A
Anonymous
Guest
Jioni ya tarehe 6, askari polisi waliovaa nguo za kiraia walifika katika Hospitali ya Selian jijini Arusha na kumtoa wodini kijana mmoja anayejulikana kwa jina la Lobulu Masiaya Tome. Baada ya kumpeleka katika eneo la mapokezi la hospitali hiyo, walimpiga pingu, wakampandisha kwenye gari na kuondoka naye.
Akiwa mikononi mwao, askari hao walimlazimisha Lobulu kuwapigia simu watu kadhaa na kuwaambia kuwa baba yake amefariki dunia. Watu waliofika kutoa mkono wa rambirambi walikamatwa na polisi waliokuwa wameweka mtego katika Hospitali ya Selian na kuondolewa eneo hilo kwa gari.
Hadi sasa, watu wafuatao bado wanashikiliwa na polisi:
Hii haiwezi kuwa njia inayokubalika kwa vyombo vya ulinzi na usalama kufanya kazi. Vitendo hivi ni vya nchi zilizofeli na wala si mfumo unaofanya kazi kwa kufuata misingi ya sheria. Utekaji, ukamataji wa kiholela, na kuwashikilia wananchi kinyume cha sheria lazima vikome.

- Salangat Mako
- Nangei Meitaya
- Ezekiel Kishau
- Thadeus Clamian
- Mtu mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Dickson