Tujikumbushe Walimu wa sekondari waliokuwa wakali sana kiasi cha kuwa maarufu hadi shule zingine

Tujikumbushe Walimu wa sekondari waliokuwa wakali sana kiasi cha kuwa maarufu hadi shule zingine

Mabagala Pugu secondary hiyo
Afu kuna mwehu alikuwa anaitwa Nampanda ana maneno balaa mswahili sana
 
Gervas Charles MKILI(r.i.p)
Green Acres yote kuanzia primary mpaka Highschool...ilibidi kwenye msiba wake wanafunze tukaage kujiridhisha ni kweli kafa,na tuone akizikwa kabisa
 
Mabagala Pugu secondary hiyo
Afu kuna mwehu alikuwa anaitwa Nampanda ana maneno balaa mswahili sana
Pugu mwaka gani mkuu

Nampanda alikuwa na kauli moja ya kifala

Anasema ""mwambie mama yako mimi ndiyo nampanda.""
 
MR.MADOSHI (R.I.P) MHONGOLO SEC KAHAMA

Huyu teacher alinifukuzisha shule maana nilishindwa vumilia ukali wake

hiyo siku akakuta namimi nishamchoka liwalo na liwe,kweli tukavaana uso kwa face

sababu tu eti nmevaa sweta nimelikunja,Kanidaka akanipa Kofiii,nikainama chini sikio linalia swiiiiiiii

ile nimeinama akaongezea mijeledi ya mgongo kama mvua, nikaona usinitanie we FAZAAA

niliiinuka na kitofali sijui nilikichomoa kwenye bustani,Nilimtwika kitofa cha tumbo,ananifata bado

nikaokota kingina rusha akapangua,Mara huyu HAPA akanidaka Nikaona isiwe kesi nikamrukia shingo

nikawa nabembea nae nipo kwa mgongoni,ah ile mechi kama sio kuja kuingiliwa na Walinzi ingeisha Bila Bila

siku hiyo hiyo Nilisikia kengele imegongwa nikafukuzwa shule saaa 1 usiku,Naenda wapiii sasa usiku huo,Nikagoma

ondoka,Ah wee saa ngapi asije na difenda ya polisi nikabebwa nikaenda malizia usiku wangu Central asubuhi nikasafirishwa kwetu

ndio mwisho wakusoma ile shule,nilimchukia yule tcha sema ndo hvyo sikua na uwezo nilimuapia viapo vingi sana

Nilipokuja sikia SIR GOD kamnyakua Ajabu et roho ikaniuma nikaona kama Mungu kamuokoa na adhabu niliyompangia...

Dingiiii apumzike tu ila alinigombanisha sana na mshua wangu kwa chumvi alizoongeza.
 
Nimeandika huu uzi baada ya kuwakumbuka waalimu wangu hasa wale wakuu wa miaka ya 90 mwishoni na 2000 mwanzoni waliokuwa wakali sana wasiotaka masikhara kiasi cha kuweza kujulikana hadi mkoa mzima na kanda. Wafuatao walivuma sana kanda ya kaskazini;

1. Mwalimu Kibatala - Shule ya sekondari Karatu, Arusha.
2. Mwalimu Shayo - Shule ya Sekondari Arusha.
3. Mwalimu wa malezi Ilboru sec, jina limenitoka ila ana jina la kimasai. Waliosoma 1998 - 2001 wanaweza kumkumbuka.
4. Mwalimu Teti - Tanga technical Secondary school. Huyu mkuu wa shule ilikuwa sio poa...
5. Mwalimu Mpande - Moshi Technical Secondary School. Huyu mwalimu kwenye umisetta alikuwa tishio. Ukileta zako ni kibano unakula.
6. Munga - Kaloleni sec, Arusha.
7. Kipingu -
8. Mwalimu Masatu na Mgimwa - Mkwawa High School (complex)
Ongezeeni majina mengine tujikumbushe enzi za u-teenage.
Mpande wa Moshi Tech. Ameshafariki. RiP. Alikua mwl. Mzuri sana wa michezo na aliipenda kazi yake ya ualimu na michezo
 
Mwalimu Mwakalinga a.k.a Kibana Mavi,Kibasila Sec. School 2000's
 
Nimesikitika sana. Ila Mwalimu Mpande nae umri ulikuwa umeenda ni vile mazoezi yalikuwa yanamweka fit. Mwaka 2002 alisema ana miaka 60.
Duh, was looking very young.. alituchangamsha sana hasa kutuamsha asubuhi kukimbia mchakamchaka. Kupitia Dom 1 hadi Dom 40 sio mchezo. we umemaliza pale mwaka gani
 
Pugu Boys Sec. hiyohiyo, 2001, Mwl Mabagala, aisee huyu mwamba alikuwa hatari sana!

Wkt wa zamu yake wanafunzi waliufyata mkia. Bilashaka alikuwa anavuta bangi pia. Manake macho yake yalikuwa hayaelewiki kbs.

Kuna siku alinikuta bwenini wkt wa vipindi, alinitoa nduki nilivyomzidi tu mbio akaanza kuropoka, "mtoto, hata ukikimbia huku umeficha sura, mimi nimeshakukariri MATAKO"...[emoji23]

Nilichoka [emoji23][emoji23]
R. I. P Mabagala
 
Back
Top Bottom