Tujikumbushe Walimu wa sekondari waliokuwa wakali sana kiasi cha kuwa maarufu hadi shule zingine

Nimeandika huu uzi baada ya kuwakumbuka waalimu wangu hasa wale wakuu wa miaka ya 90 mwishoni na 2000 mwanzoni waliokuwa wakali sana wasiotaka masikhara kiasi cha kuweza kujulikana hadi mkoa mzima na kanda. Wafuatao walivuma sana kanda ya kaskazini;

1. Mwalimu Kibatala - Shule ya sekondari Karatu, Arusha.
2. Mwalimu Shayo - Shule ya Sekondari Arusha.
3. Mwalimu wa malezi Ilboru sec, jina limenitoka ila ana jina la kimasai. Waliosoma 1998 - 2001 wanaweza kumkumbuka.
4. Mwalimu Teti - Tanga technical Secondary school. Huyu mkuu wa shule ilikuwa sio poa...
5. Mwalimu Mpande - Moshi Technical Secondary School. Huyu mwalimu kwenye umisetta alikuwa tishio. Ukileta zako ni kibano unakula.
6. Munga - Kaloleni sec, Arusha.
7. Kipingu -
Ongezeeni majina mengine tujikumbushe enzi za u-teenage.

Daah huyo Teti alikuwa mwamba kweli kweli!!!
 
Mchwa mpaka.....Azania
Nimeingia tu form one, wakati huo tunavaa kaptula za khaki! Kaptula ilikuwa inafika kwenye ugoko, shati sijachomekea lilikuwa puto (oversize) chini Nina Buti nimenunua kwa mwanangu kituo Cha zimamoto pale fire nadunda kinoma, daftari nilikuwa naweka mfuko wa nyuma wa kaptula....
kutimba skuli... mwamba huyuhapa! alikuwa Mwalimu wa nidhamu.... nilianza nae bifu siku hiyo ya kwanza naingia shule mpaka namaliza.

Yule jamaa hata tukikutana after life atanikumbuka tu kwa matukio niliyompiga.

RIP Mchwa

Anayejua kaburi lake lipo anitaarifu nikamwage mahindi na pombe kwani nimekuwa mkulima mlevi badala ya engineer kwa aniliyake.
 
Nimeandika huu uzi baada ya kuwakumbuka waalimu wangu hasa wale wakuu wa miaka ya 90 mwishoni na 2000 mwanzoni waliokuwa wakali sana wasiotaka masikhara kiasi cha kuweza kujulikana hadi mkoa mzima na kanda. Wafuatao walivuma sana kanda ya kaskazini;

1. Mwalimu Kibatala - Shule ya sekondari Karatu, Arusha.
2. Mwalimu Shayo - Shule ya Sekondari Arusha.
3. Mwalimu wa malezi Ilboru sec, jina limenitoka ila ana jina la kimasai. Waliosoma 1998 - 2001 wanaweza kumkumbuka.
4. Mwalimu Teti - Tanga technical Secondary school. Huyu mkuu wa shule ilikuwa sio poa...
5. Mwalimu Mpande - Moshi Technical Secondary School. Huyu mwalimu kwenye umisetta alikuwa tishio. Ukileta zako ni kibano unakula.
6. Munga - Kaloleni sec, Arusha.
7. Kipingu -
Ongezeeni majina mengine tujikumbushe enzi za u-teenage.
Ningeshangaa sana kama usingemtaja Mwalimu Mpande wa Moshi Technical, daah umenikumbusha mbali sana japokuwa umri umeenda sasa ila sitakaa nimsahau huyu mtu. Alikuwa noma sana na usemi wake eenhe bwaana..😄😄, mara ya mwisho nilikutana naye pale Moshi mjini Fresh coach 2018 nikamtupia wekundu kadhaa, alinishape sana kitabia namshukuru kwa kweli may be leo nisingekuwa hivi nilivyo. Live longer Mr. Mpande
 
Yule dingi alikuwa ni kwere kwerekweche. Waliosoma shule za Moshi mjini hakuna asiyemfahamu.
 
Back
Top Bottom