kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,892
- 7,780
Binafsi nimefarijika na kufurahi Afrika ya Kusini kushusha hadhi ya ubalozi wa Israel kutoka mahusiano ya ubalozi kamili na kuwa mahudiano ya kiwango cha chini.
Ukweli kinachoendelea Israel ni utawala kama ule uliokuwepo Afrika ya Kusini enzi ya Makaburu.
Walowezi wa Kiyahudi kwenye maeneo waliyovamia ya Wapalestina wanawanyima haki na uhuru wao Wapalestina na kuwaua ovyo huku jeshi la Kizayuni likiwalinda hao 'skin heads' wa Mayahudi. Ukiwaona wakirandaranda maeneo ya Wapalestina wamevaa bunduki za rashasha huku wakipewa sapoti na askari wa Israel hakika utahuzunika.
Israel nje imekuwa ikijinadi kama nchi ya kidemokrasia sawa na nchi za Magharibi, lakini kwa uhakika utawala wao wa Kizayuni ni sawa na ule wa ki apartheid uliokuwa wa Makaburu Afrika ya Kusini.
Israel kwa kufahamu inafaidika kwa Wakristo wakereketwa kufikiri Mayahudi waliyobarikiwa na kutamkwa kwenye Biblia ni sawa na hawa maharamia wanaoongozwa na kina Netanhahu. Wala Wakristo wengi hawataki kuamini Mayahudi sio Wakristo. Ili mradi Biblia iliyoandikwa na Mayahudi wenyewe wa enzi ya zamani kila mahali imewataja Mayahudi, basi Wakristo wanapata upofu kuona uovu wa hawa wanajiita Mayahudi leo.
Kwa maoni yangu, ningependa kushauri Tanzania na nchi za Kiafrika kufuata mfano wa Afrika ya Kusini na kuvunja kabisa uhusiano wa kibalozi na Israel.
Katika kikao cha wakuu wa Umoja wa Afrika kilichopita, ilitia moyo kuona uwakilishi kama watazamaji wa Israel wakitimuliwa. Inaelekea walipewa hadhi hiyo kwa kutumia hila enzi ya uenyekiti wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.