Tukio gani limewahi kukutokea mpaka ukajisemea kweli Mungu yupo?

Tukio gani limewahi kukutokea mpaka ukajisemea kweli Mungu yupo?

Nilikuta msg za mapenz anachat na rafiki yangu akaninyakua cm akafuta ushahidi akakataa hana mahusiano nae, Mungu alivyomkuu baada ya wiki 1, wakajirecord wanaongea mambo ya mapenz na jinsi mechi ilivyokua na hawakujua kama cm inarecord....nikaja sikiliza kilakitu
Usengelema tunataka ushuhuda na matendo makuu ya Mungunwewe unaleta mapenzi ...
 
Kwa bahati mbaya sana sources ambazo zinatoa uthibitisho wa uwepo wa Mungu Zina rely kwenye imani, Sasa labda uniambie wewe ni imani gani mkuu?.ili nikupe reference za kuendana na imani yako

kama source zinatokana na imani, kwa nini hizo imani zina "contradict" kuhusu huyo mungu mmoja?
 
Kupenya kwenye usaili ambao hata mmoja wa top management kwenye taasisi husika aliniambia aisee una bahati sana, sijui una imani gani ila katoe zaka huko popote unaposali

Siku naripoti hr anashangaa cv chenga , experience ya kulenga kwa manati, Na skills za mchongo ila ndio ivyo nipo Taasisini tayari, wakahisi nina connection kubwa na serikali kuu kumbe hata sekretari simjui😂

Nyie acheni Mungu aitwe Mungu, ule muujiza siamini mpaka leo ila nasadiki kweli alifanya njia pasipo na njia
Mkuu kweli haukua na connection? Au Surname yako ni famous, hongera lkn
 
Ajali zingine zinazo tokea na kuua Watu wengi licha ya kwamba Abiria Husali na kuomba sana Mungu awa kinge na kuwa epusha na Ajali hiyo,

Je Huyo Mungu huwa ana walinda kweli?

Ndege ya precision Air iliyozama ziwa Victoria, Abiria walio pona ni kwamba Mungu aliwalinda?

Je Abiria walio kufa, Hawakuwa wana muomba Mungu na wenyewe wapone kama wenzao?

Huyo Mungu ana walinda kweli watu?
Kiburi Cha uzima huwapumbaza sana watu....

KUSUDI LA MUNGU KUCHAGUA LITASIMAMA.

MUNGU HUMCHAGUA AMTAKAE, UMUHURUMIA AMTAKAE,UMREHEMU AMPENDAE NA UMUADHIBU AMTAKAE........

Haijalishi wewe ni mwema au ni mwovu....

Kisa Cha Esau na Jacob Mungu alimbaliki yakobo hata kabla hajazaliwa kwani Esau alimkosea nini MUNGU?

NDIO maana MUNGU aliufanya moyo wa farao kua mgumu Kwa makusudi....

Siku Moja HICHO KIBURI CHA UZIMA KITAKUONDOKA....
 
Mungu yupo kwa vile anakupangia kile unachostahili , mpaka leo naamini ulichopoteza haukustahili.

Nilipomaliza form 4 nilifaulu sana masomo yote mwishoe selection za advance nikapelekwa combination siitaki Dah! niliumia sana na kuchekwa ila walimu wakanipa ushauri nihame .

Nikamchek mdingi akasema hivi "Mimi binafsi siwez kupingana na Mungu ndo amekupangia na suala la kubadili kwangu hapana" nikaripot huku sina mzuka .Nikapambana huko huko .

From there ,niko mbali sana nilipata ajira fasta baada ya chuo tena taasisi hizi nyeti ,wanangu wote waolienda huko kwingine hawana cha maan walipata mpaka kesho yaani wazee wa vizinga na part time jobs.
Wazee wa plate number nyeusi
 
Mungu muweza wa yote mjuzi wa yote na mwenye upendo wote asingeweza kuumba ulimwengu huu wenye ajali kuwezekana, ili hali alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu usiowezekana kwa ajali kutokea.

That is a contradiction

Contradiction inayokuongoza kujua kuwa Mungu huyo hayupo zaidi ua hadithi tu za uongo za watu.
Huu ulimwengu wenye ajali, vifo, njaa na shida zingine umetokana na nini, yani kuna namna gani nyingine ulimwengu na vitu vyote humo ndani vimefanyika?
ebu ngoja nikuelewe vizuri, kwamba ulimwengu wenye ajali ni sababu tosha hamna Mungu.. ilikuaje kuaje sasa pakatokea haya, yani tulizuka zetu vaaap!!?
 
Mungu huyohuyo ndio anachukua roho za watu mkuu, Sasa watu watakufa bila sababu?
Hau hautaki watu wafe ?
Tukio la watu kufa na wengine kupona kwenye ajali ya ndege linathibitisha uwepo wa Mungu kwasababu zote ni kazi zake yaani anaweza kuokoa na kuangamiza at the same time ndio maana akaitwa Mungu Muweza yote huoni hapo kaweza yote? kaokoa na kaangamiza at once.
Anaangamiza shetani Mungu analinda, wachawi wanatoa makafara ya damu maajali na vifo vya ajabu ukichomoka hapo ndio unasema Mungu aliekua upande wako either mtu wa maombi au unaombewa sana na watu wako au Mungu bado ana plan na wewe , ila yeye hanaga upendeleo,
 
Darasani maisha yote nilikuwa natokea wa 25 na kuendelea huko, siku ya mtihani mzee namuona anaongea na teacher. Hafla naona mzee kampa teacher kitu nae teacher kaweka mfukoni alicho pewa.

Mwanangu matokeo yamekuja naambiwa eti nimetokea wa 3 🤣🤣.

Hapo nikasema Mungu anatuona kiazi mimi leo nime kuwa wa 3, halafu teacher alikuwa ananipa majibu muhuni yule😂😂
Noma sana🤣🤣🤣
 
Ajali zingine zinazo tokea na kuua Watu wengi licha ya kwamba Abiria Husali na kuomba sana Mungu awa kinge na kuwa epusha na Ajali hiyo,

Je Huyo Mungu huwa ana walinda kweli?

Ndege ya precision Air iliyozama ziwa Victoria, Abiria walio pona ni kwamba Mungu aliwalinda?

Je Abiria walio kufa, Hawakuwa wana muomba Mungu na wenyewe wapone kama wenzao?

Huyo Mungu ana walinda kweli watu?
Za kuambiwa
 
Nilishushwa kwenye gari (Prado) kisa nlikataa kukaa siti ya nyuma nikaenda kupanda basi kufika chalinze napata taarifa ile gari (Prado) imepatwa na ajali na wote waliokuwa ndani ya ile gari wamefariki..




Daah asee tangu hapo niliona uwepo wa Mungu kabisa na hakuna wakukuepusha/kukuletea majanga isipokuwa Mungu pekeake.
 
Back
Top Bottom