Tujuzane aina ya manukato (perfume) unayotumia

Tujuzane aina ya manukato (perfume) unayotumia

Sema niliruka na huu ushauri nikaagiza hiyo kitu kwa Emat asee, kwangu mimi ni miongoni mwa worst products nilizowahi tumia. Nikifungua tu kifuniko napiga chafya kabla ya kujipulizia.
Pesa yangu iliteketea bure wife alijaribu nae katoka nduki imebaki kama pambo tu kabatini. Mara mia zile product za Syria
Wewe ulijimwagia ndio maana
 
Waungwana na wataalam humu ndani, ni kwa muda mrefu sasa nimekua nkitafuta perfume inaitwa "dior homme intense". Natafuta zile oil based zake kwanza maana kibubu ni bubu kweli siwezi kuruka na bififte tuu a.k.a laki 5 ya ile box.
Kwa mwenye kujua wapi ntapata, natanguliza shukrani mingi.
 
Dior Homme Intense au Dior Homme Parfum ni kitu inasifiwa sana na reviews nyingi nzuri lakini sijawahi kuielewa...

Nenda kwenye maduka yale wanauza zile perfume za Wasyria, huuwezi ikosa...
 
Light Blue 200mil inauzwa ZAR 3710 approx 540,000 TZS , kuna mshikaji anakuja na ndege ya usiku ile, kama unahitaji...

Invictus kakosa...

Ila kwa ushauri, bei za perfume SA ni ghali kidogo kuliko hata TZ...

Revolution mzigo ulikuja lakini naona response yako imekuwa slow ndio maana niliagiza 50mils tu, nitautumia tu mwenyewe...

20240708_113422.jpg

20240708_113417.jpg
 
Mkuu Watu8 kwa hii ninaweza niliona 540k nikarudi nyuma kidogo😆 ngoja nije inbox naona kwa hii itakuwa ni kama 165k hivi

Karibu, mlango upo wazi...

Jamaa alinichaji 181,500 TZS (sababu ya bank charges na forex i think), mwisho wa siku exchange rate ilikuwa ni 1 ZAR = 165 TZS, hiyo perfume aliuziwa 1100 ZAR pale OT duty free...(check picha ya pili box lina sticker ya bei)

Polish_20240713_170522878.jpg
 
Emat perfume zake kali, sio uongo.
Yan uwa napulizia nguo, naingia kuoga. Mpaka nitoke imekaa moderate.

Syria perfume baba lao, nimetumia pink sugar yao aisee ni kunukia utamu tu
Hapa patam sasa mumenigusa penyewe,mimi ni mmoja kati ya mteja mzuri toka kaanza kule makumbusho,alikua na package mbovu sana ila juice super A+..hata ofisini ilikua ndogo na mbaya.

Now ana grow, which ni kitu kizuri..ukitafuta uko juu zaidi ya miaka 3 ama minne nilikua msifiaji sana wa perfumes zake..

Ila kwenye ukweli lazima tuseme, marketing strategies zake A, branding and package A+..

Juice ni takataka, sitakaa ni nunue tena kwake, sasa hivi bei kafikisha 55k chupa kubwa hio sio shida,je kilichopo ndani kinastahili?sisi hatuna shida na hio package yake, je juice ina quality ile ile, na hii kuua quality ya bidhaa ndio inaua sana biashara za wabongo wengi, wakiwa juu wanachakachua sana wapate faida kubwa ila wanasahau ukimkimbiza mteja leo, kumrudisha ni ngumu sana.
Hizi chupa zangu mbili za mwisho naona kabisaa hii dhulma, amenidhulumu..

Ya kwanza nilisema labda bahati mbaya(aventus), ya pili nikasema nibadilishe nichukue black opium nayo ovyo.
Msiseme sikuwaambia..

Tujuzane machimbo mapya ya pima pima.
 
Attachments

  • 20240808_091136.jpg
    20240808_091136.jpg
    1.3 MB · Views: 24
Hapa patam sasa mumenigusa penyewe,mimi ni mmoja kati ya mteja mzuri toka kaanza kule makumbusho,alikua na package mbovu sana ila juice super A+..hata ofisini ilikua ndogo na mbaya.

Alianza kabla ya pale Makumbusho, kabla alikuwa anafanya delivery na boda yeye mwenyewe, naona sasa kafika mbali...

Kuhusu quality yake sijui kwa sasa ipoje, ingawaje hizo oil perfume mimi huwa naona zote zinafanana tu...
 
Nunua utatuletea mrejesho.
 
Nikipata hela naenda kwa huyo Emascent kuchukua perfume za kupima zifuatazo:
  • Black Opium
  • Lacoste White
  • Bleu de Chanel
Jumla haitozidi 70,000/=

Nitadumu nazo mwaka mzima.
 
Back
Top Bottom