Tujuzane: Je, ni samaki gani mtamu kuliko wote?

Tujuzane: Je, ni samaki gani mtamu kuliko wote?

Nani ashamla samaki mmoja hivi anaitwa Samsuri?
 
Salam kwenu.

Si mjuzi sana katika nyanja hizi..hivyo naomba kujua

Je, ni samaki gani mtamu kuliko wote? Mtaje !
1. Changu
2. Sato
3. Kibua
4. Sangara
5. Kambare
6. Perege
7. Migebuka
8. Pweza
9. ________
Kuna samaki wapo Ziwa Victoria kwa majina ya kilugha wanaitwa,
1. NEMBE
2. NINGU
3. NG'HUYU
Ni watamu kuzidi wote uliowataja hapo juu, wanazidi hata sato kwa mbali sana! Na kuna wengine pia wanaitwa GOGOGO
Hawa samaki unawajua?
 
Sisi Masai hatuli samaki. Ni aibu kwa Moran kula singiri.
Nilishawahi kwenda Umasaini...Wengi hawali Samaki wanasema wana Shombo na kwao si chakula.


Nilipita maeneo ya bwawa la nyumba ya mungu,Wamasai wengi wanaishi pembezoni kabisa mwa Bwawa hilo ila samaki hawatumii Abadan...

Kilichonistaajabisha pia wengi hata kuku hawana mpango nao!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Salam kwenu.

Si mjuzi sana katika nyanja hizi..hivyo naomba kujua

Je, ni samaki gani mtamu kuliko wote? Mtaje !
1. Changu
2. Sato
3. Kibua
4. Sangara
5. Kambare
6. Perege
7. Migebuka
8. Pweza
9. ________
Hapo ni sawa na kulinganisha papuchi hautopata mahindi, maana utamu unatokana na mlaji mwenyewe, mfano mm naona Kamongo ndo samaki mtamu kuliko wote
 
Kwanini mkuu?
Maisha ya Masai halisi yanategemea Ng'ombe. Ng'ombe ndio kila kitu kwa Masai. Masai anakula ng'ombe (sio kila siku ni kwa matukio maalum), asali, anakunywa damu ng'ombe, maziwa, nyumba yake inajengwa kwa mavi ya ng'ombe.

Masai hali nyama nyingine zaidi ya ng'ombe, mbuzi na kondoo. Masai hata akiua mnyama pori atampa mbwa au kama kuna mtu wa kabila ingine, hali yeye. Hali kuku wala samaki. Ng'ombe ndio zawadi aliyopewa na Ngai.
 
Kuna samaki wapo Ziwa Victoria kwa majina ya kilugha wanaitwa,
1. NEMBE
2. NINGU
3. NG'HUYU
Ni watamu kuzidi wote uliowataja hapo juu, wanazidi hata sato kwa mbali sana! Na kuna wengine pia wanaitwa GOGOGO
Hawa samaki unawajua?
Hawa ni kiboko, hasa ningu. Tatizo upatikanaji wake


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa ni kiboko, hasa ningu. Tatizo upatikanaji wake


Sent using Jamii Forums mobile app
Sangara ndiye aliyeharibu deal. Tangu aingie sokoni, hawa samaki wameadimika sana. Nasikia mwalo wa Magu Nembe wanapatikana kipidi mto Simiyu ukiwa na maji. Huwa wanafuata mkondo wa maji ya mto Simiyu. Halafu kitu nilikuwa sijui kumbe samaki huwa wana uwezo pia wa kuogelea upstream, yaani wanaogelea kuelekea kule ambao maji yanatoka. Huwa wanafanya hivyo kipindi mto Simiyu ukiwa na maji, wanatoka Ziwa Victoria kuelekea mtoni
 
Back
Top Bottom