Tukio la Mtanzania kufariki Ethiopia: Kama kungekuwa na ubalozi wa Zanzibar huko labda ingesaidia

Tukio la Mtanzania kufariki Ethiopia: Kama kungekuwa na ubalozi wa Zanzibar huko labda ingesaidia

Asikwambie mtu wazanzibar wana hutu sana ,ukiona mzanzibar ana roho mbaya basi huyo mzanzibar wa magomeni au ilala.

Wabara wana umimi sana ,sasa serikali inashindwa vipi kugharamikia tukio kama ilo? JMT hawana funds za dharura?
Mkuu, umepiga hesabu Watanzania wangapi wanafariki nje na kuweza ku claim dharula, gharama za kuwasafirisha ni kiasi gani na bajeti za balozi zetu ni kiasi gani?

Au unalaumu serikali bila figures tu?

Sisi huku Marekani kila wiki watu wanachangishana kurudisha maiti Tanzania, na kila maiti gharama zinazidi $10,000, mara nyingine kufika hata $20,000 kutegemea na factors nyingi.

Sasa serikali itaweza kugharamia hawa watu?
 
Kwanza pole sana kwa kuondokewa na mpendwa wetu, Mungu ampe kauri thabiti huko aendako ambako ni kwetu sote but jamani hebu tuweni realistic hapa; hivi kwa uwezo wa nchi yetu inawezekana kweli kusafirisha kila anaekufa huko nje kweli? Nchi gani duniani huaga inasafirisha raia wake waliofia nje ya nchi, hasa kama raia huyo kafia huko nje ya nchini mwake but alikwenda kwa shughuli zake binafsi? Kuna nchi ya namna hiyo hapa duniani kweli? I dont think so. Umesema kuna wanafunzi waliwahi kukwama kwenye nchi X na wabara hawakusaidiwa but wa visiwani, SMZ iliwasaidia, huoni (kama ni kweli ) Wazanzibar mko vizuri zaidi kuliko sisi wabara? Again, not sure, hao wanafunzi huko nje ya nchi, walipelekwa na serikali huko au wazazi/walezi wao? Tusijaribu kutengeneza sheria ambazo sisi wenyewe hatuna uwezo wa kuzitekeleza. Hilo la Zanzibar kua na ubalozi nchi zingine, ni wazo zuri but itabidi kwanza ijulikane kimataifa kwamba Zanzibar is a sovernity state na ikifanyika hivyo, nikwambie tu ukweli, nyie hamna uwezo wa ku finance balozi zenu nje ya nchi kwasasa, uchumi wenu bado unaitegemea sana BARA. Angalia tena bajeti yenu, chief financer ni nani?
Mbona mabilioni ya dollars yanatumika hovyo? Ndege tu zinanunuliwa kwa cash
 
Hela ya dharula unafikiri ubalozi mmoja unaweza kuhitaji kiasi gani kwa mwaka?

Unaelewa hiyo hela ya dharula inatokana na kodi ya wananchi na imepangiwa mambo mengi sana?

Unaelewa kwamba hizo balozi tayari zina madeni ya kulipa kodi za nyumba na mishahara ya watu?

Kwa nini Watanzania wengi tunapenda kuivika serikali mzigo wa matatizo yetu wenyewe?

Unajua GDP per capita ya Mtanzania mmoja wa kawaida kwa wastani ni kiasi gani na gharama za kusafirisha maiti ni kiasi gani?
Kama umeshindwa kuendesha nchi kwa kuwahudumia raia ,si uache jukumu hili waachie wengine?
Ndo pale inapokuja hoja ya kusema Vyama vingi ni kushindanisha fikra za kuendesha nchi.
Hii ni kuonesha CCM baada ya miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika na 58 uhuru wa Zanzibar (Mapinduzi) bado nyimbo ni ile ile ya umasikini.
sasa nani wa kulaumiwa?
Tuwalaumu wakoloni?
au Wapinzania?
Ni kwamba hatujuwi kuendesha nchi na maisha ya watu tunayaweka hatarini kwa kuwadanganya.RAIA.
WAKE UP TANZANIANS.
1961 Tanganyika population ilikuwa kiasi ya 8- 10 millions, na hali ya uchumi ilikuwa nzuri kwa wakati ule.
1964 Zanzibar ilikuwa na population ya watu laki 2 na nusu hivi - Tatu na GDP ilikuwa kubwa sana ,
tunajiuliz miaka 50 baadae Zanzibar ina population ya 2 million na Tanganyika 58 milioni kipitunajivunia katika kumuhudumia huyu MTANZNIA?

Stand up wake up fight for your rights.
 
Haya masuala yanajadilika kiuchumi, habari ya ngoja yakukute hazina tija.

Kama ubalozi hauna bajeti hauna bajeti tu.

Na hapa tunaelimishana kwamba ubalozi hauna wajibu wa kurudisha maiti ili waliofikiri huu ni wajibu wa ubalozi wajiandae kabisa yasiwakute.
Basi naufungwe huo ubalozi ,kama hauna badget
 
Jipange, usiwaachie wenzako mzigo.

Mimi nilishakataa kusafirishwa kurudi Tanzania, licha ya kuwa na bima ya maisha.

Sitaki ujinga wa kuomba msaada ubalozini wala kushughulisha familia kusafirisha mwili.
Naomba basi invitation letter hali ngumu nije nijaribu usa
 
Mkuu, umepiga hesabu Watanzania wangapi wanafariki nje na kuweza ku claim dharula, gharama za kuwasafirisha ni kiasi gani na bajeti za balozi zetu ni kiasi gani?

Au unalaumu serikali bila figures tu?

Sisi huku Marekani kila wiki watu wanachangishana kurudisha maiti Tanzania, na kila maiti gharama zinazidi $10,000, mara nyingine kufika hata $20,000 kutegemea na factors nyingi.

Sasa serikali itaweza kugharamia hawa watu?

Mkuu sina figure kwa maana ya namba halisi ila kama nyinyi huko mnamanage kuchanga na kusafirisha why serikali ishindwe wakati ina sources nyingi sana za mapato na kuna fedha hadi zinarudhishwa hazina kwa kukosa matumizi?

Ukiangalia hayo matukio yanatokea lakini si kwa kiwango cha serikali yetu kushindwa kuhandle,labda balozi zetu zingejitahidi kutoa elimu kwa waTZ wanaoishi nje ambao wamefuata process wawe wanachangishana monthly basis kwa ajili ya issue kama hizo na just incase wakipungukiwa basi ubalozi uwashike mkono.
 
Hata siku moja ubalozi wa tanzania popote duniani ulipo, haunaga msaada kwa mtanzania ukipata matatizo ndiyo tabia yao.
Awamu ya tano ndiyo chanzo cha tatizo za ukata ubalozini. Halafu ubalozi wa ethiopia ulipiga sana hela wanayopelekewa
 
Kama umeshindwa kuendesha nchi kwa kuwahudumia raia ,si uache jukumu hili waachie wengine?
Ndo pale inapokuja hoja ya kusema Vyama vingi ni kushindanisha fikra za kuendesha nchi.
Hii ni kuonesha CCM baada ya miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika na 58 uhuru wa Zanzibar (Mapinduzi) bado nyimbo ni ile ile ya umasikini.
sasa nani wa kulaumiwa?
Tuwalaumu wakoloni?
au Wapinzania?
Ni kwamba hatujuwi kuendesha nchi na maisha ya watu tunayaweka hatarini kwa kuwadanganya.RAIA.
WAKE UP TANZANIANS.
1961 Tanganyika population ilikuwa kiasi ya 8- 10 millions, na hali ya uchumi ilikuwa nzuri kwa wakati ule.
1964 Zanzibar ilikuwa na population ya watu laki 2 na nusu hivi - Tatu na GDP ilikuwa kubwa sana ,
tunajiuliz miaka 50 baadae Zanzibar ina population ya 2 million na Tanganyika 58 milioni kipitunajivunia katika kumuhudumia huyu MTANZNIA?

Stand up wake up fight for your rights.
Kuna kuwahudumia raia halafu kuna kuwachamba mavi wakinya.

Wewe utataka serikali ikuchambe mavi ukinya?

Chukua responsibility kwenye mambo ya familia, iachie serikali wajibu wa kutengeneza uchumi mzuri kiasi kwamba ndugu yenu akifa nje, mkikutana watu wanne wa familia moja, msishindwe kuchangishana kurudisha maiti kutoka Ethiopia.

Familia inayoshindwa kuchangishana kurudisha maiti kutoka Ethiopia ama imepigika, ama haina upendo.

Nakubaliana na wewe serikali imeshindwa kuendesha nchi, lakini kwa sababu tofauti.

Serikali kwa kiasi kikubwa imeshindwa kujenga uchumi unaowapa watu uwezo wa kuchangishana kurudisha maiti Tanzania.

Kwa lawama hizo, nitakuunga mkono.

Lakini kwa lawama za kutaka serikali ichukue jukumu la gharama za kurudisha mwili Tanzania hapo sitakuunga mkono.

Hilo ni jukumu la familia yenu, ndugu, jamaa na marafiki.

Kuna Watanzania wengi sana wanaishi nje wanafariki, wakitaka warudishiwe maiti zao wote nyumbani na serikali, bajeti za hizi balozi hazitatosha.
 
Basi naufungwe huo ubalozi ,kama hauna badget
Ubalozi unahudumia hata wanaoishi, hauwezi kufungwa kwa sababu hauna bajeti ya kuhudumia watu waliofariki.

Acha kupenda kila kitu ufanyiwe na serikali, iachie serikali ifanye mambo makubwa ya kitaifa, mambo ya kifamilia yamalizeni kifamilia.

Ukiendelea hivi utalalamika umekosa mke/ mume kwa sababu serikali haijakusaidia kutafuta mke/ mume.
 
Wengi watashangazwa na na mada ya hapo juu.

Taratibu fuatilia

Tare 21/04/2021 siku ya juma tano, Dada yangu Fatma Said alifariki dunia Nchini Ethiopia akitokea Dubai kuja Zanzibar (Tanzania).
Akiwa ndani ya ndege 'Fly Dubai' aliumwa ghafla na kuilazimisha ndege hiyo kutua kwa dharura nchini Ethiopia ikiwa nio kiwanja cha karibu kwa walipokuwa.

Tukio hili la kumshusha pale ni sehemu ya taibu za ndege inapotiokea dharura. Mgonwa alipelekwa Hospitali na Kufarikiduni muda mchache baada ya kufika hospitali.

Yamkini serikali ya Ethiopia iliarifu ofisi ya Kibalozi ya TANZANIA kwa hatua stahiki.

Wana familia nao tulipopata habari tuliwasiliana na Balozi ili kujua hatua gani zifanywe ili Mwili wa marehemu urejeshwe Nyumbani kwa mazishi. Balozi wa Tanzania alianza kutudanganya na kutupiga danadana eti akidai kuwa hana FUND za kugharamia matukio ya aina hii.

Hatimae ilitubidi wanafamilia tulipishwe Gharama za Hospitali, Kusafirisha mwili na kila kilichohusu kusafirishwa kwa mwili husika.

Mwili ulifika jana tarehe 27/04/2021 kwa ndege ya Cargo ya Ethiopia Air Line.

Nilianza kujiuliza NINI FAIDA YA KUWA NA BALOZI NCHINI ETHIOPIA? Lakini mara nikakumbuka kuwa kama Zanzibar ingelikuwa na Ubalozi wake kule tungelipata matokeo tofauti?

Ilishawahi kutokea wanafunzi wa Tanzania walioko nje nchi fulani(siitaji) walipungukiwa na Masurufu ya matumizi, Wale wa Zanzibar wakatumiwa na SMZ fedha za kujikimu na wale wa Bara wakalazimika kurudi au familia zao kutuma fedha.

Nimeyasema haya nikiwa na Uchungu mkubwa wa kuona kuwa MUUNGANO WETU umekuwa kikwazo kwa raia wa Zanzibar .HILI NALO NI MOJA YA CHANGAMOTO ZA MUUNGANO kwenye mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa. We are not treted equaly.

Namuoba Waziri wa mambo ya nje Ahusike na tukio hili la Ethiopia kwani Ubalozi wa TZ haukusaidia lolote kifedha katika jambo hi la Marehemu.

Isije ikatumwa Invoice ya kuonesha kuwa Ubalozi ulitumia fedha,itakuwa ni Upigaji wa fedha za serikali.

Nawakilisha.
Pole na Msiba, pili ni vizuri tukawa tunachukua bima ya matibabu .
Mwisho mchango wa ZnZ kwenye budget kuu ni 4% sasa sijui fedha hizo zinatosha kufungua Balozi kule wewe unapofikiria au kutaka.
Na pia kusafirisha wenye matatizo.
 
Mkuu sina figure kwa maana ya namba halisi ila kama nyinyi huko mnamanage kuchanga na kusafirisha why serikali ishindwe wakati ina sources nyingi sana za mapato na kuna fedha hadi zinarudhishwa hazina kwa kukosa matumizi?

Ukiangalia hayo matukio yanatokea lakini si kwa kiwango cha serikali yetu kushindwa kuhandle,labda balozi zetu zingejitahidi kutoa elimu kwa waTZ wanaoishi nje ambao wamefuata process wawe wanachangishana monthly basis kwa ajili ya issue kama hizo na just incase wakipungukiwa basi ubalozi uwashike mkono.
Kama huna figures hayo malalamiko mengine ni ulalamishi ambao hauko katika msingi makini.

Kama kuna Watanzania 100 tu kwa mwaka wanafariki Marekani nchi moja tu, kitu ambacho si kigumu kwa sababu mimi katika group moja tu napata msiba kama mmoja kila mwezi, na mimi sipati misiba yote, na ikiwa kusafirisha mwili mmoja wastani ni kama $15,000, hapo tayari unaongelea $1,500,000 kwa watu 100.

Dola milioni moja na nusu.Kusafirisha maiti tu.

Hiyo bajeti ya kusafirisha wanaofariki Marekani tu, hujagusa nchi nyingine, hujagusa kodi ya ofisi ya ubalozi, hujagusa kodi ya nyumba ya balozi, hujagusa mishahara ya wafanyakazi, hujagusa kusaidia wanaoumwa.
 
Hata siku moja ubalozi wa tanzania popote duniani ulipo, haunaga msaada kwa mtanzania ukipata matatizo ndiyo tabia yao.
Wacha uongo. Sema ulikuwa na shida gani ukashindwa kusaidiwa? Sio kila shida lazima Ubalozi utoe msaada. Vile vile hakuna fungu la misaada kama unavyofikiria. Kila issue itaangaliwa kwa mapana yake kama nchi inaweza kulitatua au la, na hii sio kwa Tanzania tu. Serikali zote ulimwenguni hufanya hivyo.

Then tunarudi kwenye basics, tiketi za ndege popote pale unaulizwa kama unataka kukata bima tuwe wepesi wa kuchukua hizi bima kila tunaposafiri, sio kifo tu hata dharura zingine. Cost ya hii Bima ni ndogo sana.
 
Mwaka jana Nchiya Oman Illeta Ndege Kuchukua raia wake wote waliokwama kwa sababu ya Corona na kuwarudisha Oman Free of charge.
Hii ndio kujali kwa nchi na raia wake.
Mkiambiwa mlipe kodi ili mambo kama haya yawekwe kwwnye bajeti mnalialia,tatizo likitokea kama hili mnalia sasa tuwaeleweje..suala la huduma Ni suala la kibajeti..na unaposema balozi zina mchanganyiko, kuna wabara na wazenji..sasa sijui tuwaeleweje...naona mtoa mada dhamira yako Ni kuleta maneno ya ubaguzi tu kama kaburu...wewe na kaburu hamna tofauti..
 
Huyu Mtanzania alikuwa safarini peke yake, Ethiopia haikuwa destination yake , alishushwa kwa dharura ya kuumwa ghafla na umauti ukamfika huko.Sisi hatuna familia wala jamaa kule.
Kama balozi yupo ,unadhani nanai awajibike kutowa msaada?
kama hawalipi gharama zote , hata kuchangia sehemu ya Gharama ubalozi hauwezi ?
Jomba umewapa kasma kwenye bajeti ya Serikali..? Au unadhan fedha itoke wapi katika fungu lipi..Cha msingi hapa sisitiza watu wasikwepe Kodi walipe zaidi ili makusanyo yawepo yaweze kutoa huduma kama hizi mnazozililia...kuendesha nchi sio lelemama
 
Back
Top Bottom