Yofav
JF-Expert Member
- Mar 12, 2021
- 4,236
- 7,583
Habarini wakuu,
Jana night katika safari zangu za hapa na pale kwenye daladala nipo zangu na deep feeling za kusikiliza music kwa earphones siti ya dirishani macho yakiwa nje kutazama tunavyoikata miti na mito mbalimbali, it was perfect kwangu maana me hupenda kusafiri sana, Huwa safari za usiku zinanisisimua sana hasa ile unakuta mnalikata pori alafu mfano unamuona mtu yupo peke yake maybe ukizingatia giza ni nene na pia mazingira yanatisha ila unakuta huyo mtu maybe haoneshi hofu au pengine ana hofu ila ndo hivyo yupo kwenye mapito yake ya kimaisha pia, Hilo jambo likanifanya niutafakari usiku na matukio yake mabaya niliyowahi kukutana nayo....
Tukio la kwanza, Mimi nililelewa na baba pekee baba alikuwa akinionya sana kuhusu usiku, Alikuwa akinisihi sana niepukane na mizunguko ya usiku kwani ni hatari sana, Mwanzoni nilikuwa simuelewi hadi pale nilipofikia umri wa kubalehe kwenye yale mahusiano ya girlfriend na girlfriend katika zile appointments za hapa na pale siku moja tukapanga tukutane night fulani hivi na mtoto mzuri, Though nilijua nikirudi home itakuwa msala kwa mzee ila sikujali hilo sana maana niliona cha muhimu niende na nirudi salama nikajitusu...
Ile siku niliponea kuuwawa na vibaka kama sio kujeruhiwa na girlfriend wangu alibakwa, so sad ila tulisolve mambo yakakaa sawa kuanzia pale nikagundua usiku ni hatari sana.
Tukio la pili, Hili sio la muda sana
Nilikuwa natoka kazini kuelekea nyumbani, hapakuwa na umbali sana so nikawa natembea kwa mguu barabara ya mandela road kupitia service road nilikuwa nikiongozana na mdada mmoja ambae sikumfahamu ila tulikuwa uelekeo sawa yeye yupo mbele mimi nyuma ghafla wakatokea Majamaa wawili wamepakizana kwenye bike (bodaboda) wakanipita mimi na kumuingilia yule dada kwa mbele wakamblock katika kutahamaki lile tukio maana walifunga breki ya ghafla nilisikia tu wakimuambia yule dada "Tunaomba hilo begi" (dada alikuwa ana begi, Yule dada akaanza kama kuwabwatukia hivi jamaa mmoja kashuka akamsogelea kisha akachomoa pistol akamfyatua mbili za kichwa na kuchukua begi akadandia bike wakasepa, Wakati huo mimi nimebaki kama nimeduwaa tu nisijue nini cha kufanya na hofu ikiwa imenijaa, baada ya sec kadhaa tu watu wakawa wamezingira mwili wa dada yule pale chini, Police wakaja tukaojiwa na kutoa maelezo ya tukio, vipimo vikafanyika mwili wa dada wa watu ukachukuliwa kwenda kuhifadhiwa, Kwa tetesi nilizosikia pale ni kwamba mdada yule alikuwa wakala so, pale alikuwa katoka kafunga hesabu na kwenye begi mule ndo kulikuwa na pesa za hesabu so walimtime, Me binafsi iliniuma sana kuona watu wanamtoa mtu uhai kwaajili ya jasho lake na hiyo ikanifanya nizidi kuamini usiku sio muda mzuri.
Je, wewe ni tukio gani baya ulilowahi kukutana nalo usiku?