Tukiacha Unazi tuwe wakweli, je ni nani anayechezea Brand ya Simba hivi sasa bila makubaliano ya kimkataba yenye uwazi na yanayoeleweka?

Jamaa hana wivu ila ametaka uwazi( transparency) kwamba Mo kwa kutangaziwa biashara zake binafsi na page za simba kupo kwa makubaliano ya namna gani?
 
Kama nimemwelewa mleta uzi anachozungumzia ni uwazi wa mpaka kimkataba kati ya Mo kama mdhamini na Mo kama mwekezaji kitu ambacho kina uwezekano wa kuleta mgongano wa kimaslahi
Mbona hawahoji uwekezaji wa GSM? Mimi ningeona ni jambo la kheri tuhoji kotekote maana mhindi wa watu kakaliwa kooni as if ndiye mwekezaji pekee kwenye hizi timu mbili kubwa

Ifike wakati tuhoji katika mizania sawa hapo tutajenga zaidi taifa letu na soka kwa ujumla
 
Mo yupo Simba kiupigaji, yupo pale kuvuna tu, maana mashabiki wa Simba ni watu duni na upeo mdogo. Wao watakwambia wanapata vikombe vya ubingwa, sasa kwanini wahangaike kumsumbua Mo.

Akili zitawakaa siku wakikosa ubingwa.
Mbona Yanga hazijawakaa kwa kukosa ubingwa miaka nenda rudi? By the way uwekezaji haumaanishi vikombe miaka yote ndiyo maana Lile kachukua ubingwa mbele ya PSG yenye uwekezaji mkubwa.

Wewe leta tahadhari nyingine sio hizo za kukosa ubingwa brother

Man City aliukosa ubingwa na wakati kasajili kuliko wenzake na bado lawama hazikuwa eti Sheikh Mansour ni mpigaji
 
Ifike hatua kama hauna uhakika wa unachosena bora ukae tu kimyan sidhani hayo matangazo ya bidhaa za MO kuwa yanawekwa bure hicho kitu hakipo pesa ya udhamini wa hayo matangazo anatoa. Na je timu haina mafanikio..? Mbona huulize sportpesa anatoa bei gani, kule gsm magodoro anatoa bei gani.?? Nk kwenye kila jezi kutwa mna shupalia tu Mo Mo Mo jamaa anatoa pesa sio bure. Kwa kujua ukweli tembelea ofisi za simba sc. Udaku mbaya saana.
 
Kama nimemwelewa mleta uzi anachozungumzia ni uwazi wa mpaka kimkataba kati ya Mo kama mdhamini na Mo kama mwekezaji kitu ambacho kina uwezekano wa kuleta mgongano wa kimaslahi
Kuna kilindi mbona walisema udhamini au kiasi Mo extra na Mo safi, na Mo foundation wanaweka
 
Umegonga nondo nzito sana ,
 
Mo yupo Simba kiupigaji, yupo pale kuvuna tu, maana mashabiki wa Simba ni watu duni na upeo mdogo. Wao watakwambia wanapata vikombe vya ubingwa, sasa kwanini wahangaike kumsumbua Mo.

Akili zitawakaa siku wakikosa ubingwa.
Afu anaweka pesa zake[emoji15][emoji15][emoji15] upigaji ni nini..? Kuna biashara utaifanya usiwazie faida..? [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Kwani hapa tunazungumzia yanga au simba
 
Watu kama hawa ndio wakwanza kulaumu kwanini mpira wa tz haukui ikiwa wao ndio kikwazo kikubwa. Yaani Mo anaweka pesa ya maana na timu inapiga hatua na inaonekana cha ajabu mtu kutoka kwao kashiba maandazi yake anataka aseme Mo anaiba. Basi mkawekeze nyie katieni zaidi ya 20B Mo atawaachieni.

Ifike hatua watu wamuheshimu mtu anaedhubutu. Ipo azam ya barkhesa mbona ana hela lakin anashindwa kuipandisha kwa kununua wachezaji wazuri..? Watu tukubali tu Mo kaleta maendeleo ya mpira tz kulitia simba sc
 
Hela ndefu ndo shilingi ngapi??

Hiyo mikataba inajulikana wapi au kuna wanaijua??

Kwa nini hiyo mikataba iwe kama siri, mbona thamani ya mikataba mingine ya kibiashara kwenye michezo na hata kwenye hizi timu zetu huwa inajulikana.
 
Hela ndefu ndo shilingi ngapi??

Hiyo mikataba inajulikana wapi au kuna wanaijua??

Kwa nini hiyo mikataba iwe kama siri, mbona thamani ya mikataba mingine ya kibiashara kwenye michezo na hata kwenye hizi timu zetu huwa inajulikana.
nakosa muda wa kukupigia mbuzi gitaa
 
Duh hiyo 51% nayo tena inatafutiwa Wawekezaji na sio Wanachana/Club ndio wanaomiliki? Kama ndio hivyo kweli nyinyi ni Mbumbumbu msiojielewa.
 
Mkuu Mo hua ana kufanya nini mpaka umeweka picha yake kwenye avatar yako
Hata Mimi nimemshangaa huyu Kamanda,nilitegemea hata angeweka avatar ya hash tag ya Mwenyekiti Mbowe kwa madhila anayopitia badala yake kamuweka Mwamedi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…