Tukio gani ulishawahi kufanya ukajiona mshamba sana?

Kutokana na kuwa mshabiki wa soka na mpondaji wa marefa wa ligi kuu Tanzania bara niliteuliwa kuwa refa katika mashindano ya Mpira wa miguu yaliyoandaliwa na mbunge wetu.
Siku ya Kwanza nikapangiwa kuwa referee wa pembeni yani linesman shida ilikuja pale nilipokuwa nakimbia kuanzia kona hadi kona yaani kutoka kwenye kibendera hadi kibendera na nilikuwa namshangaa mwenzangu wa upande wa pili anaishia katikati ya uwanja nakumwona mvivu wa kukimbia.
Nilipogundua kuwa nilikuwa nimefanya makosa nilijifanya mnyonge na nilihama mkoa.

Nilitamani ningejuana na realMamy na Nifah wangenipa ABC zihusuzo maswala uamuzi.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]nimecheka kwa sauti
 
Enzi za kwacha kutoka Mbeya kwenda Iringa.
Rujewa pale niko na Bro.
Tumezama ndani tupige chai na mayai aisee chai ya moto balaa, puliza puliza pale kumbe bus limepiga honi likatimka.
Aisee tulitoka baru kulifukuzia yule juma ikangaa atasubiri.
Brother alinitangulia mi nilikua nimevaa glocks zile mpya tu.
Da nikaona zinachelewesha
Tupa kule piga mibio mpk bro nikamuacha mbali tu simamisha bus likasimama.dah kucheck bro viatu sina.
Ikabidi dereva asubiri tufwate viatu aisee,
Kulikua hamna watu njiani enzi hizo vinginevyo tusingevikuta.
 
Unatoka Meatu sehemu gani?
Sio kwa ubaya.
 
kweli ni babukijana sio kwa hizo mbio mkuu [emoji1787] itakuwa ni zile bus za kitambo, kwa hizi bus za yutong mapema tu ushaachwa
 
Babu Kijana we ni noma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…