Tukio la Mtanzania kufariki Ethiopia: Kama kungekuwa na ubalozi wa Zanzibar huko labda ingesaidia

Asikwambie mtu wazanzibar wana hutu sana ,ukiona mzanzibar ana roho mbaya basi huyo mzanzibar wa magomeni au ilala.

Wabara wana umimi sana ,sasa serikali inashindwa vipi kugharamikia tukio kama ilo? JMT hawana funds za dharura?
Mkuu, umepiga hesabu Watanzania wangapi wanafariki nje na kuweza ku claim dharula, gharama za kuwasafirisha ni kiasi gani na bajeti za balozi zetu ni kiasi gani?

Au unalaumu serikali bila figures tu?

Sisi huku Marekani kila wiki watu wanachangishana kurudisha maiti Tanzania, na kila maiti gharama zinazidi $10,000, mara nyingine kufika hata $20,000 kutegemea na factors nyingi.

Sasa serikali itaweza kugharamia hawa watu?
 
Ni makosa makubwa kuandika message/post ukiwa na emotions, kwa sababu you will end up kuonyesha ujinga wako.
Acha matusi musaidia wacha kashifa huyo ni mutanzia enzako
 
Mbona mabilioni ya dollars yanatumika hovyo? Ndege tu zinanunuliwa kwa cash
 
Kama umeshindwa kuendesha nchi kwa kuwahudumia raia ,si uache jukumu hili waachie wengine?
Ndo pale inapokuja hoja ya kusema Vyama vingi ni kushindanisha fikra za kuendesha nchi.
Hii ni kuonesha CCM baada ya miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika na 58 uhuru wa Zanzibar (Mapinduzi) bado nyimbo ni ile ile ya umasikini.
sasa nani wa kulaumiwa?
Tuwalaumu wakoloni?
au Wapinzania?
Ni kwamba hatujuwi kuendesha nchi na maisha ya watu tunayaweka hatarini kwa kuwadanganya.RAIA.
WAKE UP TANZANIANS.
1961 Tanganyika population ilikuwa kiasi ya 8- 10 millions, na hali ya uchumi ilikuwa nzuri kwa wakati ule.
1964 Zanzibar ilikuwa na population ya watu laki 2 na nusu hivi - Tatu na GDP ilikuwa kubwa sana ,
tunajiuliz miaka 50 baadae Zanzibar ina population ya 2 million na Tanganyika 58 milioni kipitunajivunia katika kumuhudumia huyu MTANZNIA?

Stand up wake up fight for your rights.
 
Basi naufungwe huo ubalozi ,kama hauna badget
 
Jipange, usiwaachie wenzako mzigo.

Mimi nilishakataa kusafirishwa kurudi Tanzania, licha ya kuwa na bima ya maisha.

Sitaki ujinga wa kuomba msaada ubalozini wala kushughulisha familia kusafirisha mwili.
Naomba basi invitation letter hali ngumu nije nijaribu usa
 

Mkuu sina figure kwa maana ya namba halisi ila kama nyinyi huko mnamanage kuchanga na kusafirisha why serikali ishindwe wakati ina sources nyingi sana za mapato na kuna fedha hadi zinarudhishwa hazina kwa kukosa matumizi?

Ukiangalia hayo matukio yanatokea lakini si kwa kiwango cha serikali yetu kushindwa kuhandle,labda balozi zetu zingejitahidi kutoa elimu kwa waTZ wanaoishi nje ambao wamefuata process wawe wanachangishana monthly basis kwa ajili ya issue kama hizo na just incase wakipungukiwa basi ubalozi uwashike mkono.
 
Hata siku moja ubalozi wa tanzania popote duniani ulipo, haunaga msaada kwa mtanzania ukipata matatizo ndiyo tabia yao.
Awamu ya tano ndiyo chanzo cha tatizo za ukata ubalozini. Halafu ubalozi wa ethiopia ulipiga sana hela wanayopelekewa
 
Kuna kuwahudumia raia halafu kuna kuwachamba mavi wakinya.

Wewe utataka serikali ikuchambe mavi ukinya?

Chukua responsibility kwenye mambo ya familia, iachie serikali wajibu wa kutengeneza uchumi mzuri kiasi kwamba ndugu yenu akifa nje, mkikutana watu wanne wa familia moja, msishindwe kuchangishana kurudisha maiti kutoka Ethiopia.

Familia inayoshindwa kuchangishana kurudisha maiti kutoka Ethiopia ama imepigika, ama haina upendo.

Nakubaliana na wewe serikali imeshindwa kuendesha nchi, lakini kwa sababu tofauti.

Serikali kwa kiasi kikubwa imeshindwa kujenga uchumi unaowapa watu uwezo wa kuchangishana kurudisha maiti Tanzania.

Kwa lawama hizo, nitakuunga mkono.

Lakini kwa lawama za kutaka serikali ichukue jukumu la gharama za kurudisha mwili Tanzania hapo sitakuunga mkono.

Hilo ni jukumu la familia yenu, ndugu, jamaa na marafiki.

Kuna Watanzania wengi sana wanaishi nje wanafariki, wakitaka warudishiwe maiti zao wote nyumbani na serikali, bajeti za hizi balozi hazitatosha.
 
Basi naufungwe huo ubalozi ,kama hauna badget
Ubalozi unahudumia hata wanaoishi, hauwezi kufungwa kwa sababu hauna bajeti ya kuhudumia watu waliofariki.

Acha kupenda kila kitu ufanyiwe na serikali, iachie serikali ifanye mambo makubwa ya kitaifa, mambo ya kifamilia yamalizeni kifamilia.

Ukiendelea hivi utalalamika umekosa mke/ mume kwa sababu serikali haijakusaidia kutafuta mke/ mume.
 
Pole na Msiba, pili ni vizuri tukawa tunachukua bima ya matibabu .
Mwisho mchango wa ZnZ kwenye budget kuu ni 4% sasa sijui fedha hizo zinatosha kufungua Balozi kule wewe unapofikiria au kutaka.
Na pia kusafirisha wenye matatizo.
 
Kama huna figures hayo malalamiko mengine ni ulalamishi ambao hauko katika msingi makini.

Kama kuna Watanzania 100 tu kwa mwaka wanafariki Marekani nchi moja tu, kitu ambacho si kigumu kwa sababu mimi katika group moja tu napata msiba kama mmoja kila mwezi, na mimi sipati misiba yote, na ikiwa kusafirisha mwili mmoja wastani ni kama $15,000, hapo tayari unaongelea $1,500,000 kwa watu 100.

Dola milioni moja na nusu.Kusafirisha maiti tu.

Hiyo bajeti ya kusafirisha wanaofariki Marekani tu, hujagusa nchi nyingine, hujagusa kodi ya ofisi ya ubalozi, hujagusa kodi ya nyumba ya balozi, hujagusa mishahara ya wafanyakazi, hujagusa kusaidia wanaoumwa.
 
Hata siku moja ubalozi wa tanzania popote duniani ulipo, haunaga msaada kwa mtanzania ukipata matatizo ndiyo tabia yao.
Wacha uongo. Sema ulikuwa na shida gani ukashindwa kusaidiwa? Sio kila shida lazima Ubalozi utoe msaada. Vile vile hakuna fungu la misaada kama unavyofikiria. Kila issue itaangaliwa kwa mapana yake kama nchi inaweza kulitatua au la, na hii sio kwa Tanzania tu. Serikali zote ulimwenguni hufanya hivyo.

Then tunarudi kwenye basics, tiketi za ndege popote pale unaulizwa kama unataka kukata bima tuwe wepesi wa kuchukua hizi bima kila tunaposafiri, sio kifo tu hata dharura zingine. Cost ya hii Bima ni ndogo sana.
 
Mwaka jana Nchiya Oman Illeta Ndege Kuchukua raia wake wote waliokwama kwa sababu ya Corona na kuwarudisha Oman Free of charge.
Hii ndio kujali kwa nchi na raia wake.
Mkiambiwa mlipe kodi ili mambo kama haya yawekwe kwwnye bajeti mnalialia,tatizo likitokea kama hili mnalia sasa tuwaeleweje..suala la huduma Ni suala la kibajeti..na unaposema balozi zina mchanganyiko, kuna wabara na wazenji..sasa sijui tuwaeleweje...naona mtoa mada dhamira yako Ni kuleta maneno ya ubaguzi tu kama kaburu...wewe na kaburu hamna tofauti..
 
Jomba umewapa kasma kwenye bajeti ya Serikali..? Au unadhan fedha itoke wapi katika fungu lipi..Cha msingi hapa sisitiza watu wasikwepe Kodi walipe zaidi ili makusanyo yawepo yaweze kutoa huduma kama hizi mnazozililia...kuendesha nchi sio lelemama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…