Halafu ni special kwa wenye ving'amuzi.Minara ya mawasiliano ime-haribu.Vijijini wenye uwezo mdogo mf wasio na umeme hawapati lolote.Mambo yamebadilika sana. Maisha ni mchaka mchaka[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]Siku hizi redio zimekuwa fujo tupu vipindi vyafanana na hujui usikilize redio ipi ilimradi tu tafran,na redio nyingi wanahusudu miziki
Nilikuwa std VII huko Singida vijijini. Nilisikitika sana nikafunika daftari nililokuwa nasoma.Siwezi kusahau jioni ile ya tarehe 12 April ya mwaka 1984, Mwalimu Nyerere kupitia RTD alipotutangazia msiba wa mpendwa wetu Edward Sokoine!! Siwezi sahau...
Mie naona RTD ilibamba AFRICA MASHARIKI kwa umakini na ratiba nzuri za utangazaji.Pia watangazaji wake mahiri ambao walikuwa wanatangaza kitaaluma hasa kwa kufuata maadili kama akina
Deborah mwenda
Eda sanga na wengineo nimewasahau akina kipozi kama hivyo. Siku hizi ukijua kuongea sana tu umepata kazi hata ethics huzijui mwisho wa siku watu wanakejeliana watangazaji wanaona ni lugha laini tu khaaa!
wewe unawakumbuka watangazaji gani wengine mwenzangu
Mimi nakumbuka anko wangu alikuwa anaenda kununua ofisini kwao pale nyerere road karibu na tazaraHivi ziliuzwa posta? Baba yangu alikuwa sub postmaster lakini sikuzijua hizo. Ala kumbe
Mkuu nimekukubali ila ungeongeza na misakato kila jumamosi asubuhi tunapata nyimbo mpya zinazorekodiwa halafu jioni kwa Uncle J.Nyaisanga anaposema "kwa mara nyingine tena,radio Tanzania Dar es alam yawaletea CLUB RAHA LEOOO....shoooooooo.." bila kusahau jumapili mchana sauti nzito ya David Wakati kipindi nipe habari,halafu asubuhi kuanzia saa mbili unusu asubuhi NJOO TUIMBE SOTE hapa luteni john komba ndo alipotokea na kwaya zake,ila nakumbuka kwaya moja sikumbuki aliimba nani "mtaje mtaje kiijanaa aliyekupa mimba saakina dada.....
Jumapili saa nane mchana ilikuwaga ni kipindi cha MAMA NA MWANA.
matangazo ya vifo tuu, kutwa mara saba.
Nakumbuka mwaka 1983 nikiwa std 7 nikiandika barua yangu kwenye kipindi cha mama na mwana kisha ikasomwa daa kijijini kwetu nilizua ujikooo! niliwachorea zawadi ya bata teh teh teh!![emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122]Ilikuwa ni siku ya jumamosi na mama Debora Mwenda akiwa hayupo basi Aleicia Maneno anasimamia kipindi. tulikuwa na club za mama na mwana mashuleni, mkiandika barua yenu siku hiyo ikasomwa kwenye kipindi manajiona niendio nie...lol tumetoka mbali
radio csssete maarufu enzi hizo ilikuwa ni memory Q!!
Vijana wa zamani, wazee hakuna🙄Kumbe wazee huku JF tuko wengi!
Nakumbuka nilikua sifaham maana ya kipindi cha "club raha leo shoooow" kikinikera kweli kikianza! Na hakuna station nyingine kubadilisha labda tuweke cassete ya UB40! Time hizo baba awe hajarudi home lkn, akirudi hatuna tena access na radio! Those were days
RATIBA ZA UTANGAZAJI NA VIPINDI VYA WAKATI ULE VILI REFLECT MAISHA HALISI YA ZAMA HIZO. KUMBUKENI WIMBO WA MWANAMEKA MPIGAJI AMENITOKA KIDOGO ULIINGIA KWENYE SYLABUS YA KISWAHILI O-LEVEL.
Mazungumzo baada ya habari pamoja na maneno hayoooooo