Tujikumbushe Walimu wa sekondari waliokuwa wakali sana kiasi cha kuwa maarufu hadi shule zingine


Daah huyo Teti alikuwa mwamba kweli kweli!!!
 
Mchwa mpaka.....Azania
Nimeingia tu form one, wakati huo tunavaa kaptula za khaki! Kaptula ilikuwa inafika kwenye ugoko, shati sijachomekea lilikuwa puto (oversize) chini Nina Buti nimenunua kwa mwanangu kituo Cha zimamoto pale fire nadunda kinoma, daftari nilikuwa naweka mfuko wa nyuma wa kaptula....
kutimba skuli... mwamba huyuhapa! alikuwa Mwalimu wa nidhamu.... nilianza nae bifu siku hiyo ya kwanza naingia shule mpaka namaliza.

Yule jamaa hata tukikutana after life atanikumbuka tu kwa matukio niliyompiga.

RIP Mchwa

Anayejua kaburi lake lipo anitaarifu nikamwage mahindi na pombe kwani nimekuwa mkulima mlevi badala ya engineer kwa aniliyake.
 
Ningeshangaa sana kama usingemtaja Mwalimu Mpande wa Moshi Technical, daah umenikumbusha mbali sana japokuwa umri umeenda sasa ila sitakaa nimsahau huyu mtu. Alikuwa noma sana na usemi wake eenhe bwaana..πŸ˜„πŸ˜„, mara ya mwisho nilikutana naye pale Moshi mjini Fresh coach 2018 nikamtupia wekundu kadhaa, alinishape sana kitabia namshukuru kwa kweli may be leo nisingekuwa hivi nilivyo. Live longer Mr. Mpande
 
Yule dingi alikuwa ni kwere kwerekweche. Waliosoma shule za Moshi mjini hakuna asiyemfahamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…