Mkuu P. heshima kwako? Umeshajiuliza swali kwanini mambo hayo yanatokea sasa sio miaka ya nyuma?
Inawezekana mimi na wewe tunawaombea pia wenzetu wafe lakini hatujijui tu. Kama sijakosea kuombea maanake, kutaka/ tamani/wish someone die. Hii inaweza kuwa kwa kutamka, andika, mawazo au kutotekeleza wajibu wako ambao utahatarisha au wafanya watu wafe.
Wewe ni mkristo, kiimani unaweza tenda dhambi kwa kukusudia au kutokukusudi. Je, mfamo wewe kwa kutoelewa ukipinga post humu kwa kutokukusudia au elewa siutakuwa umewatakia walengwa wafe?
Je, wenye mamlaka ambao walitakiwa wachukue hatua kunusulu maisha ya wananchi mfano Cotona hawa hawawatakii wananchi kifo?
Je, anaetamka namwombea fulani afe kwa sababu hajanunua ventilator na yule mwenye mamlaka wa kununua Ventilator then hanunui yupi hasa anaemwombea mwezake afe?
Wakati mwingine sisi wananchi masikini tunaombea wenye mamlaka wafe kwa maandishi au kusema kwa hasira tu tena kwa kugafirika tu lakini wenye mamlaka wao hawaombei tu ila wanaua wananchi intentionally kwa kutochukua hatua ambazo ziko ndani ya uwezo wao. Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.