Tukiacha ushabiki wa kivyama na Unafiki, Hoja ya Spika haijajibiwa

Tukiacha ushabiki wa kivyama na Unafiki, Hoja ya Spika haijajibiwa

Tukiacha ushabiki wa kivyama na kujipendekeza (unafiki), Licha ya kila mtu kujitokeza kujaribu kujibu hoja ya Spika Ndugai ama kuizungumzia hoja hiyo, na hata Serikali (Rais) ameitisha mkutano wa kidola nikidhani anajibu hoja, badala yake wamejikuta wanamjadili Ndugai ama kumdhihaki ama kumdhalilisha tu, hoja ya Spika Job Ndugai haijajibiwa hata chembe, na ina nguvu kubwa. Hoja ya Ndugai si kwamba ina nguvu za kitaasisi tu, bali ni hoja inayohatarisha madaraka ya Rais, kwasababu kuu mbili,

Mosi: Liko kundi kubwa la Watanzania waliopewa jina la masikini na utawala wa John Magufuli, wakaaminishwa kuwa Rais Magufuli alikataa kukopa popote duniani tangu aingie madarakani hadi anafariki, na kwamba aliwagomea wazungu kwakuwa ni mabeberu waliotaka kupora raslimali zetu. Hawa waliaminishwa ujinga kuwa miradi yote nchini inajengwa kwa pesa yetu wenyewe.

Hili kundi utaliambia nini leo ukianza kukopa kwa uwazi na kutangaza hivi kila mkopo, bila kwanza kulipa elimu kuwa Magufuli katika utawala wake alikopa kimyakimya mikopo mikubwa ya kibiashara iliyovunja rekodi ya mikopo nchini? Kosa kubwa ambalo Rais Samia alifahya ni pale alipoingia madarakani akataka kuwawin makundi yote masikini na wenye akili, akasema yeye na Magufuli ni kitu kimoja. Ni wazi hili kundi la masikini litamuunga mkono mtu yoyote atakayekosoa mikopo yenu.

Pili: Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 ibara ya 63(2) nanukuu; Ibara ya 63 (2) "Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwaniaba ya wananchi, kuisimamia na KUISHAURI Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wamajukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii."

Kwa ibara hii ya 63 (2), Spika Ndugai ametimiza wajibu wa kikatiba wa Bunge katika kuishauri serikali, Kwamaoni yangu Spika hajakosea chochote katika kauli yake kuhusu serikali kuacha kukopa. Ametimiza matakwa ya kikatiba kama mkuu wa muhimili,

Ukiacha wajibu wa kibunge kama Spika, Job Ndugai kama rais wa Tanzania ametumia ibara ya 18 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoa maoni yake. Ni sheria ipi Tanzania inayomzuia mtu kutoa maoni yake, ama kukosoa serikali?

Na Yericko Nyerere

View attachment 2069920
View attachment 2069921
Hoja kuu ya Spika ilikuwa inatetea kwa nini Bunge lilipitisha hoja ya tozo. Ni kweli kuna sentensi ukizichukulia peke yake zinaonekana kama kumkosoa Serikali lakini hiyo haikuwa hoja yake. Sasa Serikali inasemaje? Kwamba tozo na mikopo vyote viendelee? Hatimaye atakayelipa mikopo ni huyo huyo. anayetozwa!
 
Kuomba msamaha kwake hakuondoi hoja aliyoiweka mezani
Ameshasema mitandao ilikuza alichokiongea na hivyo alikuwa ni kama anajisafisha kuwa hakumaanisha kilichovumishwa na mitandao sasa kwa Hali hiyo msimamo wake ni upi. Huyu Ndugai jina lake lishapatikana wamesema ni lingombe kama yule aliyepkotwa jalalani.
 
Amesema hoja hiyo hakuisema jinsi ilivyonukuliwa kwenye mitandao ya kijamii. Anasema ni vipande vya video zilizotengenezwa na kuungwaungwa ili kumchafua. Sasa wewe ni hoja ipi unayotaka ijibiwe kwamba ni ya Ndugai?
Kwakuwa Rais ameendelea kujaribu kujibu hoja ambayo wewe unasema haipo? Basi hoja hiyo ya Ndugai inaendelea kuwa hai
 
Unataka ajibiwe Nini wewe ,hii nchi ni maskini Tena maskini kweli kweli .....

imekuwa ikikopa Toka inapata uhuru ,na hakuna mwaka umeisha bila kukopa ,huyo ndugai analijua Hilo ....

Kitendo cha kusimama na kulopoka ujinga ule ni dharau kabisa ....Sasa unataka ajibiwe Nini hasa ....kwamba hii nchi inaweza kujiendesha kwa tozo ? ....

Mambo mengine ni ujinga mtupu ..

Mama kashasema hii nchi lazima ikope ,ni maskini ..

Tanzania ni masikini ,lazima ikope
Utawaweza hawa bavicha,, vichwa vyao vizito sana kuchanganua mambo, wanadai ndugai hajajibiwa so walitaka majibu yapi?
Yale yale ya kudai katiba mpya process ikianza wanaweka mpira kwapani,,
Kwao hakuna jema,, lengo lao ni moja tu,, kukamata madaraka, [emoji23] basi
Unadai katiba na huna watu, utaipitishaje?, Au wanadhani Trump atakuja kunya katiba mpya hapa?

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Tukiacha ushabiki wa kivyama na kujipendekeza (unafiki), Licha ya kila mtu kujitokeza kujaribu kujibu hoja ya Spika Ndugai ama kuizungumzia hoja hiyo, na hata Serikali (Rais) ameitisha mkutano wa kidola nikidhani anajibu hoja, badala yake wamejikuta wanamjadili Ndugai ama kumdhihaki ama kumdhalilisha tu, hoja ya Spika Job Ndugai haijajibiwa hata chembe, na ina nguvu kubwa. Hoja ya Ndugai si kwamba ina nguvu za kitaasisi tu, bali ni hoja inayohatarisha madaraka ya Rais, kwasababu kuu mbili,

Mosi: Liko kundi kubwa la Watanzania waliopewa jina la masikini na utawala wa John Magufuli, wakaaminishwa kuwa Rais Magufuli alikataa kukopa popote duniani tangu aingie madarakani hadi anafariki, na kwamba aliwagomea wazungu kwakuwa ni mabeberu waliotaka kupora raslimali zetu. Hawa waliaminishwa ujinga kuwa miradi yote nchini inajengwa kwa pesa yetu wenyewe.

Hili kundi utaliambia nini leo ukianza kukopa kwa uwazi na kutangaza hivi kila mkopo, bila kwanza kulipa elimu kuwa Magufuli katika utawala wake alikopa kimyakimya mikopo mikubwa ya kibiashara iliyovunja rekodi ya mikopo nchini? Kosa kubwa ambalo Rais Samia alifahya ni pale alipoingia madarakani akataka kuwawin makundi yote masikini na wenye akili, akasema yeye na Magufuli ni kitu kimoja. Ni wazi hili kundi la masikini litamuunga mkono mtu yoyote atakayekosoa mikopo yenu.

Pili: Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 ibara ya 63(2) nanukuu; Ibara ya 63 (2) "Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwaniaba ya wananchi, kuisimamia na KUISHAURI Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wamajukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii."

Kwa ibara hii ya 63 (2), Spika Ndugai ametimiza wajibu wa kikatiba wa Bunge katika kuishauri serikali, Kwamaoni yangu Spika hajakosea chochote katika kauli yake kuhusu serikali kuacha kukopa. Ametimiza matakwa ya kikatiba kama mkuu wa muhimili,

Ukiacha wajibu wa kibunge kama Spika, Job Ndugai kama rais wa Tanzania ametumia ibara ya 18 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoa maoni yake. Ni sheria ipi Tanzania inayomzuia mtu kutoa maoni yake, ama kukosoa serikali?

Na Yericko Nyerere

View attachment 2069920
View attachment 2069921
msamaha wa ndugai ni wanamna mazingira alotumia kuwasilisha hoja yake lakini hakuna mahala popote palipoondoa hoja zake nandomana wanaendelea kutoa majibu yakupaniki,, kila wanapojitokeza kumdhihaki wanajikuta wanazidi kuharibu
 
Tatizo ni hata wewe kuona kwamba ile Hoja ni ya Ndugai na sio Hoja /Swali / Issue sio tu inayotakiwa kujibiwa bali majibu yake yawe wazi kwa kila mwenye macho au Mtanzania apate kujua na sio kuambulia kejeli...

Sisi watanzania ni watu wa matukio na kuangalia nani kasema na sio nini kimesemwa ndio maana always tunajikita kwenye personalities na sio issues....

Thus tupende kuangalia nini kimesemwa na sio nani kasema...., na kila kilichosemwa hata kama ni upuuzi kipatiwe majibu na sio kejeli ili kuwekana sawa, hii nchi yetu sote na kama ilivyo kukopa harusi kulipa matanga hata ambao hawakuwepo kwenye hizo harusi kwenye matanga watajumuika watake wasitake....
Majibu yawe wazi kiaje yaani?, Hayo majibu ya siku ile kama hukuelewa hakuna kitu utaelewa maishani mwako

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Ndugai hana hoja.Ndugai hana hoja. Siyo kweli unachosema. Bunge ndiyo hupitisha bajeti ya recurrent and development. Wanaposema makusanyo yatakuwa Tsh 24 T rillion huku Bajeti ya mwaka ni Tsh 32 Trillion unadhani hiyo nakisi inatoka wapi? Nakisi hujazwa kwa grants, donations and loans. Ndugai hajitambui, he is lunatic and unfit to the position
Kabla serikali haijakopa mkopo wowote lazima ipewe kibali na bunge. Hivyo ndivyo imekuwa ikifanyika?
 
Hoja kuu ya Spika ilikuwa inatetea kwa nini Bunge lilipitisha hoja ya tozo. Ni kweli kuna sentensi ukizichukulia peke yake zinaonekana kama kumkosoa Serikali lakini hiyo haikuwa hoja yake. Sasa Serikali inasemaje? Kwamba tozo na mikopo vyote viendelee? Hatimaye atakayelipa mikopo ni huyo huyo. anayetozwa!
Mikopo inalipwa kila mwezi, ni suala endelevu, mikopo inayomature, inalipwa,,,

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Andamaneni Chadema mumtetee ndugai kenge nyinyi, jitu ambalo limewanyanysa Sana bungeni Leo mnalitetea ,nyie kweli mbwa,

Na hamtokuja mshike Madaraka yoyote hapa Tz,nashauri mama awakazie Kama alivyokuwa anawakomesha dikteta magufuli
Shida ya cdm wako very stressed, maisha magumu sana tangu wakose ubunge,, lakini sasa hawajui wanakosea approach,, kumnanga hangaya eti wanaita supana,, itawacost dearly yaani in a long run...

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Ndugai inabidi mama amuwahi awekwe nje kinyume na hapo ataanzisha songombingo mama awekwe nje ingawaje sina uhakika kama atafanikiwa. ...mama ashauriwe vizuri asimtoe Kasim Kwa kiti ashauriwe pia amuachie Mbowe haraka mwisho tuombe giza naloliona mbele lisiwepo. ....
 
ili hii nchi isikope na tuishi kwa tozo...basi wote tukubali kufanya kazi kweli kwa bidii... Hivi huyo mtanzania wa kufanya kazi kiasi cha nchi kuwa na pato lake na ijitegemee yuko wapi? hawa watanzania wa kidimbwi....kujenga nchi kufikia level ya kujitegemea na kutokuwa na madeni kunataka sacrifice na commitment ya watanzania wote leo hii wakubali kufa njaa kwa manufaa ya vitukuu
 
Ingawa wengi wanaona kuwa ndugai kaonewa na kudhalilishwa mno ila anakosa uhalali kwa vile alikuwa Ni mtu wa. Kiburi na jeuri Sasa anaachwa tu Bila msaada wowote maskin ya mungu mam kamdhliidha haswa Kawaita wakuu wote wa mikoa kuja kumsaidia kumsuta ndugai na kundi lake

Afu kamalizakapanda ndege an kurud ddm muda ule ule
 
Andamaneni Chadema mumtetee ndugai kenge nyinyi, jitu ambalo limewanyanysa Sana bungeni Leo mnalitetea ,nyie kweli mbwa,

Na hamtokuja mshike Madaraka yoyote hapa Tz,nashauri mama awakazie Kama alivyokuwa anawakomesha dikteta magufuli
Sijui kama unaelewa hoja inayojadiliwa hapa....
 
Ingawa wengi wanaona kuwa ndugai kaonewa na kudhalilishwa mno ila anakosa uhalali kwa vile alikuwa Ni mtu wa. Kiburi na jeuri Sasa anaachwa tu Bila msaada wowote maskin ya mungu mam kamdhliidha haswa Kawaita wakuu wote wa mikoa kuja kumsaidia kumsuta ndugai na kundi lake

Afu kamalizakapanda ndege an kurud ddm muda ule ule
😂😂😂😂😂
 
Mwendawazimu tu ndio atamuunga mkono Ndugai, kwanza anasema hiyo hoja ni ya kutunga. Pili ameomba msamaha kwa hoja hiyo. Kama yeye binafsi anakataa hoja yake, kwanini sisi tujipe jukumu la kuitetea hoja yake? Akitaka hoja yake ibaki na nguvu ashikilie msimamo wako.
😁😁😁😁😁
 
Hakuna Raisi alikuwa mwongo Kama Magufuli.Ali uaminisha umma kuwa anaedesha serikali kwa fedha za ndani,kumbe ni mkopaji gwiji.leo watu Wana mlaumu mheshimiwa Raisi SSH.Kaazi kweli kweli.
 
Back
Top Bottom