Tukio kwenye mataa ya Mwenge: Tofauti ya Wazungu na Waafrika

Kuthamini kazi kama hizo ni kuendeleza kudumaza akili za wahusika
Sipingani nawe lakini sidhani kama ni sahihi. Kuna watu hufanya kazi za kubeba takataka na kuenda kuzitupa. Vipi hao nao kuthamini kazi zao ni kuwadumaza akili?! Wasipokuwepo kazi hizo zifafanywa na nani?! Kuna watu huokota makopo mifaani, tukisema wasifanye kopo zitaokotwa na nani?!

Nadhani kila kazi ina umuhimu wake na watu wanaopaswa kufanya. Ikiwa ni kazi ya halali na inampatia kipato kinacho mtosheleza kwa mahitaji yake na familia basi na tuache afanye. Tumuunge mkono maana soko la ajira Afrika bado changa. Usipojiajiri na kuwa mbunifu katika ajira yako huwezi toboa.
 
Watu wa Asia kamwe siwezi fanya kazi naye isipokuwa Mwisrael kidogo ana tofauti kubwa
Hivi unajua Ulaya watu hufanya kazi kwa masaa, yaani ikiwa muda wako wa kazi ni saa 1 asbh hadi saa 10 jioni utalipwa kutokana na huo muda. Na ikiwa uta over time pia ufalipwa. Sasa njoo Afrika uone, utafanya kazi mchana na wakati mwingine hadi usiku lakini malipo ni yale yale. Na unalipwa kwa tabu sana, hadi udanganye kuwa una tatizo ndio pengine utawahishiwa malipo yako.
 
Kuokota makopo au kubeba taka hizo kazi ni nzuri na nitawaunga mkono lakini hiyo ya kuosha gari sehemu za makutano ya magari ni kuchochea ajali pia . Chukulia watu kama wanaweza kupata hela nzuri hapo kwenye makutano ya magari hali itakuwaje. In short hapo siyo sehemu rafiki kwa kazi hiyo
 
Ukizungumzia hilo nakataa sababu kibongo bongo you will never be as fortunate as ukifanya kazi na mzungu!

Fanya kazi na wadosi,wabongo,wachina non of them care..Hawa watu hawana utu kabisa yani. Anakufanya kama punda wake tu. Fanya kazi masaa 12 akuhenyeshe na lugha mbovu mitusi juu ila by the end of the day akupe buku 5-7 kwa hali ya sasa na hajali umekula hujala yeye kazi yake ufanye tu! Na unafanyishwa mikazi hata nje ya scope ya makubaliano.

Ila siku ukipata kazi ya mzungu ndio utaelewa, system ya kazi iko straight utafanya jambo a,b,c kwa masaa 8! Baada ya masaa hayo ujira wako ni 80K au anakwambia kila lisaa limoja nitakulipa elfu 10...On top of that kuna buffet kwa ajili ya wafanyakazi mtakula through the day kisha
kuna transport allowance utachukua kila siku ni 10K. Natumai kazi itaenda vizuri ambapo kuna ugumu basi muombe kuelekezwa mumuone flani.

Unakuta kazi ni ya miezi mitatu tu ila mpaka kazi imeisha una kiwanja mahali. Achana na mzungu wewe!!!

Bongo sijawahi kutana na kazi ya mzungu ambayo haina maslahi, wanaoharibugi maslahi ni wabongo wenzetu walioko top management ambao wao wanachofanyaga ni kupiga panga salio tofauti na mikataba anayotoa mzungu mwenyewe!
 
Hawa ni miongoni mwa watu wansotakiwa kupigwa marufuku mijini!!! Waje vijijini tulime tufuge waachana na ujinga huo wa kufuta magari ya watu!!
 
Mkuu, mbona wazungu ni wengi wanaendesha gari za kawaida.kuna mzungu ana drive subaru yupo kenya na ana pesa. Hapa jirani yangu kuna wazungu wanapanda boda boda. Na wengine wana NOAH
Ukimsoma mleta mada vizuri utamuelewa
Asante kwa kunielewa. Na katika hii mada kuna logic, wala ishu sio aina ya gari. Mshikaji anapaswa afikiri zaidi ili apate kuelewa nimelenga nini katika mada hii.
 
Mkuu. Hata trafiki nao hufanya kazi barabarani tena all the time na luna wakati ajali huwakuta vile vile, lkn bado hilo haliwafanyi kuacha kufanya kazi yao. Vijana hawa wapo makini sana na wanatambua kuwa kuna ajali, ndio maana hufanya kazi zao wakati taa nyekundu zimewaka na gari zimesimama. Taa zinaporuhusu tu utaona wakikaa kando ya barabara.
 
Sawa mkuu lakini barabarani siyo sehemu ya kuoshea magari. Hao walitakiwa wapigwe marufuku
 
Sema kwenye suala la kutoa kwa moyo na ku appriciate nadhani inatokana na moyo wa mtu na mood aliyo nayo kwa muda huo, Wala sio wazungu wote na pia ata Africans tupo pia wenye moyo wa kutoa
 
Sema kwenye suala la kutoa kwa moyo na ku appriciate nadhani inatokana na moyo wa mtu na mood aliyo nayo kwa muda huo, Wala sio wazungu wote na pia ata Africans tupo pia wenye moyo wa kutoa
Yes, ni kweli lakini ni wachache cos sio asili yetu kusaidiana. Asili ya mtu haipotei Mkuu.
 
Africans bana.

Mzungu ni neno ambalo sipendi kulitumia.
Lakini hii mada kila mtu anajadili kuhusu mzungu kama miungu au aina fulani hivi ya demigods.

Ni akili tu ya kibinadamu pia wapo africans wengi wanaofanya hivyo ila kwakua ni mtu mwenye asili ya nje afrika basi ikawa sababu ya sifa zote hizi.
Na nina uhakika kama muafrika angefanya hivyo usingeandika hii thread.

Sina uhakika lakini ni vizuri ukasoma history ili kujua ni nani aliyefanywa mtumwa na nani aliyemfanya mwenzake mtumwa.
Kwa kuwaua,kuwatumia kama punda pia kuwafunga minyororo kama mbwa, kuwatesa na kuwadharirisha.
Bila kusahau yule jamaa mweusi aliyepigwa kabali ya goti mpaka kifo na polisi mweupe.
Pia bila kusahau ubaguzi juu ya mtu mweusi huko nje.

Alafu unasema wamweumba tofauti really?
Huyo aliyewaumba labda alikuwa high at the time.


Ni ajabu Africans mpaka leo bado wana ile low self esteem na inferiority mbele ya mzungu iliyotokana na history ya nyuma na kusahau kwamba wote ni binadamu waliotofautiana utashi na rangi iliyotokana na mazingira.

Mimi sioni cha ajabu hapo zaidi ya sign za low self esteem na inferiority complex.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…