Sipendi kuwa karibu na wanafiki, wazandiki, wezi, mafisadi, waongo, wala na walinda rushwa, wabaguzi, wanaotoa ahadi na kutozitimiza, wanaolinda ubadhirifu na maovu kiitikadi.
Yako mambo ya msingi ya kujadili ambayo fisiemu haiyataki na haitayataka.
1. Katiba ya mwananchi
2. Kufuta ujinga na umaskini
3. Nini faida kwa elimu ya kijana wa kitanzania (maana inasemwa "kusoma na kuandika inatosha na darasa la saba...)
4. Wakulima kwanini wanadhulumiwa miaka yote na hawapewi usaidizi unaofaa?
5. Kwanini vyama vya ushirika havina nguvu inayostahili?
6. Kwanini utu, hadhi na heshima ya wasio makada havithaminiwi? Na
7. Kwanini waliochagua upinzani/wapinzani hawatakiwi kufanya siasa na wastaarabu?
8. Kwanini...? Kwanini....? Kwanini...?
HITIMISHO: IKIWA USTAARABU NA UUNGWANA NI KUKATA VIUNO HUKU MMESHIKA ILANI MSIYOITEKELEZA ENDELEENI NAO TU RUKSA SI TUTAWATAZAMA TU. TUVUMILIANE TU
Nimei LOVE sababu ya kunickesha. Ey

Nitakujibu ifuatavyo.
1.Katiba ya mwananchi ni haki yake ya kimsingi maana sheria nyingi ZILIZOPO zina elements za UKOLONI-Magufuli HAJAKATAA ila timing haikuwa nzuri. Na serikali naamini haikuwa na hela za KUPOTEZA kwa mambo ambayo hayakuwa ni ya KIPAU MBELE
Ilibidi kufanya Maendeleo ya nchi ya nchi kwanza halafu Katiba ITAFUATA.-
Huo NI MTAZAMO WANGU BINAFSI.
2.Katika kufuta Ujinga na umasikni Tanzania chini ya Magufuli imepunguza kiwango cha UMASKINI kwa asilimia kubwa sana kwa asilimoa 8%
Kutoka 34.4% 2007 mpaka {26.4%-2018 kumbuka ni miaka MITATU tu Baada ya Magufuli kushika Utawala.wakuingoza nchi.{ 2019 World Bank Report}
3.Hilo la darasa la saba si kweli. Vijana wengi sasa wanahimizwa wasome na wanasoma kweli. Zingine ni siasa za uongo.
4.Wakulima kwa miaka mingi tulipotoka tu Ujamaa na kuubakiza kwenye nadharia tu, ilichukuwa muda mrefu MKULINA mwenyewe KUJIELEWA. Sasa anaweza kuuza mazao yake atakavyo-SOKO HURU.
5 Ni NGUVU GANI ya vyama vya Ushirika ambayo ungetaka wapewe? Maana vyama vya Ushirika ndo vunahimizwa ili kuwasaidia wakulima WASIDHULUMIWE na MADALI- Hilo si kweli.
6. Binadamu wote ni sawa na Africa ni moja. Mtu mmoja akikosea ni yeye peke yake na si kujumlisha.
7.WALIOCHAGUA UPINZANI ni Watanzania na wana haki yao ya Kikatiba kufanya siasa zao WAKATI UNAPOFIKA kama sasa hivi. siku hizi si WANAKUSANYIKA na tena wanapata coverage ya vyombo vya habari kama TV.? -Hilo pia si kweli.
8. Wanapozuiwa LABDA wahusika wanataka kuvuruga amani ama MATAMSHI ya UCHOCHEZI.La sivyo Sioni sababu ya wao kutouza sera zao kwa USTAARABU.
Naamini nimekujibu nilivyoweza. Kumbuka haya ni MAONI YANGU BINAFSI na ni mtazamo wangu mimi mwenyewe.