Tukiacha ushabiki wa kivyama na Unafiki, Hoja ya Spika haijajibiwa

Tukiacha ushabiki wa kivyama na Unafiki, Hoja ya Spika haijajibiwa

Issue sio hoja issue ni credibility ya mleta hoja! Ndugai alikua radhi kuibaka katiba kufanya kila awezalo kumuwezesha Mwendazake kufanya analojisikia. Leo all over suddenly awe na uchungu na nchi kisa mikopo, we sio kweli!
 
Msikilize vizuri ndugai jinsi vitu vya ajabu vinavyopitishwa bungeni, ndio utaelewa
Kama vitu vinapita tofauti na matakwa yake na akaamua kutoa maoni yake binafsi nje ya bunge, kwanini aombe msamaha kwa kitu anachoamini yuko sahihi?
 
Na hoja ya Ndugai ni ya msingi kwa sababu:
1. Sio uongo kwamba kuna nchi zimezidiwa na mikopo.
Mfano, jirani yetu Zambia tayari ni International defaulter. Na tayari kwenye management na bodi za mashirika yake matatu, kuna raia wa kigeni ili kurejesha mkopo wao kwa kusimamia mapato na matumizi ya hayo mashirika.
Sri Lanka pia waliachia bandari kwa mchina baada ya kuzidiwa na mkopo.
Mkopo wa Ujenzi wa Reli unawatesa jirani zetu wa Kaskazini.
2. Kutoa tahadhari juu ya mikopo, sio jambo baya hata kidogo. Ni kujibizana na kueleweshana.
Kudhalilishana, kuona kwamba watu wanataka kiti 2025; ni hofu tu ya madaraka na hofu ya kupoteza kitumbua. Kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake hasa kwa swala la kitaifa kama hilo.
3. Wananchi wana haki ya kusikilizwa. Ni jambo la ajabu kuwasikiliza wale waliokuzunguka tu. Waliokuzunguka hawawezi kumwambia SSH ukweli. Ni kama ambavyo hawakumwambia JK ukweli juu ya Richmond Dowans na Escrow.
Hawakumwambia Mkapa ukweli juu ya EPA, Radar, Meremeta, Kagoda na Alex Stewarts.
Nadhani wewe ndio umeandika ukweli na bila ushabiki, nami kwa kuongezea naona mama amepanic pasipo sababu.
 
Mimi binafsi nipo na Ndugai.
Wapinzani tutakosea sana tukiwa upande wa Samia kisa Ndugai ni mtu tusiyempenda, Hoja ya Ndugai ni moja kati ya sera zetu "kupunguza mikopo na kutumia rasilimali zetu na uwekezaj"
Ndugai hatumpendi lakini upepo wa wananchi wajinga wa Tanzania upo na Ndugai maana wanaamini Magufuli alikuwa jembe hakopi nje.
Soon ndugai atahamia kwenu chadema na mtamsimamisha kuwa mgombea urais
 
Kama ni kweli kutokubaliana na mikopo ilikua ndio hoja yake, kwanini aombe radhi kwamba alieleweka vibaya?
Mimi naamini alikosea kuomba msamaha, lakini kwa uoande wake alitaka kutuliza upepo hasa ukizingatia mifumo yetu ya kumdhibiti mtu ilivyotengenexwa, lakini naamini pia alijua anekwushaamsha mjadala ambao utakuwa mwanzo wa kuangalia suala zima la mikopo.
 
Tukiacha ushabiki wa kivyama na kujipendekeza (unafiki), Licha ya kila mtu kujitokeza kujaribu kujibu hoja ya Spika Ndugai ama kuizungumzia hoja hiyo, na hata Serikali (Rais) ameitisha mkutano wa kidola nikidhani anajibu hoja, badala yake wamejikuta wanamjadili Ndugai ama kumdhihaki ama kumdhalilisha tu, hoja ya Spika Job Ndugai haijajibiwa hata chembe, na ina nguvu kubwa. Hoja ya Ndugai si kwamba ina nguvu za kitaasisi tu, bali ni hoja inayohatarisha madaraka ya Rais, kwasababu kuu mbili,

Mosi: Liko kundi kubwa la Watanzania waliopewa jina la masikini na utawala wa John Magufuli, wakaaminishwa kuwa Rais Magufuli alikataa kukopa popote duniani tangu aingie madarakani hadi anafariki, na kwamba aliwagomea wazungu kwakuwa ni mabeberu waliotaka kupora raslimali zetu. Hawa waliaminishwa ujinga kuwa miradi yote nchini inajengwa kwa pesa yetu wenyewe.

Hili kundi utaliambia nini leo ukianza kukopa kwa uwazi na kutangaza hivi kila mkopo, bila kwanza kulipa elimu kuwa Magufuli katika utawala wake alikopa kimyakimya mikopo mikubwa ya kibiashara iliyovunja rekodi ya mikopo nchini? Kosa kubwa ambalo Rais Samia alifahya ni pale alipoingia madarakani akataka kuwawin makundi yote masikini na wenye akili, akasema yeye na Magufuli ni kitu kimoja. Ni wazi hili kundi la masikini litamuunga mkono mtu yoyote atakayekosoa mikopo yenu.

Pili: Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 ibara ya 63(2) nanukuu; Ibara ya 63 (2) "Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwaniaba ya wananchi, kuisimamia na KUISHAURI Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wamajukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii."

Kwa ibara hii ya 63 (2), Spika Ndugai ametimiza wajibu wa kikatiba wa Bunge katika kuishauri serikali, Kwamaoni yangu Spika hajakosea chochote katika kauli yake kuhusu serikali kuacha kukopa. Ametimiza matakwa ya kikatiba kama mkuu wa muhimili,

Ukiacha wajibu wa kibunge kama Spika, Job Ndugai kama rais wa Tanzania ametumia ibara ya 18 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoa maoni yake. Ni sheria ipi Tanzania inayomzuia mtu kutoa maoni yake, ama kukosoa serikali?

Na Yericko Nyerere

View attachment 2069920
View attachment 2069921
Hoja hii ingelikuwepo toka enzi za magufuli leo ingekuwa na nguvu,lakini Yeriko tuambie uhalali wa hoja ya ndugai unaanzia wakati wa samia, wakati magufuli alifanya mambo ya hovyo mengi tu ambayo yalitakiwa yaanzie na aidha kupitishwa na bunge?

Yeriko kama unakubaliana na ndugai mwambue atoke hadharani akiri maovu yote aliyotutendea watanzania wakati wa magufuli.
Wananchi tumfikirie kumsamehe au hapana. Tofauti na hivyo astahili kuwa kiongozi wabunge letu.
 
Kabla serikali haijakopa mkopo wowote lazima ipewe kibali na bunge. Hivyo ndivyo imekuwa ikifanyika?
Hapana, Bunge likipitisha Bajeti kinachofuata ni UTEKELEZAJI tu. Serikali ndiyo ina wataalamu wanaojua watakopa wapi? Kiasi gani? Na watalipaje principal na interests?

Kazi ya Bunge inakuja wanapopitia kama UTEKELEZAJI ulikwenda kadri ya Bajeti iliyopitishwa mwaka uliotanguliwa
 
Mimi binafsi nipo na Ndugai.
Wapinzani tutakosea sana tukiwa upande wa Samia kisa Ndugai ni mtu tusiyempenda, Hoja ya Ndugai ni moja kati ya sera zetu "kupunguza mikopo na kutumia rasilimali zetu na uwekezaj"
Ndugai hatumpendi lakini upepo wa wananchi wajinga wa Tanzania upo na Ndugai maana wanaamini Magufuli alikuwa jembe hakopi nje.
kwa hiyo wewe ni bendera fuata upepo
 
Kwa akili yako ndogo na pumba ulizozoea kupost unadhani Ndugai hajui nakisi ya bajeti inapatikana vipi? Hoja ilukuwa kama kuna tozo zinazojenga madarasa kwa nini tukope? Tumia akili acha kujibu ishu kwa chuki.
Kama hujanielewa nilichojibu kwenye ile post yangu jihesabu kuwa wewe ni MLEMAVU wa akili. Sina namna ya kukusaidia
 
Mpaka sasa Mshindi ni Ndugai. Hakukanusha hoja yake Bali alisema amenukuliwa vibaya na aliomba radhi kwa sintofahamu iliyojitokeza. Alitumia busara tu yakawaida pale unapoomba msamaha ili mtu fulani alidhike wakati mwenye kosa ni mwombwaji msamaha.
 
Mimi binafsi nipo na Ndugai.
Wapinzani tutakosea sana tukiwa upande wa Samia kisa Ndugai ni mtu tusiyempenda, Hoja ya Ndugai ni moja kati ya sera zetu "kupunguza mikopo na kutumia rasilimali zetu na uwekezaj"
Ndugai hatumpendi lakini upepo wa wananchi wajinga wa Tanzania upo na Ndugai maana wanaamini Magufuli alikuwa jembe hakopi nje.
Hatumpendi tena hatumtaki.
Ameshafanya mambo ya hovyo sana.
Mbona hakumkosoa magufuli,ununuzi wa midege ilipitishwa na bunge, hata kama ni pesa ya ndani?
 
Kuomba msamaha kwake hakuondoi hoja aliyoiweka mezani
Ndungai ametukosea sana sisi wananchi sidhani kama amemkosea mama, akiwa kiongozi wa kutuwakilisha anabariki na kuisifia na kuipitisha mikopo ofisi kwake, halafu anatoka kulalamika mtaani.
Bado najaribu kumuelewa Job lakini nashindwa aliemuelewa anieleweshe.
 
Ndugai hana hoja.Ndugai hana hoja. Siyo kweli unachosema. Bunge ndiyo hupitisha bajeti ya recurrent and development. Wanaposema makusanyo yatakuwa Tsh 24 T rillion huku Bajeti ya mwaka ni Tsh 32 Trillion unadhani hiyo nakisi inatoka wapi? Nakisi hujazwa kwa grants, donations and loans. Ndugai hajitambui, he is lunatic and unfit to the position
Haya yote unayosema Lisu kakanusha juzi na kuwashangaa mnaosema huwa yanapita na kujadiliwa bungeni!
 
Kwa hiyo hapo umejibu hoja ya Ndugai?

Acheni porojo na kumshambulia mtu badala ya kuja na majibu ya hoja
Yeye mwenyewe kaikana hoja yake. Sasa tumjibu hoja ipi?
 
Ndugai inabidi mama amuwahi awekwe nje kinyume na hapo ataanzisha songombingo mama awekwe nje ingawaje sina uhakika kama atafanikiwa. ...mama ashauriwe vizuri asimtoe Kasim Kwa kiti ashauriwe pia amuachie Mbowe haraka mwisho tuombe giza naloliona mbele lisiwepo. ....
Wacha inyeshe tuone panapovuja mkuu.
 
Ingawa wengi wanaona kuwa ndugai kaonewa na kudhalilishwa mno ila anakosa uhalali kwa vile alikuwa Ni mtu wa. Kiburi na jeuri Sasa anaachwa tu Bila msaada wowote maskin ya mungu mam kamdhliidha haswa Kawaita wakuu wote wa mikoa kuja kumsaidia kumsuta ndugai na kundi lake

Afu kamalizakapanda ndege an kurud ddm muda ule ule
Eti mtaani wanasema mama kamchamba. [emoji16][emoji16]
 
Back
Top Bottom