Tukio gani limewahi kukutokea mpaka ukajisemea kweli Mungu yupo?

Tukio gani limewahi kukutokea mpaka ukajisemea kweli Mungu yupo?

Kupenya kwenye usaili ambao hata mmoja wa top management kwenye taasisi husika aliniambia aisee una bahati sana, sijui una imani gani ila katoe zaka huko popote unaposali

Siku naripoti HR anashangaa CV chenga , experience ya kulenga kwa manati, na skills za mchongo ila ndio ivyo nipo Taasisini tayari, wakahisi nina connection kubwa na serikali kuu kumbe hata sekretari tu simjui😂

Nyie acheni Mungu aitwe Mungu, ule muujiza siamini mpaka leo ila nasadiki kweli alifanya njia pasipo na njia.
 
Je tukio hili la kufaulu kidato cha Sita lina Thibitisha vipi uwepo wa Mungu na si mawazo yako tu ya kufikirika na imani?

Je vipi kama wasahishaji wa mitihani na wapangaji wa matokeo walifanya "Standardization" ya matokeo?
Linathibitisha kwasababu nilimuomba yeye, Kama walifanya standardization Basi Mungu alinijibu kupitia wao ili ipatikane sababu.
That's Why Hatukufaulu wote Kama itakuwa walifanya standardization So, in anyway bado inarudi palepale Mungu alinijibu.
Anything else??
 
Kupenya kwenye usaili ambao hata mmoja wa top management kwenye taasisi husika aliniambia aisee una bahati sana, sijui una imani gani ila katoe zaka huko popote unaposali

Siku naripoti hr anashangaa cv chenga , experience ya kulenga kwa manati, Na skills za mchongo ila ndio ivyo nipo Taasisini tayari, wakahisi nina connection kubwa na serikali kuu kumbe hata sekretari simjui😂

Nyie acheni Mungu aitwe Mungu, ule muujiza siamini mpaka leo ila nasadiki kweli alifanya njia pasipo na njia
Hii ni kubwa sana, Shukuru sana Mungu Mkuu.
 
Nikikumbuka naishia kusema kweli Mungu yupo na anatenda maana nilijua nikijitahidi sana ntakuwa na division 3 ila asilimia kubwa nilijua hii ni division 4 lakini matokeo yalivyokuja daah! Sikuamini niliishia kusema kweli Mungu yupo kwani nilifaulu vizuri.
Na wale vipanga ambao walikuwa wanafanya vizuri sana na kujitahidi wanategemea one au two kwa uzembe wa either msahishaji au kuumwa karibia na paper wakapata zero unawashauri / kuwaambia vipi ? Waamini kwamba Mungu ana upendeleo ?
 
Sitosahau 2006 kaka anauza majan(bangi) mimi dogo janja tu nina miaka 19 sasa geto kwangu ndio ilikuwa stoo ya mizigo ya kaka sasa bwana watu wakalengesha Mara difenda hii hapa polisi kama kumi na balozi halafu kaka hayupo nipo mwenyewe tu aisee asikwambie mtu hofu niliyokuwa nayo moyoni sasa pale hom tulikuwa na mbwa mkali sana nadhan kaka alikuwa anamvutisha nyasi bas akawadindia polis anabweka vibaya mno polisi wakanambia mfungie choon mbwa sijui akili ilitoka wap kwa vile gheto langu lilikuwa uwan wazee wanawakaa fungia choon choo hakina komeo nje kwa hiyo nikamfungia gheto kwangu basi polisi wakaanza upekuz nyumba nzima gheto kwa kaka wakakuta bangi kidogo bas wakaridhika hata vyumba vingine hawakusachi mda wote mm naomba mungu wasije sema mtoe mbwa huko tusachi maana wangenipiga vibaya sana kwa mzigo uliokuwepo nami nilikuwa nawaambia chumban kwangu nilikomfungia mbwa huku kwenye bangi ni kwa kaka Mimi sihusiki na biashara zake bas tukaondoka hadi kituoni mimi nawaza hivi ingekuwaje polis wangejua kama nilikomfungia mbwa ndio stoo ya mizigo hakika huwa nasema mungu yupo kaka nwenyewe alipagawa alivyoambiwa polis wamenichukua akajua na mizigo yote imekamatwa alishangaa sana kukuta gheto kwangu kuko poa mbwa tu anabweka jaman mungu yupo.
 
Ajali zingine zinazo tokea na kuua Watu wengi licha ya kwamba Abiria Husali na kuomba sana Mungu awa kinge na kuwa epusha na Ajali hiyo,

Je Huyo Mungu huwa ana walinda kweli?

Ndege ya precision Air iliyozama ziwa Victoria, Abiria walio pona ni kwamba Mungu aliwalinda?

Je Abiria walio kufa, Hawakuwa wana muomba Mungu na wenyewe wapone kama wenzao?

Huyo Mungu ana walinda kweli watu?
Mungu huyohuyo ndio anachukua roho za watu mkuu, Sasa watu watakufa bila sababu?
Hau hautaki watu wafe ?
Tukio la watu kufa na wengine kupona kwenye ajali ya ndege linathibitisha uwepo wa Mungu kwasababu zote ni kazi zake yaani anaweza kuokoa na kuangamiza at the same time ndio maana akaitwa Mungu Muweza yote huoni hapo kaweza yote? kaokoa na kaangamiza at once.
 
Na wale vipanga ambao walikuwa wanafanya vizuri sana na kujitahidi wanategemea one au two kwa uzembe wa either msahishaji au kuumwa karibia na paper wakapata zero unawashauri / kuwaambia vipi ? Waamini kwamba Mungu ana upendeleo ?
Hana upendeleo ana tenda kwa haki huenda huyo kipanga aliefeli akaja kuwa na maisha mazuri sana kuliko kilaza aliyefaulu alafu baada ya muda kipanga akafilisika na aliyefaulu kwa Magumashi akafaulu tena, That's how life is. It's circle of good and bad.
 
Katika dunia tunapitia mambo mengi ya huzuni na furaha, ya amani na magomvi vipi katika maisha yako jambo gani limewahi kutokea na ukajisemea kweli Mungu yupo.

Binafsi ni jinsi nilivyo faulu kidato cha sita yaani daah!

Nikikumbuka naishia kusema kweli Mungu yupo na anatenda maana nilijua nikijitahidi sana ntakuwa na division 3 ila asilimia kubwa nilijua hii ni division 4 lakini matokeo yalivyokuja daah! Sikuamini niliishia kusema kweli Mungu yupo kwani nilifaulu vizuri.

Vipi wewe kwa upande wako please share experience.

ANGALIZO: Wale wazee wa Mungu hayupo tafadhali hii sio thread ya ubishani juu ya uwepo wa Mungu so pita kimya kimya tu.
Ngoja nikuulize swali: Je, mwanafunzi aliyefanya mtihani wa kidato cha sita akiwa na mategemeo ya kupata division 1 lakini matokeo yalipotoka hakuamini akajikuata amepata division 4 atasemeja? Atasema hilo tukio linaonyesha ''kweli Mungu hayupo''? Ninachotaka kuku-challenge ni kuwa kupasi kwako hakuonyeshi kweli Mungu yupo kwani kuna wengi walidhani watapasi lakini wakafeli. Na wewe ungepata div 4 ulivyotegemea ina maana usingeamini kuwa Mungu yupo? Kwa nini unadhani matukio mazuri tu yanayotokea kwako ndiyo huonyesha Mungu yupo?
 
Hebu leta hizo source zako za knowledge zinazo prove uwepo wa Mungu.

Hukatazwi kuwa na imani yako, Lakini ukianza kusema kuna source za kuthibitisha uwepo wa Mungu uzilete hapa tuzione.
Kwa bahati mbaya sana sources ambazo zinatoa uthibitisho wa uwepo wa Mungu Zina rely kwenye imani, Sasa labda uniambie wewe ni imani gani mkuu?.ili nikupe reference za kuendana na imani yako
 
Hana upendeleo ana tenda kwa haki huenda huyo kipanga aliefeli akaja kuwa na maisha mazuri sana kuliko kilaza aliyefaulu alafu baada ya muda kipanga akafilisika na aliyefaulu kwa Magumashi akafaulu tena, That's how life is. It's circle of good and bad.
Kwahio ni kama kamchezo fulani ka kuwapa watu maumivu na furaha kwa hatua ? For whose Benefit ?

Na hayo mazuri au mabaya hayana uhusiano wowote na mtu binafsi ? (Yaani ukipanda mchicha huwezi kuvuna bangi ) na kama utavuna bangi ni kwamba kuna chizi alichukua mchicha wako anapanda hizo bangi hence wa kulaumiwa yupo hapo na bila uwepo wake zile bangi zisingeingia shambani kwako ? Yaani its all in happenstances....

Logically ukisema fulani kanipendelea basi fahamu kwamba kuna aliyeonewa......
 
Ngoja nikuulize swali: Je, mwanafunzi aliyefanya mtihani wa kidato cha sita akiwa na mategemeo ya kupata division 1 lakini matokeo yalipotoka hakuamini akajikuata amepata division 4 atasemeja? Atasema hilo tukio linaonyesha ''kweli Mungu hayupo''? Ninachotaka kuku-challenge ni kuwa kupasi kwako hakuonyeshi kweli Mungu yupo kwani kuna wengi walidhani watapasi lakini wakafeli. Na wewe ungepata div 4 ulivyotegemea ina maana usingeamini kuwa Mungu yupo? Kwa nini unadhani matukio mazuri tu yanayotokea kwako ndiyo huonyesha Mungu yupo?
Mimi nimeamini yupo kwa sababu nilimuomba.
Tuje kwa aliyetegemea div 1 akapata 4 huenda akaja kuwa na maisha mazuri kuliko mimi lakini sababu ya kupata hayo maisha huenda ni kupitia changamoto aliyeipata ya kufeli wangapi wamefeli shule na walikuwa na akili sana tu lakini baadae wakaja kufanya Wonders wanaishia kusema kweli Mungu yupo na anatenda.
Mwisho nikuambie kuwa sio nisingefaulu nisingeamini uwepo wa Mungu hapana, Naamini uwepo wa Mungu kabla ya mimi kufaulu ila namanisha kitu ambacho kilitokea kikakazia imani yangujust make my belief to be more solid.
Mfano mtu anaweza kunywa sumu akawa hoi alafu akaletewa maziwa akanywa akapata nafuu baada ya nafuu akasema kweli maziwa yanasaidia yaani nimepata nafuu hii aimaanishi kuwa alikuwa hajui kuwa maziwa yanasaidia au asingepata nafuu ingeondoa ukweli kuwa maziwa yanasaidia hapana ni lugha tu yakiuandishi
 
Kwahio ni kama kamchezo fulani ka kuwapa watu maumivu na furaha kwa hatua ? For whose Benefit ?

Na hayo mazuri au mabaya hayana uhusiano wowote na mtu binafsi ? (Yaani ukipanda mchicha huwezi kuvuna bangi ) na kama utavuna bangi ni kwamba kuna chizi alichukua mchicha wako anapanda hizo bangi hence wa kulaumiwa yupo hapo na bila uwepo wake zile bangi zisingeingia shambani kwako ? Yaani its all in happenstances....

Logically ukisema fulani kanipendelea basi fahamu kwamba kuna aliyeonewa......
Shida yako unataka dunia iwe ya mazuri tu. It's not like that utajuaje madhara ya mabaya wakati hujawahi experience na utajuaje thamani ya wema wakati ujawahi experience.
Ili maisha yawe na balance Ni lazima vyote vitokee kabla sijaendelea samahani wewe ni dini gani mkuu?
 
Dini Imani ni yako na faida yako..., sihitaji kujua Imani yako ili kuongea na wewe mimi ninachoongelea ni ulichoweka hapa hakileti logic / hakina mtiririko..., Katika magical world ambayo lolote linaweza kutokea sio lazima liwepo baya ili upate zuri ? Niambie mtoto wa kike mdogo anayebakwa na kufanyiwa unyama kitu kinachopelekea anakuwa depressed maisha yake yote na mwisho wa siku kujitia kitanzi anapata funzo gani katika maisha yake ya baadae ?
 
Mwaka jana daladala likapinduka nikatoka mzimaaa nikiwa na mchubuko kwenye mkono huku abiria wenzangu wengi wakiwa wamevunjika mikono na wengine miguu hawawezi kusimama.

Mwaka huu nimepanda bodaboda nyuma nimeshikilia godoro likiwa kati yangu na boda wangu. Ghafla kishindo kikali kikasikika tahamaki mimi mzimaaaa kabisa ila boda wangu kazimia baada ya kuigonga daladala kwa nyuma mpaka uso wake umepasua kioo cha nyuma na hakuwa na helmet. Pikipiki ipo mvunguni mwa daladala na boda wangu alizimia masaa 5 hajitambui toka saa 6 mpaka 11. Uso wake autamaniki. Mimi nilipata tu maumivu ya pua. Abiria wote wa daladala hawakuamini kama nilikuwa nimepamda ile bodaboda. Kiukweli acha MUNGU aitwe Mungu.
 
Natamani Jf waweke option ya muanzisha thread kuweza kublock wachangiaji asiowataka katika thread yake. kuna baadhi ya mada huwa zinaanza vizuri, ila bahati mbaya ikiambukizwa virus wa ubishani hufia njiani, na hali hiyo inapunguza wingi/uwanda wa maarifa ambayo yalitegemewa kupatikana.
 
Kwa kweli MUNGU yupo na anatenda miujiza tunashuhudia wasio amini wapate kuamini. Nakumbuka nikiwa darasa tano, siku ya jumamosi tulikuwa tunarudi shuleni kwa ajili ya masomo ya dini kuna mzungu mmoja mwanamke alikuwa a nafundisha watoto masomo ya dini, binafsi nilikuwa napenda sana kujifunza lakini pia kuimba nyimbo za walimu wale wakiongozwa na huyo mama wa kizungu anapiga gitaa vizuri sana. Nikiwa njiani narudi toka mafundishoni kwa wanaofahamu location ya shule ya msingi kimara baruti, kuna short cut moja unapita nyuma ya shule na kutokea kimara mwisho enzi hizo ilikuwa ni mapori mapori tu! Nakumbuka nilikuwa peke yangu najibu rudisha na nyimbo na furaha ya masomo tuliyofundishwa siku hiyo taratibu natembea kurudi zangu nyumbani!!! Ghafla niliona nyoka mkubwa hata alipo tokea sikujua alijiviriga miguuni mwangu, nilibaki natetemeka sana, na kwa ujasiri nilijikuta nasema kimoyo moyo "MUNGU NISAIDIE" nikiwa katika hali ya hofu kubwa yule nyoka alijikunjua na kuondoka kwa kasi kuelekea vichakani. Nilibaki nimesimama pale barabarani kwa muda sikuweza kunyanyua hata mguu kwa haraka mwili wote ulikuwa unatetemeka!! Baada ya muda nilianza kuondoka taratibu nikiwa siamini kabisa kilichotokea. Kumbu kumbu hii hajawai futika kichwani mwangu mpaka Leo. Na kwa mara ya kwanza nashuhudia hapa. Jamani maajabu yapo duniani hapa na Mungu anatenda kweli. Asante mtoa Mada wengi tutaendelea kujifunza kwa mambo halisi yanayotutokea maishani.
 
Hana upendeleo ana tenda kwa haki huenda huyo kipanga aliefeli akaja kuwa na maisha mazuri sana kuliko kilaza aliyefaulu alafu baada ya muda kipanga akafilisika na aliyefaulu kwa Magumashi akafaulu tena, That's how life is. It's circle of good and bad.

vichekesho hivi.
 
Back
Top Bottom