Tukifanya Hivi, Kina Mwamposa na Manabii kuwa Walipa Kodi Wakubwa

Wewe ulishasikia hayo makanisa yanayofanya hivyo mchungaji au padre kajenga hotel ya nyota tatu au ana walinzi binafsi hao unaowatetea wanafanya kwa manufaa yao wala sio jamii iliyowazunguka.
Wachungaji na mapadre mbona wengi tu wana miradi binafsi ya biashara
 
Mimi nimemuuliza,ina maana Jimbo la Arusha liko juu ya TEC? Maqna anavyoelezea utadhani Jimbo la Arusha lina utaratibu wake tofauti kabisa na Majimbo mengine yote Tanzania yaliyo chini ya TEC
 
Je mafuta na chumvi ? Na yenyewe ana kiwanda cha kutengeneza ambacho kinalipa kodi?
 
Ambayo wanalipa kodi za Serikali.
Nakubali mapadre na wachungaji wako wenye miradi binafsi ya biashara tuje sasa kwenye mitaji ya hizo biashara zao wamepata toka wapi? Chanzo cha mitaji yao nini? Tuanze na Mapadre katoliki wenye miradi binafsi ya biashara tena wanazolipia kodi mitaji ya hiyo miradi pesa walipatia wapi?
 
Sijawahi kuona Kanisa kwa maana ya Parokia or Jimbo likisema waumini mtatoa kila mmoja mfano laki 3 kwa mwaka.Wewe unachanganya na kupangiwa na Jumuiya unasema ni Parokia/Jimbo.

Kinachofanyika ni huwa Jimbo linapangia kila Parokia ikusanye kiasi flan tuseme kwa ajili ya mavuno.Parokia ikipokea inagawanya kile kiasi ilichopangiwa katika Jumuiya zake na inagawanya kulingana na ukubwa wa Jumuiya mfano Jumuiya ya Mt.Yuda Thadei wanaweza kuambiwa wachangie 2.5M wakati Jumuia ya Mt.Clara wakapangiwa watoe 600K.

Jumuiya zinavyopokea kiasi kilichopangiwa wanakaa chini na kukubaliana sasa kila kaya ya hiyo Jumuiya wachangie kiasi gani? Huwezi kuta mchango huo unalingana.Lakini pia swala la michango ya dhaka,hiyo ni mtu mwenyewe ndiyo anaamua mwaka huu nitachangia kiasi gani,zaka hazilingani pia.

Mnapotuambia Arusha wako tofauti,mna maana Arusha wan Dunia yao peke yao katika utaratibu wa uendeshaji wa Kanisa Catholic nnje ya utaratibu mama unaowekwa na TEC?
 
Asilimia kubwa ya maji anayotumia Mwamposa kwenye mambo yake kiimani ni ya Hill Water, na hicho kiwanda kipo Mapinga, Bagamoyo..

Wewe kama unajua hicho kiwanda chake, weka hapa jina lake, maji anayotengeneza yanaitwaje, na wapi hicho kiwanda kilipo?
Eti kisa yana lebo yake ndiyo amekuwa na Kiwanda.Kumbe ni Order tu anapeleka pale Hill water wanampakia maji na lebo zake.
 
SASA NIAMBIENI MODALITIES YA HIYO SHERIA ITAKAAJE KIASI KWAMBA ITAMKAMATA MWAMPOSA IACHE SADAKA ZA KAWAIDA KANISANI na Msikitini
Kwenye makanisa mengine hukuti wakiuza ila Mwamposa&Co wao wanauza nje nje yale maji ya Hill 1ltr anauza Tsh 5,000/= wakati dukani kwa mangi unayapata 500/=.

RC KKkT wala misikitini hawafanyi hayo sadaka itabaki kuwa sadaka.
 
Mishahara yao
 
Kafungue na wewe uuze na utoe kodi kama ni rahisi. Kuwa weka watu na kuwa na furaha ya moyon ni zaid ya kodi
kwakweli tutaendelea kupaza sauti hadi manabii,mitume,makuhani na wainjilisti matapeli watokomed au wajirekebishe na walipe kodi.
 
Jinsi huu mjadala ulivyo sio rahisi kwetu kupata sheria rafiki kwa mambo haya..

Kila mmoja hayuko tayari kuona kiongozi wa kanisa lake akilipa kodi.. ni kwa sababu ya kuendekeza hisia za kiimani tulizopata kwa watu hawa.

JIBU RAHISI LILIKUWA YEYOTE ANAYETENGENEZA PESA, IWE BIASHARA, MSHAHARA, ZAWADI, SADAKA, N.K ALIPE KODI STAHIKI..

Habari za kusema hii inaendeleza injili, hii inasaidia watu, hii sijui nn.. ISIWE SABABU YA KUONDOLEWA KWENYE KODI. Haijalishi ww ni nani; mbunge, rais, mchungaji, padri, sister, nabii, mfalme, unalea yatima n.k.

Pia kodi iwe kiduchu na rafiki. Kila mtu atoe KWA HIARI. Ukiingiza buku ujue sh. 50/= sio yako

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Ningekutaka uthibitishe ila tutaamsha malumbano yasiyo na maana sababu usingeweza kuthibitisha haya

Ila nimepigwa butwaa kuona ulichoandika hapa maana sijawahi kukutana na kitu kama hicho ktk maisha yangu imani
 
Mkuu kwani ni lazima kila dhehebu lifuate sheria za Wakatoliki?
Ulipaswa kwanza kuelewa tulianzia wapi na niliyekuwa namjibu,usingekuja na hili swali maana hata siwezi kujibu kwakuwa umerukia kati kati.
 
Mkuu hayo Maji ananunua kwa bei ya jumla hata Lori Zima linaagizwa so sheria itake hao wanaofanya bulk purchase for resale value walipie kodi kama retailer mwingine yoyote.
 
Unadhani wafanyakazi wanalipwa na nini?. Channel za Tv Kama azam, chan. Ten, radio mpaka mikoa mbali mbali wanatakiwa walipwe. Na anajaribu kutafuta fedha ili kulipia gharama zote za uendeshaji. Siku moja alisema kwa azam wanalipia milion 22 kwa mwezi au zaidi.
Hakuna kanisa lolote kwa sasa waamini wao hawatoi sadaka, michango na zaka labda kipindi cha uenezaji ukristo ndo watu walipewa vitu mbali mbali ili wavutike.
 
Kafungue na wewe uuze na utoe kodi kama ni rahisi. Kuwa weka watu na kuwa na furaha ya moyon ni zaid ya kodi
Mbona makumbi ya disco wanalipa Kodi.
Yaaani MTU anakibanda anauza katoni moja ya Maji Kwa Siku alipe Kodi halafu MTU anayeuza katoni mia Tano Kwa Siku asilipe Kodi . Afrika Sijui tumelogwa na nani ?
Ni Bora basi Kama angekua anatoa huduma nyingine Kwa jamii kama kujenga mashule ya walemavu Bure , kichimba visima Bure , kujenga mabweni ya watoto Wa Kike n.k. lakini anapata Fedha nyingi za kuinua maisha yake Binafsi kama wafanyabiashara WENGINE wanaolipa Kodi halafu yeye halipi. Anatembelea Magari ya kifahari anajenga mahoteli yake Binafsi Kwa mgongo Wa taasisi ya kidini halafu halipi Kodi. Dini ni taasisi sio biashara ya MTU Binafsi Kwa sababu Ukristo au YESU SIO Mali yake .
Biblia ni kitabu cha Taasisi ya Kikristo huwezi kukitumia Kwa biashara zako Binafsi kitapeli ukaachwa tu.

Brand ya Kristo ilitangazwa Duniani Kwa Jasho na damu za watu ukianzia na ya Kristo Mwenyewe ivyo kuitumia Kwa manufaa Binafsi Badala ya jamii ni Makosa . Walipe Kodi Ili serikali ihudumie wananchi. Kanisa limelala sana ndio Maana Taifa linaangamia kidogo kidogo na serikali nayo isipoona kama Alivyoona Ruto SIO muda mrefu Taifa hili kitapata adhabu kubwa sana .
Ukiangalia watu wamejawa na roho mbaya ya tamaa ya Fedha ,kupitiliza, uaminifu umepungua sana Kwa Wakristo Kwa sababu Wachungaji na manabii wao na maaskofu wamejawa na tamaa kubwa na ubinafsi . YESU amebaki kama biashara ya watu Binafsi na SIO mwokozi Wa roho za watu WOTE kwenye jamii iliyojaa uzinzi,uongo, ulafi,ulevi, Wizi, mauaji, ulawiti , uonevu, na Kila aina ya ubaya lakini Jumapili watu Hao wamejaa makanisani Kununua majai ya upako Badala ya kutubu dhambi na kuziacha Kwa kumaanisha. Watu hawatoi sadaka Kwa ajili ya watumishi na huduma ya Injili Bali wananunua Maji na kuuza Maji.



Kanisa la Kirumi nalo Karne za giza zilizopita Lilifanya utapeli Kama Huo Kwa kuuza Vyeti vya msamaha Wa dhambi . Watu walikimbilia Kanisani kwanye kanisa Katoliki Kwa ajili ya kupata vyeti vya msamaha Wa dhambi.
Wasiokua na vyeti walihesabiwa kuwa ni watu Wenye dhambi na kutengwa.
Hali hiyo ya ukengeufu ilipingwa na Padri mmoja Wa kanisa Katoliki aliyeitwa Martín Luther. Aliupinga utaratibu huo Kwa nguvu zote Hata pale alipotangaziwa kuuawa lakini alisimamia msimamo wake. Baadae walijitokeza waumini WENGINE Kuunga mkono na kuitwa waasi.
Hapo likatokea kanisa la Lutheran na Kanisa Katoliki Kwa kiwango kikubwa likabadili baadhi ya taratibu za kitapeli na kurudi kwenye taasisi ya KIROHO.

Hata hivyo utapeli uliofanywa na Kanisa la Rumi ulifanywa kitaasisi na SIO matakwa ya MTU Kwa manufaa yake. Sasa Leo uuzwaji Wa Maji tiba unaofanywa na Watu Wanaojiita mitume unafanywa Kwa manufaa Binafsi . Ndio Maana kanisa linarithishwa MKE na Watoto wake. Kwa Maana kwamba ni Biashara ya familia kama biashara nyingine zilivyo.
 
Mvinyo unauzwa kama kawaida,mzee wangu huwa anaenda kununua Lita 5 anakaa nayo
Alter wine inatengenezwa Dodoma na huwa inapelekwa moja kwa moja Majimboni na Parokia zote wanakwenda kuchukulia pale Jimboni.Sasa hiyo ya kuuziwa 5lts nani anamuuzia? Pale Jimboni au Parokiani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…