Tukifuata ushauri wa Professor Janabi tutaangamia kwa njaa

Hivi huyu doctor yupo sawa kweli? Maana haya anayoshauri naona kama anataka watu tusile anaona tunafaidi
 
mnawezahisi profesa yuko serious kumbe yuko ktk kampeni ya kuzuia wageni nyumbani kwake😀😀😀.

fikiria huyu ni shemeji yako au baba yako mdogo,ukienda kwake utakaa siku ngapi🤣🤣🤣
Mwenyewe na familia yake hawataki kula Mimi niende ili nikajisababishie vidonda vya tumbo?
 
Literally ni kama professor Janabi yupo katika kampen ya #kataa chakula sababu anapingana na kila mlo uliozoeleka kwa WaTanzania. Nashauri asipuuzwe ila asitiliwe maanani sana.
Professor Janabi yupo sahihi ukila hata mara 1 kwa siku Mwezi mzima haufi, na hautaumwa magonjwa yasiyoambukiza
 
Janabi hajaongea clear bila utata.

Labda standards zako za clear bila utata na zangu ni tofauti. Labda una very low standards.

Na siwezi kushangaa.

Kwa sababu, Watanzania wengi mna vipaji vya kufanya kazi na unclear, vague communication, msielewane, halafu wote mkaona mmeelewana.

Mnarahisisha mambo tu kuyaita mepesi kama ulivyofanya wewe.

No nuance.

Daktari anasema hizi ni dalili za ugonjwa wa figo. Ukiona hizi dalili ugonjwa uko advanced stage tayari.

Hajasema ukiona dalili yoyote kati ya hizi, ukiona dalili zote 15, au ukiona dalili tano kati ya hizi 15.

Unasema vipi kuwa daktari kasema kitu clear hapo?
 
Mwenyewe na familia yake hawataki kula Mimi niende ili nikajisababishie vidonda vya tumbo?
Hauumwi hata hivyo vidonda vya tumbo inategemea unakula nini, na alishaelezea unachotakiwa kula ni nini sio unakulakula tu tatizo hamsikilizi kwa makini
 
Kuna haja ya kumsikiliza Mimi mwenyewe huyu doctor inawezekana watu wanapindisha uwasilishaji humu mitandaoni au wanachukua kipande kimoja na kuacha vingine
 
Hauumwi hata hivyo vidonda vya tumbo inategemea unakula nini, na alishaelezea unachotakiwa kula ni nini sio unakulakula tu tatizo hamsikilizi kwa makini
Nahitaji nimsikilize mwenyewe maana humu mitandaoni nimeshagundua watu wanaleta taarifa isiyokamilika.
Tatizo ni kwamba sijui napataje haya mafunzo yake.
 
Nahitaji nimsikilize mwenyewe maana humu mitandaoni nimeshagundua watu wanaleta taarifa isiyokamilika.
Tatizo ni kwamba sijui napataje haya mafunzo yake.
Ingia YouTube andika Jina lake Prof Janabi video zinakuja angalia anavyoeleza
 
Cha msingi kabisa
Ni kujitambua. Kila mtu awe na self awareness ya mwili wake. Ajue metabolic rates, Calories anazohitaji kulingana na shuguli anazofanya.
Baada ya hapo ndio atumie hizi insights za Profesa.

Tatizo kubwa wengi hatuna utamaduni wa kupima kabisa ili tujue miili yetu. Lakini Profesa yupo sahihi sana Guys gharama za matibabu ni kubwa mno. Surgery tu ya moyo India ni karibu milioni 60 (Angalau kidogo JKCIA Wameanza kufanya)
Ukila kwa usahihi wake utaondoa matatizo mengi sana hapo baadae.
 
Unafanya kazi gani??
Umeshwahi kuona au kusikia wafanyakazi wa kiwanda cha bakhresa pale buguruni wanavyohenyeka kila siku??
Halafu baada ya hiyo kazi ngumu ya kupakia viroba eoli zaidi ya 20 kwa siku aje anywe gahwa, mtaua watu aisee.
Kiranga hapo juu kaua winga, kula kulingana na shughuli zako na uahauri wa dkt.
 
Huyu Prof ni mgonjwa na ndiyo maana kakauka utadhani anakula sementi. Anataka kutu preempt tusihoji hali yake kiafya. Yuko kwenye grid ya Taifa kitambo huyo
 
Ndugu yangu naomba kama una nyimbo za #jkalikawe hasa ile album ya usimdharau
 
Marehemu Justine kalikawe nilikuwa namkubali Sana lifestyle yake MTU wa watu humble alikuwa akija home by that time kabla kifo chake the guy was nice guy


Kiranga unaibuaga mambo 🙌🏽
Namkubali sana Justin Kalikawe
Nakumbuka kuna album nyingi niliwahi kuwa nazo ila katika harakati za utafutaji nikajikuta nipo nje ya mfumo kuja kurudi tape zote zimeharibika
Nikiingia mtandaoni nakutana na nyimbo chache sana
Sijui ndugu kama waweza kusaidia kupata hata kupitia familia yake nilipie
 
Point sana
 
Fanya kitu kulingana na uwezo wako na mazingira yako,si kila ushauri wakufuata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…