Tukio gani ulishawahi kufanya ukajiona mshamba sana?

ahahahaha me perfume nilikua hata sijui majina yake nilivoanza kupuliza napuliza mpaka kwenye viatu mpaka mdomoni alooh [emoji1787]
 
Enzi hizo mwaka 1992 nilipoenda kujifunza gereji sitasahau pale nilipoambiwa nipige jeki ili tutoe tairi nikashindwa sitosahau ile siku nilijiona mshamba kupita kiasi
 
Kukorogea masala kwenye chai nikidhani ni chocolate
Kujipaka sanitizer nikidhani ni mafuta
Alooh sitaki kukumbuka vingi
 
Kukorogea masala kwenye chai nikidhani ni chocolate
Kujipaka sanitizer nikidhani ni mafuta
Alooh sitaki kukumbuka vingi
[emoji1787][emoji1787]aisee nilidhani nimeskia yote hii nayo kali
 
Kukabwa na nyama Sea cliff Hotel Kwani hawakutupa vijiko wala kunawa mikono.

Nilitakiwa kula kwa kisu na umma nami sijazoea. Nimezoea kutafuna nyama then nalitoa na kuanza kulivuta kwa mkono huku nikilitafuna tena.

Sasa kwa delegete ile niliyokuwa nayo na kila.mtu anakula kwa umma na kisu. Nikachukua linyama, nikalikata kidogo na kulitia mdomo. Tafuna dakika mbili tatu na kulimeza. Lioande likagoma kuingia.


Hahahaaa. Aibu ileπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Nyingine kushindwa kujua kazi ya yale mavitambaa meupe pale Element Hotel Dar.

Kizunguzungu na kuanguka kwenye lift.πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…