mwenge ambapo huyo mwanamke alidaiwa kushiriki kwa kuongoza majambazi wenzie.

Nimetaja haya matukio yote matatu kwa sababu yalifuatana ndani ya muda mfupi kwa mpangilio niliouweka.
 
Kama miaka kumi iliyopita kuna wafanyabiashara wa madini walikuwa nane walikuwa wanaenda Mahenge walipofika nanenane walimiminiwa risasi na Polisi wakidhaniwa ni majambazi akiwemo aliyekuoa mfadhili wa bendi nyingi za muziki mjini Darisalama aliyeitwa JB

Mnaokumbuka vizuri tukio hili mtukumbushe.
Ni kweli walidhaniwa ni majambazi au ni ujambazi wa polisi tuliong'amua nyakati hizi, ulishaanza tangu wakati huo na kabla?
 
Back
Top Bottom