Tukio gani ulishawahi kufanya ukajiona mshamba sana?

Tukio gani ulishawahi kufanya ukajiona mshamba sana?

Sintosahau ushamba nilioufanya nilipokuwa darasa la tatu niliingia chumbani kwa bimkubwa, maana kuna perfum alikuwa akijipulizia nilipenda harufu yake nikavizia siku hayupo nikachukua namimi nijipulizie sasa nimejipulizia akili ikanituma bado kwenye macho nayo yanahitaji kunukia nikapulizia, ebwanaee haikupita dakika macho yakaanza kuniwasha mara pu bimkumkubwa kaingia palikuwa hapatoshi..kweli ushamba mzigo.
ahahahaha me perfume nilikua hata sijui majina yake nilivoanza kupuliza napuliza mpaka kwenye viatu mpaka mdomoni alooh [emoji1787]
 
Habari wakuu
Mara ya kwanza kujiunga na huduma za kibenki nilienda kwenye tawi la benki wakanisajili ikafika mda wa kufanya kadi iwe active.
Nimeenda kwenye ATM na yule mhudumu akaiweka kadi ndani ya ATM ananiambia chagua lugha, me hapo hata sijui wanabonyeza wapi, akanionesha zile button za pembeni nikachagua, akanambia bonyeza hapa nikabonyeza, akasema weka namba ya siri nikaanza kuijaza.

Sasa yeye akatoka nimemaliza akakawia kuja. Namsubiri mara nashangaa kadi inamezwa nikamuita nikamuuliza mbona kadi imedumbukia tena, akasema aisee ungeitoa dah, me nikamwambia sasa hukuniambia, nilikaa pale saa zima nasubiri wailete dah!

Mara ya pili, nimeenda ATM pekeangu kufika kumbe ile ATM ni ya touchscreen haina buttons za pembeni zipo za namba tu maandishi yale ya pembeni kumbe unatouch, duh nikadata nje kuna bonge la foleni wanasubiri nitoke, naweka kadi naweka PIN nasubiri hola! duh nikaona nitoke hapa nishatolewa ushamba, hata nikaona kuuliza watanicheka nikaenda kutoa kwa wakala, haha dah!
ushamba mzigo
Enzi hizo mwaka 1992 nilipoenda kujifunza gereji sitasahau pale nilipoambiwa nipige jeki ili tutoe tairi nikashindwa sitosahau ile siku nilijiona mshamba kupita kiasi
 
Kukorogea masala kwenye chai nikidhani ni chocolate
Kujipaka sanitizer nikidhani ni mafuta
Alooh sitaki kukumbuka vingi
[emoji1787][emoji1787]aisee nilidhani nimeskia yote hii nayo kali
 
Kukabwa na nyama Sea cliff Hotel Kwani hawakutupa vijiko wala kunawa mikono.

Nilitakiwa kula kwa kisu na umma nami sijazoea. Nimezoea kutafuna nyama then nalitoa na kuanza kulivuta kwa mkono huku nikilitafuna tena.

Sasa kwa delegete ile niliyokuwa nayo na kila.mtu anakula kwa umma na kisu. Nikachukua linyama, nikalikata kidogo na kulitia mdomo. Tafuna dakika mbili tatu na kulimeza. Lioande likagoma kuingia.


Hahahaaa. Aibu ile😀😀😀😀😀
 
Nyingine kushindwa kujua kazi ya yale mavitambaa meupe pale Element Hotel Dar.

Kizunguzungu na kuanguka kwenye lift.😀😀😀
 
Back
Top Bottom