Tukifuata ushauri wa Professor Janabi tutaangamia kwa njaa

Aaaah a
 
β€œBaada ya kuzidiwa na njaa kisha kupata kizungu zungu na kuanguka ofisini” [emoji23][emoji23] pole sana mkuu maisha ya kizungu hatuyawezi engine zetu ni kubwa
Engine Scania unaambiwa uweke wese la bajaji
 
Du mambo ya wahenga haya,πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Hoyo resta vegan hakuwa anakula maharage, kunde, njegere, au karanga pia?

Kuna mtu namfahamu ambaye sio rasta wala vegan lakini hali nyama wala samaki kwa sababu hapendi tu hivyo vyakula na ana afya nzuri sana na pia hana hata mpango wa chakula maalum kufidia Protein anayokosa kwenye nyama na Samaki.
 
Kuna protein nyingine hupati bila nyama, na ukipoata inakuwa kidogo sana.

Kuhusu mtu kuweza kuwa vegetarian bila kuhitaji kufidia protein, hapo ndipo point yangu ya kila mtu yuko tofauti inapokuja, na kabla ya kuanza mfumo mpya wa kula au kufanya mazoezi, inabidi kupata ushauri wa kitaalamu.

Nasikitika sana ninaposikia watu wanaotakiwa kuwa wataalam wanatoa ushauri wa one size fits all.
 
Janabi alikuwa anazungumzia utambuzi wa matatizo ya figo kwa kutaja dalili kadhaa kwa pamoja, zilikuwa nyingi mojawapo ikiwa mwili kuchoka sana, kuvimba miguu, kupumua n.k alichomaanisha ni kama mtu anazo hizi dalili kwa pamoja, sio moja moja. Yani sio tu kwamba ukiwa mchovu wakati wote una dalili za figo ila kwa sababu tumekuwa nchi ya mizaha na utani sana watu wakakuruka na hiyo ya mkojo tu.
 
Sioni shida kuwepo kwa rule of thumb au ushauri general wa afya kwa kuanzia katika masuala ya vyakula. Kwamba kuna watu wanakunywa pombe sana na kuvuta sana sigara na wanaishi muda mrefu hata kufika miaka 90 bila matatizo yoyote makubwa ya kiafya kama ya kansa au ya figo haizuii kusema pombe na sigara sio nzuri kwa afya.
 
Mkuu,

Tulishalijadili hili.

Kuna mtu alimtetea hivyo hivyo unavyomtetea, akanibishia nikaweka mpaka video hapa. Nikaweka mpaka dakika na sekunde ya kuanza kusikiliza.

Jamaa alikimbia. Hakuweza kuendelea kumtetea Janabi.

Usibisje. Janabi alivyosema ni kwamba ukiona dalili yoyote kati ya hizi umefika advanced stage ya ugonjwa wa figo.

Niliweka video mpaka dakika za kwenda kusikiliza nikaziweka hapa.

Don't make me do it again.

Tatizo hao maprofesa wenu wanaongea sana bila kufikiri na bila kujua kwamba kila neno lina uzito, na watu wengi sana wanawaamini. Wanawachanganya watu.
 
Sasa hapo umeweka rule of thumb positive.

Ukiweka rule of thumb ya kusema tupunguze kula tule milo miwili halafu mtu anahitaji kula zaidi, akiacha kula anadondoka na kufa, unakuwa umeharibu sana.

Ndiyo maana msisitizo wa kwamba kabla hujaanza mfumo mpya wa kula au kufanya mazoezi pata ushauri wa mtaalamu ni muhimu sana.

Rule of thumb inaweza kukuua.
 
Mkuu Iweke hiyo video, wakati mwingine ni uelewa wa lugha tu unaweza kuwa tofauti.
 
Jamaa kuna mambo anatupeleka chaka kwa wanaojua mambo ya biology wanacheka chini chini πŸ˜‚, kwanza huyu ni mtaalamu wa lishe au cardiac issues??
 
Sio rahisi kwa dereva dalala au wa bus ambaye amekaa siku nzima anabugia na kujishilindia soda, ice cream na energy drinks kwenda kumuona mtaalamu wa afya ampe ushauri wa chakula na afya. Jamii yetu bado iko nyuma sana katika masuala ya kumuona mtaalamu wa afya kabla matatizo makubwa hayajatokea. Kiafya inashauriwa kumuona daktari wa meno angalau mara moja kwa mwaka lakini kuna watu mpaka wanakufa na miaka 90 hawajawahi kumuona daktari wa meno.
Hapo ndio umuhimu wa rule of thumb unapokuja kupitia mass media.
 
Jamaa kuna mambo anatupeleka chaka kwa wanaojua mambo ya biology wanacheka chini chini [emoji23], kwanza huyu ni mtaalamu wa lishe au cardiac issues??
Huwezu kuwa mtaalamu wa cardiac issue bila kuwa na utaalamu mkubwa sana wa lishe. Hakuna popote unapopotoshwa na Janabi, ni uelewa wako tu wa ki layman au uwezo mdogo wa ubongo ku process mambo saa nyingine mambo yanakupita juu ya kichwa.
 
Bob alikuwa hali nyama lkn alidanja
 

Kama jamii yetu haina utamaduni wa kupata ushauri wa wataalamu, tgat is even more reason kuwaambia wapate ushauri wa wataalam.

That is no excuse to neglect that.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…