Tukifuata ushauri wa Professor Janabi tutaangamia kwa njaa

Prof.Janabi anahitaji Mwanasaiklojia mahili ili amsaidie,yawezekana kuna maradhi yanayomsumbua kiasi ya kutoa tahadhali kwa wengine wasije kuwa kama yeye.
Hata hivyo yuko sawa,ingawa kwa % kubwa ya watu wenye kipato/kima Cha chini na ambazo kazi zao ni tiba tosha ushauri wake hauwafai.
 
Lizee puuzi hili!
 
mnawezahisi profesa yuko serious kumbe yuko ktk kampeni ya kuzuia wageni nyumbani kwake[emoji3][emoji3][emoji3].

fikiria huyu ni shemeji yako au baba yako mdogo,ukienda kwake utakaa siku ngapi[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Ha ha ha .....
 
Umetoa maoni mazuri sana sana. Umenikumbusha, nadhani nilisoma mahali fulani kuwa kuna utafiti ulionyesha kuwa hata kuacha kula vyakula vya aina fulani eg red meat kunaweza kusiwe na faida kwa baadhi ya makundi ya watu na pengine kukaleta matokeo hasi.
 
Uongoooo! Yaani sukari ndiyo inaleta kisukari? Biochemistry ya wapi hiyo?😁😁
 
Huyu profesa kazaliwa vijijini? Maisha ya vijijini huko mtu anaweza kumaliza miezi 3 bila kula nyama, siyo kwamba ni vegetarian, la hasha, hana uwezo.
 
Ratiba yako unayofuata lengo lake ni lipi hasa? Uko overweight au ulikuwa overweight?
 
Mkuu,

Miaka ya mwanzo ya tisini nilikuwa nafanya shughuli fulani kwenye studio ya Don Bosco Upanga.

Kulikuwa na recording sessions za mwanamuziki wa reggae, Justin Kalikawe.

Justin, kwa imani yake ya Rastafari, aliamua kuacha kula nyama. Akawa anakula mbogamboga tu. Alikuwa anafuatilia strict dietary rules za U Rastafari. Yani ukimpa chakula chenye chumvi tu, hata kama hakina nyama, Justin alikuwa hali. Ilifika wakati Justin akawa mpaka anatembea na chakula chake kwa sababu hawezi hata kula chakula cha hotelini.

Siku moja baada ya kurekodi, Justin alianguka chini studio, karibu azimie.

Ikaonekana kuwa Justin amekuwa very strict katika chakula, na kutokula nyama, bila kuwa na mpango maalum wa kufidia ukosefu w a protein, ambayo kwa kiasi kikubwa inapatikana kwenye nyama, kulimuathiri Justin.

Ikabidi sasa Justin afanye mpango maalum wa kufidia protein ambayo anaikosa kwenye nyama.

Sasa, ukisikiliza maneno kijumlajumla tu "usile nyama, nyama mbaya" , unaweza kuanguka ukafa kwa kukosa protein.
 
Kupika mboga za majini kuziivisha Kiswahili ni mojawapo ya mapishi ta hovyo sana kiafya.
 
Tuna jamii kubwa ya watu ambao hawajelimika kabisa tena wengine wakiwa wasomi wa madigrii. Ushauri wa Janabi hata haupaswi kuwa controversial na wenye kuzua mjadala mkali hivyo kama watu wangekuwa na maarifa ya msingi tu ya lishe.
 
Janabi anasikilizwa zaidi na watu maofisini wenye afya mbovu sana, sio hata mawinga.
Kwa watu wanaofanya maofisini hasa kwa Tanzania, ni kweli, wanatakiwa kupewa mafundisho sana. Kwa wale wenye magari ndiyo kabisa. Mtu anaamka asubuhi, anaingia kwenye gari (gate anafungua na kufunga mfanyakazi) akifika ofisini anakaa. Mchana anapata mlo, jioni akitoka anapitia bar anakunywa na kula anarudi nyumbani. Haya ndiyo yanakuwa maisha yake. Ma-boss wa kwetu huko hata kutengeza chai wanaagiza wahudumu.
 
Tuna jamii kubwa ya watu ambao hawajelimika kabisa tena wengine wakiwa wasomi wa madigrii. Ushauri wa Janabi hata haupaswi kuwa controversial na wenye kuzua mjadala mkali hivyo kama watu wangekuwa na maarifa ya msingi tu ya lishe.
Dr. Janabi huwa anatoa kauli nyingi controversial.

Alishawahi kusema ukikojoa mkojo wenye povu tu tayari una matatizo advanced ya figo. Alisema hizi si dalili za awali tu.

That is definitely controversial.

Kotu kingine, naona jamii nzimanya Tanzania ina tatizo la monolithic thinking, kuanzia wataalam mpaka washamba.

Tunahitaji kusisitiza ku tailor ushauri at the individual level.
 
Ukiangalia mtandaoni mkojo wenye povu ni dalili mbaya sana ya afya ya figo. Mimi simuoni Janabi kama anatoa kauli controversial, pia sio rahisi kutoa ushauri mahususi kwa muda mfupi katika vyombo vya habari.Ni muhimu kuanza na taarifa/ushauri wa jumla kabala ya kwenda kwenye tailor made. Mfano, kula chakula kingi sana cha wanga sio jambo zuri kiafya kwa ujumla, na uhalisia wa hili ni kwamba kuna watu wengi zaidi wanaopata matatizo kwa kula wanga mwingi ila ni nadra kwa watu wa makundi yote kupata matatizo yatokanayo na kula wanga kidogo sana. Pombe pia ni hivyo, mafuta pia ni hivyo.

Labda tu pia angesisitiza watu kuwaona madaktari kwa ufafanuzi na msaada zaidi kama hafanyi hivyo kwa sasa.
 
Mkojo wenye povu unaweza kuupata kwa kunywa bia moja tu, au kula vidonge vya multivitamins tu.

Sasa daktari mzima anatoaje ushauri irresponsible hivyo?

Ni kweli kuna ushauri wa jumla na ushauri tailored, lakini Janabi anasema hilo? Au anasema tu jumla ukishaona mkojo wenye povu una ugonjwa wa figo tena dvanced stages, bila kujali umekula au kunywa nini kabla ya kukojoa?

Wanga unaweza kuwa mbaya, lakini, kuna watu wanafanya kazi za shurba wanahitaji wanga sana kwa ajili ya energy. Sasa utatoa vipi ushauri wa wanga mbaya kiujumla wakati mbeba zege na mfyatua matofali wanahitaji sana wanga?
 

Marehemu Justine kalikawe nilikuwa namkubali Sana lifestyle yake MTU wa watu humble alikuwa akija home by that time kabla kifo chake the guy was nice guy


Kiranga unaibuaga mambo πŸ™ŒπŸ½
 
Marehemu Justine kalikawe nilikuwa namkubali Sana lifestyle yake MTU wa watu humble alikuwa akija home by that time kabla kifo chake the guy was nice guy


Kiranga unaibuaga mambo πŸ™ŒπŸ½
Mkuu,

Nakumbushia tu historia ya Upanga ya tangu enzi hizo Yoweri Museveni anakodi teksi kurudi kwake halafu akakimbia kulipa bill.

Leo nikimuona Museveni rais wa Uganda anazingua miaka yote hii nacheka sana jinsi maisha yanavyobadilika.

Leo nikirudi mimi Upanga naonekana mgeni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…