Tukifanya Hivi, Kina Mwamposa na Manabii kuwa Walipa Kodi Wakubwa

Kweli Mkuu watu wanapenda kuropoka,kama inalipa na wao si wauze maji yao ya upako!
Wataweza wapi ule ni uchawi usifikiri ni hivihivi, na si kila mtu aweza mambo ya ndumba.
 
Mkuu watu wanapenda kuropoka kama Mwamposa anapiga hela si na wao wafungue ya kwao wapigie Hela!,kuuza vitu ata makanisha makongwe kama Moravian, KKKT T wanafanya.Kwa mfano Huwa kunakuwa na minada,utakuta mkungu wa ndizi wa 5000,waumini wanauziwa mpaka 50000 na pesa wanaita sadaka ila Mwamposa akiombea maji na kuwauzia waumini wake Ili apate pesa za kuendesha Kanisa lake,wanasema anauza!Kanisa lina Wafanyakazi wanalipwa mishahara,Kuna vibali vya TCRA kulipia matangazo ya Radio,mafuta ya magari nk.
 
Mwamposa ana kiwanda cha maji na duka la kuuzia ayo maji unayoyasema?
 
Yale maji, chumvi au vitambaa ni sadaka au biashara?
Na unadhani kule Kenya mpaka katamka vile (mind you jamaa ni mlokole) hakuifahamu sheria ya kodi kama wewe unayefahamu zaidi?
Hivyo vitu si nao wao wananunua madukani au wana viwanda vya kutengenezea!
 
Kwani kqnisa gani ambalo viongozi hawajitajirishi Mkuu?
KKKT wanagombania nini,Biblia?
 
Kwani Kuna Kanisa ambalo siyo la mtu au taasisi iliyoanzishwa na mtu?.Ata sadaka ya KATOLIKI inaenda Vatican na wewe unabaki na ulofa wako.Bora wakina Mwamposa wanazungusha pesa humuhumu ndani ya nchi!
 
Acha uongo yanauzwa kati ya 1000 au 2000 na pesa inaenda kwenye uendeshaji wa huduma za Kanisa.Kuna umeme unawaka pale,Kuna Redio analipia TCRA,Kuna Wafanyakazi na wachungaji wanalipwa pia nk.
Sasa ulitaka pesa atoe wapi?
Mbona kwenye makanisa ya KKKT na Moravian na ata Katoliki Huwa kunakuwa na minada makanisani muumini analeta Kuku wa Tshs 20000 na anauzwa kwa 200000,apo inakuaje Mkuu.Au ndiyo kunywa anye Kuku,akinya Bata kaarisha?
 
Hapo maana yake ni pure biashara,maji yatakuwa yanauzwa kwa 5,000.Sadaka huwa haina kiwango.Kwanini kama ni sadaka basi asiwape hayo maji hata waliotoa shs 100 maana zote ni sadaka.
Kwani hayo maji watu wote wananunua?Sauala la maji ya upako,pia siyo lazima ununue Huwa anaombea ata ya kwako uliyokuja nayo.Kuna kipindi saa tatu usiku kinaitwa "OPERESHENI KOMBOA FAMILIA"mwishoni Huwa anaombea maji na Mafuta yoyote uliyonayo.Kwaiyo tuache uzushi !
 
Ata Katoliki anauani yake ni Vatican kwa Papa!
Acha uzushi,dini ni Biashara kitambo ila shida inaanza kwasababu wakina Mwamposa wamekuja na njia tofauti ya kuabudu.
 
Sacraments haziuzwi.Utauzaje Sacrament ya Kipaimara ,ubatizo au Komunio? Kama ulimaanisha ile ekarist wanayokula hizo zinatengenezwa Kanisani na masister,huwezi zikuta ziko zinauzwa dukani kama maji,chumvi na mafuta.
Ata maji ya upako yameombewa kanisani au unadhani Yale maji ni ya kawaida Mkuu!
 
Sio chuki ndugu
Anachokifanya kinaonekana kiko kibiashara....awaambe watu waje na maji yao ayaombee warudi nayo makwao.
Vinginevyo inakuwa biashara alipe kodi ikiwa sheria itamwi giza kwenye wigo.
Mapadre , masister, wachungaji walipe Kodi za PAYE
Mkuu umewahi kwenda ukashuhudia akilazimisha watu kununua maji?ninavyojua Huwa anaombea maji yoyote ata ya kwako siyo lazima ya kwake.
 
Kauli bora kabida kutoka kwa rais wa kenya. Hebu na sisii tanzania serikali ije na uamuxi kudhibiti hawa wakora kwenye imani. Tuige ile ya rwanda kudhibiti uanzishwaji ovyo wa madhehebu za dini na hii ya biashara za kitapeli kuuzia watu bidhaa bila kulipa kodi.
 
Mwamposa ana kiwanda chake binafsi ..Maji yake Yana label yake binafsi na waumini wanauziwa hayo maji....uzembe Tu WA Tra...

Hawatakiwi hata kwenda kabisani..
Waende straight kiwandani kwake
Unaweza kufungua kiwanda bila TRA kujua?
 
Mkuu naona unaingilia madhabahu, hela ya sadaka ni mwiko kukatwa kodi, hela yoyote inayotolewa wakati wa Ibada ni sadaka na ni mali ya kuhani - imeandikwa kwamba Makuhani wote watakula madhabahuni.
 
Timu ni ileile ila viwanja ni tofauti![emoji1787][emoji1787]
 
Ruto atakuwa one term present

Alikuwa kutwa anazurura makanisani kutqfura kura hadi ya vichochoni kumbe tapeli akapata kura kageuka kupiga vita waliompa kura

Akimaliza kipindi chake Uhuru Kenyatta atarudi kwenye madaraka ya uraisi Ruto atakuwa one term president

Wanasiasa hawana loyal members makanisa ndio yanao Ruto ahesabu kuwa atakuwa president kipindi kimoja tu vaada ya hapo kwa heri
 
Unaweza kusema hapa posho wanazolipana wafanyakazi wa serikali even hao TRA kuna wakati hufanya vikao vyao wakajilipa posho huwa zinakatwa kodi?

Una chuki kubwa sana na RC bro kuwachukia hakukuongezei chochote kwenye maisha yako ya kiroho zaidi ya kupoteza muda sasa nakushauri kaa chini kunywa maji kidogo(sijui yatakuwa ni ya mwamposa au vipi utajua mwenyewe) kisha tafakari je ni sahihi kwa mwamposa kuwauzia watu Hill Water 1litre ya Tsh 500/= mtaani kwa gharama ya 5,000/= hapo Kawe na popote kwenye matamasha yake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…