Hapo shida yako ni tangazo la sabuni, kama ingekuwa ile Mo energy uliyoizoea usingelia.
Simba imekuwepo miaka mingi, lakini hata mishahara ya wachezaji ilikuwa tatizo, timu ilikuwa inategemea viingilio vya milangoni ambavyo havikutosha chochote zaidi ya wale makomandoo kuneemeka kwa kupitia jina la timu.
Leo amekuja Mo, anasajili wenye viwango, anawalipa mishahara mizuri kwa wakati hatusikii wakilalamika kama upande wa pili, wanafanya vizuri ndani na nje ya nchi, brand ya timu inazidi kukua, lakini cha ajabu kwenu anayechangia kuikuza hiyo brand hatakiwi kutangaza biashara zake.
Kila siku mmekalia majungu Mo anaiibia Simba SC, bila kutuonesha ushahidi usio na shaka anaiba vipi na wapi, Simba inaingiza kiasi gani na Mo anaiba ngapi.
Wazungu husema "he who alleges must prove" if you can't shut up; vinginevyo nyie mnaoutumwa na makomandoo au ndio makomandoo wenyewe kupiga kelele mnajisumbua tu, Simba SC ilishatoka huko.
Hamjiulizi pesa za usajili, posho, gharama za usafiri na malazi, mishahara ya wachezaji na benchi la ufundi hutoka wapi, mnalialia tu; toa hizo gharama zote halafu tuambie Mo anaiba ngapi tofauti na kile alichoweka Simba SC sio maneno matupu kila siku.
Kama mlikuwa na hii akili ya biashara kwanini hamkujitokeza kabla Mo hajaenda Simba SC? au mmepata akili baada ya Mo kwenda Simba? wacheni kelele, mlilia na bil 20 zikawekwa, mmebaki kuhamisha magoli wachovu nyie.