Tukibadili mtizamo pale Kivukoni Kigamboni tutaondoa kero ya kudumu na kuzalisha Masaki mpya kama hivi

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Historia ya mji wa kigamboni ilikuwa shamba, kama ilivyokuwa mbezi beach na maeneo mengine yaliyokuwa pembezoni mwa mzizima (Dar)

Mawazo ya kuleta kivuko pale kigamboni yalilenga tiba ya dharula kwa wakati huo teknolojia ilikuwa haijasambaa duniani!

Hivyo matumizi ya kivuko siyo usafili wa kudumu pale kigamboni bali ni kama ARV ya kujipanga kutatua tatizo enzi hizo!

Wangapi mmewahi kujiuliza hatima ya kivuko itakoma lini? Wangapi mmewahi kuwaza hadi kitokee nini ndipo tubadili mtizamo wa ARV kivuko?

Nchi yetu siyo changa, inaweza kubadili mtizamo huu sasa, Naomba serikali iwaoondolee mzigo wa kutumia ARV kivuko kila siku wadau wa vivuko pale kigamboni.

Uwepo wa daraja la mwalimu nyerere kule kurasini hautoshi kuondoa tatizo pale kivukoni! (Pale kivukoni ni njia fupi hivyo lazima suluhisho la kudumu lipatikane palepale)

Ebu kila mmoja atafakali, ulishaonea wapi chombo kinachofanya kazi saa 24 kila siku (January hadi December) kikaondoa tatizo la kudumu?

Kama binadamu tu huhitaji kupumzika, je hivi vivuko mapumziko yake ni lini?

Tunaweza kuwalaumu Temesa kwa huduma mbovu lakini ni nani anaeweza kuvaa nguo moja kila siku na asibaki mtupu wakati nguo ikiwa imekwisha au kufuliwa?

Utupu wa temesa pale kivukoni unaweza kuleta maafa makubwa siku moja na dunia nzima ikasikitika kwa kushindwa kuamua sasa!

Ukiachana na hatari ya kivuko kuzama, hata ile kuwarundika abiria kwenye banda ni hatari kubwa mno (Mungu aepushie mbali!)

Yale Mabanda ya abiria yapo karibu sana na maisha mengine ya kijamii ambapo mtu anaweza kurusha chochote hatari kwa mkono na kikafika, hata hizo bar maeneo ya kivuko hazikustahili kuwepo pale kubana nafasi!

Najua afrika hatujui kubadili paa la nyumba hadi nyumba nzima iungue moto!

Lakini tukumbuke pesa pasipo usalama wa wananchi haina maana!

NINI KIFANYIKE?
Ni muda muafaka pale kivukoni kigamboni tujenge daraja la chini ya maji kama ninavyoshauri kwenye mchoro huu hapa chini!

Gharama yake inaweza ikawa kati ya billion 280 hadi 350 kulingana na design ya wizara!

Design ya kwanza ya Barabara inaweza kuanzia pale maeneo ya hoteli ya kempiski na barabara ikaaambaaa na kingo ya fukwe ya bahari kuelekea chini ya bahari na kuibukia kigamboni minazi mikinda katika njia iliyonyooka!

AU

Design ya pili ni spiral way inajengwa pale ilipo stendi ya mwendokasi kivukoni, panakuwa na barabara ya mzunguko (spiral) kuelekea chini halafu then inanyoosha chini ya bahari hadi kigamboni ambako itaibuka na kunganishwa na barabara zingine!

Stendi ya mwendo kasi pale magogoni inakufa itabaki kituo kidogo cha kushusha na stend itahamishiwa kigamboni

Wakati wa mradi madadala yataishia posta ya zamani, na vivuko vitabeba abiria wa miguu tu ambao watashuka palepale kwenye gati na kutembea sambamba na bahari hadi maeneo ya hotel ya kimpisk ilipo au watashushwa posta ya zamani kwa kujengwa gati la muda!

Faida ya mradi!
1. Tutakuwa tumetatua tatizo la kudumu
2. Usalama wa watu ni mkubwa
3. Tutakuwa tumezalisha mji mwingine kama masaki au pengine kama ilivyo dubai
4. Uwekezaji, ofisi na hoteli za kitalii zitajengwa kigamboni n.k
5. Gharama za ukarabati ni rahisi zaidi kuliko ilivyo daraja la juu ya maji
6. Ni salama na rahisi kutumia
7. Pantoni zinaweza kugeuzwa kuwa boti za utalii

VIONGOZI MNAWEZA HILI, AMUENI SASA
IMG-20220603-WA0000.jpg
 
Hili litaenda sambamba na ujenzi wa viwanja vipya kwaajili ya Afcon 2027 au
 
Suluhisho kamili la kigamboni ni kujenga barabara ya chini ya bahari tu. Kisayansi ni jambo linawezekana kwa asilimia 100 na jambo linyekuwezekana kiuchumi kwa nchi yetu kwa asilimia 100%.

Jambo muhimu kwa sasa ni wadau mbalimbali kuja na michanganuo ya kisayansi na kiuchumi (kama hili la mleta mada hapa JF) ili kuiamsha jamii kifikra na hapo serikali itaamshwa kutoka usingizini.
 
Nasikia Mondi kanunua kisiwa chote sehemu fulani, ramani ya kimataifa!
Sasa msianze tena kumpigia kelele, maana ni wazi atateka watalii wote!
Qualification: Mhudumu yeyote lazima awe na ujuzi wa lugha saba!(fluent)
 
Uko sahihi kabisa... Daraja la chini ndiyo suluhisho pekee....

Option ya kwanza iko straight zaidi... Bil. 350 ni pesa ambayo serikali ikiamua inawezekana tu.....

Sent from my TECNO LA7 using JamiiForums mobile app
 
Kigamboni itakuja kuwa moja ya sehemu Bora kabisa, asilimia kubwa ya kigamboni imepimwa na Ina beach nzuri sana
 
Suluhisho kamili la kigamboni ni kujenga barabara ya chini ya bahari tu. Kisayansi ni jambo linawezekana kwa asilimia 100 na jambo linyekuwezekana kiuchumi kwa nchi yetu kwa asilimia 100%.

Jambo muhimu kwa sasa ni wadau mbalimbali kuja na michanganuo ya kisayansi na kiuchumi (kama hili la mleta mada hapa JF) ili kuiamsha jamii kifikra na hapo serikali itaamshwa kutoka usingizini.
Tutumie 200+b kujenga baharini,sehemu ambayo Pana vivuko na daraja,badala ya kujenga miundo mbinu ya imwagiliaji au lami au hospitali kubwa!..mnadhani Tanzania ni dar tu!?
 
Historia ya mji wa kigamboni ilikuwa shamba, kama ilivyokuwa mbezi beach na maeneo mengine yaliyokuwa pembezoni mwa mzizima (dar)
Mawazo ya kuleta kivuko pale kigamboni yalilenga tiba ya dharula kwa wakati huo teknolojia ilikuwa haijasambaa duniani!

Hivyo matumizi ya kivuko siyo usafili wa kudumu pale kigamboni bali ni kama ARV ya kujipanga kutatua tatizo enzi hizo!

Wangapi mmewahi kujiuliza hatima ya kivuko itakoma lini? Wangapi mmewahi kuwaza hadi kitokee nini ndipo tubadili mtizamo wa ARV kivuko?

Nchi yetu siyo changa, inaweza kubadili mtizamo huu sasa, Naomba serikali iwaoondolee mzigo wa kutumia ARV kivuko kila siku wadau wa vivuko pale kigamboni.

Uwepo wa daraja la mwalimu nyerere kule kurasini hautoshi kuondoa tatizo pale kivukoni! (Pale kivukoni ni njia fupi hivyo lazima suluhisho la kudumu lipatikane palepale)

Ebu kila mmoja atafakali, ulishaonea wapi chombo kinachofanya kazi saa 24 kila siku (January hadi December) kikaondoa tatizo la kudumu?
Kama binadamu tu huhitaji kupumzika, je hivi vivuko mapumziko yake ni lini?

Tunaweza kuwalaumu Temesa kwa huduma mbovu lakini ni nani anaeweza kuvaa nguo moja kila siku na asibaki mtupu wakati nguo ikiwa imekwisha au kufuliwa?

Utupu wa temesa pale kivukoni unaweza kuleta maafa makubwa siku moja na dunia nzima ikasikitika kwa kushindwa kuamua sasa!
Ukiachana na hatari ya kivuko kuzama, hata ile kuwarundika abiria kwenye banda ni hatari kubwa mno (Mungu aepushie mbali!) Yale Mabanda ya abiria yapo karibu sana na maisha mengine ya kijamii ambapo mtu anaweza kurusha chochote hatari kwa mkono na kikafika, hata hizo bar maeneo ya kivuko hazikustahili kuwepo pale kubana nafasi!

Najua afrika hatujui kubadili paa la nyumba hadi nyumba nzima iungue moto!

Lakini tukumbuke pesa pasipo usalama wa wananchi haina maana!
NINI KIFANYIKE?
Ni muda muafaka pale kivukoni kigamboni tujenge daraja la chini ya maji kama ninavyoshauri kwenye mchoro huu hapa chini!

Gharama yake inaweza ikawa kati ya billion 280 hadi 350 kulingana na design ya wizara!

Design ya kwanza ya Barabara inaweza kuanzia pale maeneo ya hoteli ya kempiski na barabara ikaaambaaa na kingo ya fukwe ya bahari kuelekea chini ya bahari na kuibukia kigamboni minazi mikinda katika njia iliyonyooka!
AU
Design ya pili ni spiral way inajengwa pale ilipo stendi ya mwendokasi kivukoni, panakuwa na barabara ya mzunguko (spiral) kuelekea chini halafu then inanyoosha chini ya bahari hadi kigamboni ambako itaibuka na kunganishwa na barabara zingine!

Stendi ya mwendo kasi pale magogoni inakufa itabaki kituo kidogo cha kushusha na stend itahamishiwa kigamboni

Wakati wa mradi madadala yataishia posta ya zamani, na vivuko vitabeba abiria wa miguu tu ambao watashuka palepale kwenye gati na kutembea sambamba na bahari hadi maeneo ya hotel ya kimpisk ilipo au watashushwa posta ya zamani kwa kujengwa gati la muda!

Faida ya mradi!
1. Tutakuwa tumetatua tatizo la kudumu
2. Usalama wa watu ni mkubwa
3. Tutakuwa tumezalisha mji mwingine kama masaki au pengine kama ilivyo dubai
4. Uwekezaji, ofisi na hoteli za kitalii zitajengwa kigamboni n.k
5. Gharama za ukarabati ni rahisi zaidi kuliko ilivyo daraja la juu ya maji
6. Ni salama na rahisi kutumia
7. Pantoni zinaweza kugeuzwa kuwa boti za utalii

VIONGOZI MNAWEZA HILI, AMUENI SASA
View attachment 2250307
Hebu tufungulie code ARV ni nini mheshimiwa mbunge?

Unapotumia terminologies au abbreviations usidhani kila mtu anazijua.

Fafanua hapo au naondoa shilingi
 
Usiondoe shilingi mkuu! Maendeleo ni yetu sote
 
Tutumie 200+b kujenga baharini,sehemu ambayo Pana vivuko na daraja,badala ya kujenga miundo mbinu ya imwagiliaji au lami au hospitali kubwa!..mnadhani Tanzania ni dar tu!?
Dar ni mji mkubwa wa kibiashara, dar ina idadi kubwa ya watu, miundombinu inafuata kuokoa wingi wa watu, idadi ya wananchi wanaovuka pale kigamboni ni sawa jumla ya watu wa mikoa miwili huko Nyantakala!
Hivyo kwasababu zoezi la wakulima linahitaji liwe la kitaifa linaweza kufanyika kidogo kidogo
 
Back
Top Bottom