Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Wanabodi,
Nimekutana na picha hii kwenye posti fulani ya Safari ni safari, nikaona imenikumbusha mbali,
hivyo sio vibaya nikishare na nyinyi kuwakumbuka ma celeb wetu enzi hizo.

Naweza kuwa nimeyakosea baadhi ya majini, ni kitambo- 1995!.


Asante umetukumbusha mbali.
Msatari wa mbele waliokaa toka kushoto ni Charles Hilary 'Mzee wa Macharanga(BBC-London), Mikidadi Mahamud (Mkurugenzi, Radio Uhuru), Mzungu aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa kwanza,Julius Nyaisangah (Uncle J).
Nyuma waliosimama toka kushoto. Deo Mshigeni, (sijui alipo), Mike Mhagama(DW-Radio), Monica Mfumia (sijui Alipo), Flora Nducha (Mkuu wa UN-Radio-NewYork), Vicky Msina (PRO-BOT), Aboubakar Liongo (DW-Radio-Ujerumani, Sunday Shomari (VOA-Marekani), kabinti kadogo sikakumbuki, na wa mwisho ni Taji Liondi (Mr.T) (Mkuu wa TBC-FM).
 
Deo Mshigeni yupo USA anabeba boxex mkuu.
Mimi ndiye niliyewapiga picha hiyo ndo maana sijaonekana hapo
 
Walikuwa vichwa...
sidhani kama TBC ya sasa wanaweza wapata wengine wa level hizo..
 
Iza sizani kama hiyo ilikua tbc1 hiyo ilikua ni radio one ya kwanza kabisa by the way wakati huo hatukua na
btc1
Walikuwa vichwa...
sidhani kama TBC ya sasa wanaweza wapata wengine wa level hizo..
 
wapi blandina mungezi (aunty ndina) dah!, sauti yake ile kama kala yai bichi, na Peace kwiyamba (peace K.) mwenye sauti chombeza!
 

Hii inanikumbusha enzi zile watu wanakwenda shule bila ya viatu wala malapa, zikaja chachacha, duh!
 
Nimefurahishwa sana na thread hii kwani imenikumbusha mbali sana. Kuanzia babu yangu na baba yangu, wote walikuwa wasikilizaji wazuri sana wa redio, kwa hiyo nimekuwa nikisikiliza redio kadri kumbukumbu zangu zitakavyoweza kukumbuka. Nimeona kuna wengine wameongelea humu, kwa kukumbuka na kukosa enzi hizo, kwamba vipindi vya nyakati zile vilikuwa vizuri na hakukuwa na habari za ufisadi na maovu mengine katika jamii. Nakubaliana na wachangiaji, ila napenda kuongeza tu kuwa, badala ya kuwa na habari za maovu katika jamii, kulikuwa na kipindi ambacho kilikuwa kinakemea na kuwataarfu wananchi kuhusu maovu hayo. Hiki kilikuwa ni kipindi cha MAZUNGUMZO BAADA YA HABARI.

Binafsi nilikuwa nasubiri kwa hamu kipindi hiki, kwani sio tu kwamba kilikuwa kinafundisha, vilevile kilikuwa na hadithi kem kem za kusisimua ambazo mtangazaki aliweza kutoa maudhui yake kutokana na hadithi hizo. Kipindi cha Mazungumzo Baada ya Habari kilikuwa kinaelimisha wananchi kuhusu maovu ambayo watu wachache wanaweza kufanya, ili kuuhujumu umma. Mtungaji na mtangazaji wa kipindi hiki alikuwa ni Mzee Paul Sozigwa, ambaye yupo mpaka leo lakini ameshakwisha kustaafu.

Nimekuwa nikitamani sana kama ningeweza kupata nakala au kusikiliza mikanda ya kipindi hicho kwa sasa. Maudhui yaliyokuwa yanatolewa katika kipindi hicho yanahitajika sana katika jamii ya Watanzania, wakati huu kuliko wakati mwingine wowote ule. Natamani sana kama kipindi hicho kingewezwa kutangazwa tena.
 
Wakurugenzi wa RTD je?
  1. David Wakati
  2. Ngw'nakilala
  3. nani vile?
  4. Edda Sanga
  5. Mshana

Umenikumbusha mbali sana, i can restrospect my childhood! unakumbuka ile hadithi ya kunyenge kwenye kipindi cha mama na mwana? unasikiliza hadithi lakini una-digest kama unaangalia movie!
 

Mkuu unanikumbusha mbali sana..........kipindi hicho watu wanakusanyika sijui walikuwa Studio au Mtaani wanahojiwa na kucheza Muziki...wakati wanajieleza kunawekwa na kibezi cha nyuzi za gitaa...........utapendaaaaaaaaaaa
 
Duuh kweli mwana umenikumbusha mbali sana time ile kule kwetu tulikuwa tunasikiliza RTD na KBC tu.Hebu naomba anaefaham ule mziki/gitaa lililokuwa likipigwa kwenye kiashirio cha zilipendwa na mtu mzima Khalid Ponela ni mziki wa bendi gani?
 
Tuntemeke Sanga..... aaah samahani nimekosea kumbe watangazaji tu
 
Mkuu unanikumbusha mbali sana..........kipindi hicho watu wanakusanyika sijui walikuwa Studio au Mtaani wanahojiwa na kucheza Muziki...wakati wanajieleza kunawekwa na kibezi cha nyuzi za gitaa...........utapendaaaaaaaaaaa

kipindi kilikuwa kinaitwa- klabu la leo shoo na mtangazaji wake ni Dominick Mlekoni
 
Dominick Mrekoni alikuwa mtangazaji wa vipindi vya salamu tu tena ni hapa "juzi tu".........Mambo ya Club Raha leo Shoo ya Enock Ngombale bana..........kipindi hicho ni marufuku kuingia na Jinsi ukumbini...........hapa tutawajua tu umri wenu......
 
Na matangazo yao yalikuwa na Adabu na yanayoeleweka na rika zote. Sasa tumebaki na mitangazo mibovu na isiyo na mvuto. Pia lugha fasaha ya kiswahili ilikuwa ikitumika, kwa umakini na staha kwelikweli. Wakati huo wazazi wangu walikuwa na Radio aina ya National 277 (tamka mbili saba saba) au Dudu proof, maarufu kama Mkulima. Ikitumia betri 4 ambazo ni kutoka kiwanda cha National and Matsushita electric Co Ltd pale Pugu road. Aaah... WAKATI UMEENDA WAPI JAMANI?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…