Tukibadili mtizamo pale Kivukoni Kigamboni tutaondoa kero ya kudumu na kuzalisha Masaki mpya kama hivi

Kwanini pasijengwe daraja linalofunguka na kufunga?View attachment 2250347View attachment 2250348
Hili linaweza kuwa wazo zuri japo pia mtoa mada amewaza vyema. Changamoto hapa nazoziona mimi ni mbili

i. Umeme wetu sio wa uhakika na pia utunzaji na usimamizi wa miundombinu kwetu sio kipaumbele. Si ajabu mtu kung'oa kibao cha jina la mtaa ili akauze chuma chakavu. Pia si ajabu askari wa barabarani (sijaweka neno usalama kwa kuwa siamini kuwa salama mikononi mwa askari mbele ya pesa) akang'oa kibao hichohicho ili tu apige faini raia. Daraja hilo litahitaji umeme ili kufanya kazi wakati Tanesco inajulikana sana.

ii. Kivuko ni mradi wa watawala hivyo kujenga barabara ama daraja ni kupunguza faida. Nchi yetu haiendelei kwakuwa mabwanyenye yamekalia uchumi hivyo unafuu kwa mwananchi wa chini ni kujifilisi wao.
 
Mkoa mmoja una watu zaidi ya 1.5m
 

Kuhusu wasiwasi wa umeme nakubaliana na wewe. Lakini utatuzi walioutumia kwenye SGR utatumika hapo pia. Ikumbukwe SGR inahitaji umeme muda wote, sifikirii Hilo hawajalizingatia kuja na mbadala.

Shida yangu hizo spiral pande mbili zitahitaji eneo kubwa sana. Itabidi maeneo yabomolewe na sioni uwazi wa kutosha bila kuathiri stand ya mwendo Kasi, ya daladala au huko ikulu ya Dar.

Yote Kwa yote, penye Nia Pana njia.
 
Hizo mambo zinataka mtu mmoja mwenye kufanya maamuzi magumu, vinginevyo itaendelea kuwa simulizi.
 
Eneo linatosha sana mkuu! Umeme wa Ku opareti hapo siyo mwingi, ni Transifoma moja la KVA 300 Linatosha kabisa kutoa umeme wa kutosha hapo na ukabaki umeme mwingi tu, hata ikihitajika kufungwa stand by jenereta bado yapo ya kutosha!
Umeme mwingi pale ni taa tu na compyuta, n.k
 

Kuhusu umeme nilikua namaanisha upatikanaji wa uhakika. Hapo kwenye eneo nawaza kipenyo Cha mzunguko au diameter ya spiral inawezakuwa na urefu kiasi Gani?

Na Je, haiwezi kuwa soura kwenda juu? Badala ya kupita chini zikazunguka kwenda juu meli zikapita chini? Hii ni tofauti kimuundi na like la kufunika na kufunga. Itarahisisha maintenance kuliko ikiwa chini ya maji.

Mwisho wa siku kama nilivyosema awali, penye Nia Pana njia.
 
Eneo ni kubwa mno pale linatosha hata ukichukua kipenyo kikubwa kabisa cha mita 100 nafas linatosha!
Sasa wanaweza kufanya pungufu ya kipenyo hiko.
Pia kuhusu umeme unatosha kutokana na kwamba hakuta kuwa na mitambo mikubwa zaidi ya taa!
Hivyo hata kama umeme ukikatika taa hizo zinawezwa kuwashwa kwa backup ya jenereta na maisha yakaendelea!
Ikumbukwe kwa huko chini kutakuwa na mwanga wa taa pia magari yana taa in case of imegence ukikatika ghafla hautazuia magari kukwama hivyo uhitaji wa taa sanasana ni kwa pedestrian
 
Kuna mktaba hapa tumesaini na kampuni ya kihindi ya kutupatia software ya kufuatilia umeme unapokatika. Tumetumia Kama 69bilioni na bado tunahitaji tuzunguke na helcopter nchi nzima tucheki kina Cha maji mana kinapungua.
Bwawa la nyerere haliwezi kukamilika ili kuwe na umeme nafuu wakati inahitajika tutumie gesi Kuna perse ya wajanja wachache tuliotangulia kuiona dunia. Subirieni Kwanza mnyonywe mpaka mavi yaaishe.
Nchi kubwa hii Ina raslimali nyingi sema anayezi control hawazidi hata watano ama kumi.hebu waza aliyeleta suala la nchi Kama Ana akili nzuri ama Bora tungeishi kabla ya ukoloni.
Nani alikuambia mwanasiasa yupo kwa akili ya manufaa ya Taifa sio kukunyonya mpaka update akili.
Watu wanataka kuweka utajiri kizazi Chao millele wewe umelala. Utawala wa sultani seyyid said huko uarabuni mpaka saivi wanaeendelea kuwa matajiri so ndio target zetu.
Utaendelea kuwa mtumwa milele.
If you don't political affairs in your country you're doomed to be lunder embicile leaders.
Huyu Ni Plato alisema sio mie Sasa wewe ni Nani ukamzidi Plato mtizamo
 
Kazi kwelikweli
 
 
Mkimalizana na hapo Kigamboni, tunataka daraja kwenda Zanzibar. Tunawaachia muamue lipite chini ya maji au juu ya maji, kazi kwenu.
 
Hiyo itakuwa gharama sana na issue ni ndogo sana. Pale inachapwa flyover moja simple tu ya line nane. Story inaisha. Hiyo spiral ni gharama sana halafu kipande chenyewe cha maji kina upana mfupi hauzidi hata kilometers 2.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…