DADECK. ..
Nilikua nauchukulia poa huu Uzi, maana nilisomaga post ya kwanza post ya pili nikaitafuta wee nikaikosa so nikaamua kuachana nao, Leo nimesoma wooote. MAZEE hii dunia ni zaidi ya ujuavyo nimesoma hapo mikasa ya majini n.k daaaah moyo umeingia baridi sana.
Sisi watoto wa maskani tunaona kama movie vile lakini kiukweli watu mmepitia msoto. Binafsi sijawai kuona mchawi wala jini.
scenario ya kichawi ninayo kumbuka labda kukututana na vitu njia panda vimepasuliwa, picha linaanza nimeamka nawai shule Mimi na dogo flani mida ya asubui tayari jua limechomoza tumefika njia panda tukakuta mayai, Nazi na vitu vingine vimepasuliwa pia kulikua na shilingi kama 20 zilikua nyingi nyingi, so watu walikua wanapita wanaogopa nilipofika na yule dogo tukachukua zile chenchi zilizokuepo (zile shillingi 20)....Siku hiyo ilikua murua tulikula mandazi na barafu za kutosha pale Pamba primary......kila Siku tulikua tunapita hiyo njia tuone nani mwingine ataweka hela hapo.
Scenario ya pili nilipokua Chuo na mshikaji wangu tumetoka club, pikipiki ikaogopa kuendelea so tukaamua tutembee kwa mguu mida ya saa 9 kasoro usiku, kwa mbele njia panda tukamuona mtu hivi so kwasababu kulikua kuna vichaka tukapitia vichakani huku tunanyata. Dah kumbe alikua ni mwanamke anaoga alikua anapasua na nazi kitu kama hicho, mshikaji wangu akanambia hapa tusiondoke tuangalie mpaka mwisho (nadhani lile umbo la Yule mama lilichanganya). Daah kwa upande wangu nilitamani nimuibukie yule mwanamke pale sema uoga pia ulichangia, alimaliza mambo yake akasepa na sisi tukasepa nikaenda kupiga nyeto kwa kupitia taswira ya yule mwanamke.
Scenario ya tatu nimemaliza kucheck movie Nipo geto nataka kulala (nilipokua Chuo ) Mara nasikia juu ya bati kishindo Mara paka wanalia nje nikaona huu ni udwanzi, nilikua na Panga langu nikatoka nalo nje nikaanza kujiongelesha huku nikiwa nimejaa uoga ""oyaa acheni ungese kama mnajiweza jitokezeni tukutane" nikarudi ndani huku uoga umejaa nikasali nikalala sikuwai kusikia tena mpaka nimegraduate.
Kitu ambacho Baba alinambia katika maisha kuna nguvu mbili zina operate ni Nuru pamoja na Giza it depend na wewe huko wapi lakini vyote vinanguvu na vinafanya kazi.
Kuna kipindi mzee wangu alinihadhitia tulipokua wadogo aliamka asubui akakuta mtu kapasua Nazi mlangoni pamoja na karatasi ina maandishi ya kiarabu hakuwaza wala hakujipa time kufatilia tafsiri yake, alichoma hicho kikaratasi then akapiga ombi na mpaka leo anadunda na anao uwezo wa kufanya mambo yake ya maendeleo.
Mwisho, nitaogopa usiku nikikutana na mwizi au jambazi maana nitatumia akili nyingi kumzuia physically na sijui amebeba nini, ila siwezi muogopa mchawi maana yeye awezi kukupiga anafanya kunitisha . Ikitokea siku endapo nikipigwa kofi na mchawi na nisione kofi limetokea wapi hapo ndipo nitatoka barutiiiiiiii....