Tukiacha ushabiki wa kivyama na Unafiki, Hoja ya Spika haijajibiwa

Tukiacha ushabiki wa kivyama na Unafiki, Hoja ya Spika haijajibiwa

Bajeti ya 32T au 34T au 36 T ni ya serikali yote including taasisi zake ambazo hazitegemei makusanyo ya TRA kujiendesha.
Kwa hiyo kama naksi ipo, basi haiwezi kufika 10T
 
Nyama hizo za mtori mbona hatuzikuti? Au mnada ushapigwa imekula kwetu.
Glass please
 
Kwa mujib wa huu mjadala, spika alihoji kuhusu mikopo, kitu ambacho kinaweza kujadiliwa bungeni wakati wa budget. Sasa kama huko wanapitisha na hasemi chochote, iweje huku nje aseme kwamva anashangazwa na mikopo inavyoongezeka?
 
Nape bado hajaomba msamaha kutaka ukaguzi wa mikopo ya awamu ya tano.
Uko sahihi mkuu, ila kwa vile hoja ni hii kauli ya spika kuhusu huu mkopo wa 1.3, ndiomaana huyo hajatajwa.

Huyo nae ana hoja, lakini nakuhakikishia leo hii hawezi kusema hilo akiulizwa kama uchunguzi ni kwa awamu ya tano peke yake au hadi awamu ya sasa? Hatoweza kunyoosha maelezo. Tena isiwe wakati huu wakati tuna fukuto la kusubiria teuzi.

Ila nashindwa kustaajab kama hata Mama mwenyewe alipita na kuwaambia watu kuhusu umeme gharama kuwa 27,000/- na huyo huyo anakuja kupindisha kauli tena kana kwamba haelewi chochote, nikaona kumbe huu ni ukoo mmoja.
Kinachotokea wakati mtu anaongea anatazama upepo ukoje na maslahi yake yanaathirika vipi.
 
Mwendawazimu tu ndio atamuunga mkono Ndugai, kwanza anasema hiyo hoja ni ya kutunga. Pili ameomba msamaha kwa hoja hiyo. Kama yeye binafsi anakataa hoja yake, kwanini sisi tujipe jukumu la kuitetea hoja yake? Akitaka hoja yake ibaki na nguvu ashikilie msimamo wako.

Kwahyo Yericko ni mwendawazimu..!??

Afu ni kamanda mwenzetu ujue
 
Kwa hiyo hapo umejibu hoja ya Ndugai?

Acheni porojo na kumshambulia mtu badala ya kuja na majibu ya hoja
Ndugu usiumize kichwa na baadhi ya watu humu jamii forum utapagawa pale utakapokosoa serikali ya sasa na kumsifiwa JPM utapata majibu ya shopo huwezi amini binafsi nimegundua kuwa wao wanatumika kwa kazi hiyo na wanapinga tu bila hoja ni matusi na kejeli kama mlevi
 
Haya yote unayosema Lisu kakanusha juzi na kuwashangaa mnaosema huwa yanapita na kujadiliwa bungeni!
Kwa hiyo akikanusha Lissu ndiyo na wewe unakubali? Lissu ndiyo kakuahikia akili yako?
 
Kama serikali huwa inakopa bila mikopo kupitiwa na kupewa kibali bungeni Ndugai na Nape wako sahihi kuhoji mikopo na afya yake kwa uchumi wa taifa.
Naomba unipe kifungu cha Katiba/ Sheria inayosema Bunge ndiyo mamlaka ya kuidhinisha mikopo. Short of that mnakuwa mnabisha tu kufurahisha wasomaji
 
Tukiacha ushabiki wa kivyama na kujipendekeza (unafiki), Licha ya kila mtu kujitokeza kujaribu kujibu hoja ya Spika Ndugai ama kuizungumzia hoja hiyo, na hata Serikali (Rais) ameitisha mkutano wa kidola nikidhani anajibu hoja, badala yake wamejikuta wanamjadili Ndugai ama kumdhihaki ama kumdhalilisha tu, hoja ya Spika Job Ndugai haijajibiwa hata chembe, na ina nguvu kubwa. Hoja ya Ndugai si kwamba ina nguvu za kitaasisi tu, bali ni hoja inayohatarisha madaraka ya Rais, kwasababu kuu mbili,

Mosi: Liko kundi kubwa la Watanzania waliopewa jina la masikini na utawala wa John Magufuli, wakaaminishwa kuwa Rais Magufuli alikataa kukopa popote duniani tangu aingie madarakani hadi anafariki, na kwamba aliwagomea wazungu kwakuwa ni mabeberu waliotaka kupora raslimali zetu. Hawa waliaminishwa ujinga kuwa miradi yote nchini inajengwa kwa pesa yetu wenyewe.

Hili kundi utaliambia nini leo ukianza kukopa kwa uwazi na kutangaza hivi kila mkopo, bila kwanza kulipa elimu kuwa Magufuli katika utawala wake alikopa kimyakimya mikopo mikubwa ya kibiashara iliyovunja rekodi ya mikopo nchini? Kosa kubwa ambalo Rais Samia alifahya ni pale alipoingia madarakani akataka kuwawin makundi yote masikini na wenye akili, akasema yeye na Magufuli ni kitu kimoja. Ni wazi hili kundi la masikini litamuunga mkono mtu yoyote atakayekosoa mikopo yenu.

Pili: Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 ibara ya 63(2) nanukuu; Ibara ya 63 (2) "Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwaniaba ya wananchi, kuisimamia na KUISHAURI Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wamajukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii."

Kwa ibara hii ya 63 (2), Spika Ndugai ametimiza wajibu wa kikatiba wa Bunge katika kuishauri serikali, Kwamaoni yangu Spika hajakosea chochote katika kauli yake kuhusu serikali kuacha kukopa. Ametimiza matakwa ya kikatiba kama mkuu wa muhimili,

Ukiacha wajibu wa kibunge kama Spika, Job Ndugai kama rais wa Tanzania ametumia ibara ya 18 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoa maoni yake. Ni sheria ipi Tanzania inayomzuia mtu kutoa maoni yake, ama kukosoa serikali?

Na Yericko Nyerere

View attachment 2069920
View attachment 2069921
Katila bandiko lako umekosea kusema , nanukuu' MASIKINI NA WENYE AKILI' mwisho wa kunukuu, ina maana kuwa masikini ni kukosa akili au ni matokeo tu ya maisha? Hoja ya Ndugai ilikuwa inakwenda mbali mbali sana ila tatizo hakuimalizia nadhani aliogopa usalama wake, alipaswa amalizie kwamba mikopo tunayokopa pesa nyingi zinaporwa na kupelekwa Zanzibar na mwisho wa siku mwenye kubeba deni na kulilipa ni Tanganyika
 
Bajeti ya 32T au 34T au 36 T ni ya serikali yote including taasisi zake ambazo hazitegemei makusanyo ya TRA kujiendesha.
Hata ukichanganya maduhuri kutoka vyanzo vingine utakuta kuna NAKISI tu. Kwani wanaposema Budget yetu ni donor dependent by 40% huwa mnaelewaje?
 
Back
Top Bottom