Tukio la kusisimua nililolishuhudia kwa macho yangu katika msitu wa Nairoto

Mkuu nipe muongozo Mimi mwenyewe nimegraduate mwaka huu sioni mbelee
 
Sijajua kwa upande huo sijabahatika kuwajua jamii hizo, hata hawa huwa mara nyingi wanalalamika kuvamiwa na majini wa baya kwenye ngome yao na kutokea vita baina yao.
Naunga mkono hoja zako kuwa ni kweli wapo majini wazuri wacha Mungu na wengine wabaya. Nilishapiga stori na mmoja akiwa ndani ya mwili mwa mtu aliyepandisha majini. Alikua mpole japo wenzake wawili ndio walikua waleta fujo.
Wana uwezo mkubwa sana hawa viumbe. Aliniambia mambo mengi ya ajabu kuhusu uso wa hii dunia, sisi tunaona juujuu tu.
Nakumbuka aliniambia anifunulie nione ya dunia kwa muda lakini alinipa sharti la kutokuogopa wala kushituka, kusikia hizo habari za masharti nikamwambia acha tu nibaki kujua hayahaya nayoona hayo mengine yasiyoonekana kwa macho ya nyama tuachane nayo.
 
Nahisi hiyo njia panda uliyopata sarafu ni ile ya MBUGANI PRIMARY nyuma ya Thaqaafa au ni nyingine?
 
Mkuu, tutashukuru sana ukituwekea hayo mambo ya ajabu aliyokwambia kuhusu uso wa dunia ili tujifunze kama story za wengine
 
Huyo jini Angekuwa mzuri angemuacha huyo mtu huru. Aende Yeye kwa majini wenzake. Kitendo cha kumkalia huyo mtu ni uvamizi na uharamia
 
Huyo jini Angekuwa mzuri angemuacha huyo mtu huru. Aende Yeye kwa majini wenzake. Kitendo cha kumkalia huyo mtu ni uvamizi na uharamia
Hilo usemalo ni kweli na nilimuuliza huyo jini na alisema yeye pia hapend kukaa kwa mtu huyo sababu anaumia lakini analazimishwa kukaa kwake sababu akikataa wale wanaomtuma wanampiga, kumtesa na kumpa adhabu kali. Kwa hiyo anaona ponapona yake ili asiuawe ni yeye kukaa humo.
 
Jamaa kanifurahisha pale walipoingia dukani wakamukuta jamaa kafa na dhahabu aliyoificha ktk kifungashio cha shingoni. Wakamalizia kusomba Dragon wakati pombe ni haramu huko matandani.
Dragonj sio pombe ni energy drink sawa na Azam energy
 
[emoji38][emoji38]
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mkuu nimekufuatilia masimulizi yako kuhusu majini unayoshirikiana nayo napata maswali mengi sana,

1.Faida ya kushirikiana nayo wewe ni ipi?wewe unapata faida gani na wao wanapata faida gani?
2.Wanamzunguziaje Yesu?je wanamfaham?
3.Umesema unasali na unapata maono kupitia Mungu,Je ulipomuuliza kuhusu hao viumbe alikujibu nini?
4.Hizo sauti unazikia wewe tu? je sio kwamba wewe ndio upo 'Possesed' na majini

Asante
 
Beautiful...
 
Nimesoma tangu mwanzo wa uzi na comment zake zote 1,500+,Uzi unasisimua sana.

Niwashukuru wadau wote humu nikianza na Kitoabu ,Mbwichichi na fyddell kwa simulizi zao,hakika zina mafunzo mengi na niwape pole pia kwa waliyoyapitia katika harakati za kutafuta maisha

Pia niwashukuru wachangiaji wote kwa namna moja au nyingine waliendelea kuchangamsha Uzi kwa kuuliza maswali au kujibu hoja mbalimbali wakati wasimuliaji wakuu wakiwa wameenda kuoga na majukumu mengine[emoji3]
Hapa nitawaja Kazakh destroyer,Angel Nylon na nicksonmoses na wachangiaji wote kwa ujumla wenu.

Bila kusahau wale waliokuwa wakiamsha amsha wasimuliaji kuleta muendelezo bila kuchelewa wakiongozwa na Jimena na hata wale waliojitolea kuzama PM kuwatisha au kuwabembeleza[emoji3]kwa namna yeyote ile,juhudi zao zimezaa matunda,naomba wakaze kidogo bado fyddell tunamdai episode za mwisho.

Ahsanteni[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
 
1)Faida ni kama kubadilishana mawazo,ufahamu,kusaidiana kwenye matatizo na furaha.

2)Yesu wanamfahamu,wanamzungumzia kama nabii anaefuatwa na watu walioamua kumfuata ikiwemo sisi na wanatambua makanisa kama nyumba za ibada, hawana ufahamu mkubwa sababu ya imani yao ni islamic.

3)Mara zote nilizomshirikisha Mungu hakunionesha hatari katika hilo,ndio maana mara zote naamini katika mipango yake maana ukomo wetu wa kufikiri uwezo wake huanzia hapo kujiinua.

4)Sauti hata wewe unaweza kuisikia maana hutumia kinywa cha mke wangu kuzungumza na sio nasikia peke yangu.

Sent from my Infinix X573S using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…