Tujikumbushe Walimu wa sekondari waliokuwa wakali sana kiasi cha kuwa maarufu hadi shule zingine

Ambonisye Iyunga Tech we acheni ye hachapi ila utakachokutana nacho akikubamba
 
[emoji28][emoji28]
 
Bora wewe unatambua hilo Jambo wengine wanawaona kuwa sio poa
 
Mkuu sec 2000 mpaka 2006 kuna Mwamba alikuwa anaitwa Meleki,acha alinifanya nikajenga ukuta wa parade pasaka ya mwaka 2002 sikwenda nyumbani mimi
 
Kuna mwamba anaitwa Morega Simon Mongate a.k.a double M, alikuwa mkuu wa Ndanda high school, Masasi sasa hivi nasikia amekuwa afisa elimu Kagera huko

Huyu mwamba alikuwa anaogopwa Hadi na staff wenzake, alikuwa anapenda usafi balaa yaani Bora ukutwe bweni umedodge kipindi kuliko ukutwe haujasafisha eneo lako la usafi

Mwalimu akimkuta darasani anafundisha wakat darasa likiwa chafu alikuwa anamuokotesha makaratasi huku wanafunzi wanaangalia

Usiombe ukamatwe na simu au local
 
Chodota - The Highlands
 
Nasi wa nyanda za juu kusini miaka hiyo 1999-2003 KIGONSERA SEC SCHOOL kuna mwamba anaitwa SHELIMO huyu alitusumbua Sana n mkuu wa shule aliogopwa had na staff wake

Nasikia alienda PUGU SEC SCHOOL
 
Daah huyo Mwl Mpande wa Moshi tech alikuwa ni mbabe wa kupitiliza alikuwa anaonea sana wanafunzi saa 11 asubuhi alikuwa anakuja bwenini kuwaamsha wanafunzi kwa bakora
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…