Na sasa umenikumbusha nyimbo zilizokuwa zinapigwa wakati huo kama ule usemao; "Amewaua ndugu zetu bila kosa lolote masikini....ooh mungu warehemu ndugu zeetu,ameaua na watoto wasiojua lolote masikini...ooh jama,malaika wa muungu...",na ule wa " kufyeka fyeka pori tumkamate nduli huuyoo,tutamkata na kumnyoa manyoya yake...."Siyo kweli. Amin alipigwa moja kwa moja toka vita ilivyoanza, japo kulikuwa na majibizano hapo Lukaya na mahali panaitwa Luweero na Kapeeka. Wakati wote huo, Ben Kuko alikuwa ni burudani tosha kwa ripoti zilizokuwa zibawakejeli askari wa Amin, unaweza kumlinganusha na Jerry Muro lakini kwa sauti ya Hemedi Kivuyo anapokuwa anainanga timu yenu iliyofungwa!!
Ni marehemu Sara Dumba. Alifariki March 22 mwaka huu akiwa mkuu wa wilaya ya Njombe.Kweli usemayo,ilikuwa sauti ya pekee.Yes alishatangulia sikumbuki vizuri kama ilikuwa ni mwishoni mwa mwaka jana au mwanzoni mwa mwaka huu akiwa mkuu wa wilaya katika moja ya wilaya kama sio mkoani mbeya basi ni mkoani iringa.
Mola amrehemu mufti Hemed Bin JumaHalafu ijumaa mchana waumini wa dini ya kiislamu watakumbuka sauti tulivu ya mufti wao sheikh Hemed bin Jumaa bin Hemed akitoa mawaidha kwa upole na uhakika tena bila jazba....mpaka sie tusio waislamu tulikuwa tunavutiwa kusikiliza...
Ha ha ha haaa.. Hii comment imenichekesha alfajiri yote hii...batery za Nationa ilikuwa deal mjini,kidogo za phillips utapata...,zikizingua unazibonda bonda na kuzianika juani huku unazilinda...
Paulo Sozigwa ndiye alikuwa mwandishi maana alikuwa "party ideologue". Wakati mwingine Moses Nnauye naye alikuwa anachangiaMkuu
Jamaa wa Mazungumzo baada ya Habari alikuwa ni Salimu Seif Mkamba almaarufu S.S.Mkamba, au walikuwa wanapokezana na Paulo Sozigwa ?
Mkuu nashukuru kwa kujazia, sikuthibitisha iwapo tulipigwa ndio maana nilisema inasemekana.
Ila hilo la Kivuyo na Jerry Muro umenivunja mbavu.
Hili neno limenipa shida kidogo kulielewa. Ila baada ya kujua kuwa unatokea Kilomeni nimelielewa.Umesahau idhaa ya biadhara special kwa vijana wa enzi hizo. Na idhaa ya taifa na kipindi cha mkulima wa kisasa special kwa wazee
yaaani we acha tu mtoa thread kanikymbusha Zama!!
Ha ha ha ha! sory unajua uzee tena! nilimaanisha biashara!!Hili neno limenipa shida kidogo kulielewa. Ila baada ya kujua kuwa unatokea Kilomeni nimelielewa.
1.Michezo na Abdul Omar Masoud na Juma Ngondae
2.Club Raha Leo show na Brother Enock Ngombare
3.Usiku wa Raha na Debora Mwenda/Halima Mchuka
4.Malimwengu
5.Mazungumzo baada ya habari na Salum Seif Mkamba
6.Majira na Mshindo Mkeyenge
7. From me to You (External service)
Acha tu rafiki, ni bora tuendelee tu kutumia Unverified IDs maanake huku kazi ingekuwa ni kuamkia tu kutwa nzima.duh kumbe humu kumejaa wazee
Haya bhana, nacho narekunde..!Ha ha ha ha! sory unajua uzee tena! nilimaanisha biashara!!
NI HUVO!! AHO HE KEY PAD "S" NA "D" JIHO HAFUHI!!!Haya bhana, nacho narekunde..!
Ha ha ha sawa bhana, mthi wedi.NI HUVO!! AHO HE KEY PAD "S" NA "D" JIHO HAFUHI!!!
HAMWE NAWE!!Ha ha ha sawa bhana, mthi wedi.
naona atakuwa Michael KatemboNaomba mnikumbushe mtangazaji wa kipindi cha ngoma zetu. Alifariki kitambo ila alikuwa na sauti nzuri na vituko akiweka ngoma za wajaluo kwa sana.