Tukio la Mtanzania kufariki Ethiopia: Kama kungekuwa na ubalozi wa Zanzibar huko labda ingesaidia

Tukio la Mtanzania kufariki Ethiopia: Kama kungekuwa na ubalozi wa Zanzibar huko labda ingesaidia

Wengi watashangazwa na na mada ya hapo juu.

Taratibu fuatilia

Tare 21/04/2021 siku ya juma tano, Dada yangu Fatma Said alifariki dunia Nchini Ethiopia akitokea Dubai kuja Zanzibar (Tanzania).
Akiwa ndani ya ndege 'Fly Dubai' aliumwa ghafla na kuilazimisha ndege hiyo kutua kwa dharura nchini Ethiopia ikiwa nio kiwanja cha karibu kwa walipokuwa.

Tukio hili la kumshusha pale ni sehemu ya taibu za ndege inapotiokea dharura. Mgonwa alipelekwa Hospitali na Kufarikiduni muda mchache baada ya kufika hospitali.

Yamkini serikali ya Ethiopia iliarifu ofisi ya Kibalozi ya TANZANIA kwa hatua stahiki.

Wana familia nao tulipopata habari tuliwasiliana na Balozi ili kujua hatua gani zifanywe ili Mwili wa marehemu urejeshwe Nyumbani kwa mazishi. Balozi wa Tanzania alianza kutudanganya na kutupiga danadana eti akidai kuwa hana FUND za kugharamia matukio ya aina hii.

Hatimae ilitubidi wanafamilia tulipishwe Gharama za Hospitali, Kusafirisha mwili na kila kilichohusu kusafirishwa kwa mwili husika.

Mwili ulifika jana tarehe 27/04/2021 kwa ndege ya Cargo ya Ethiopia Air Line.

Nilianza kujiuliza NINI FAIDA YA KUWA NA BALOZI NCHINI ETHIOPIA? Lakini mara nikakumbuka kuwa kama Zanzibar ingelikuwa na Ubalozi wake kule tungelipata matokeo tofauti?

Ilishawahi kutokea wanafunzi wa Tanzania walioko nje nchi fulani(siitaji) walipungukiwa na Masurufu ya matumizi, Wale wa Zanzibar wakatumiwa na SMZ fedha za kujikimu na wale wa Bara wakalazimika kurudi au familia zao kutuma fedha.

Nimeyasema haya nikiwa na Uchungu mkubwa wa kuona kuwa MUUNGANO WETU umekuwa kikwazo kwa raia wa Zanzibar .HILI NALO NI MOJA YA CHANGAMOTO ZA MUUNGANO kwenye mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa. We are not treted equaly.

Namuoba Waziri wa mambo ya nje Ahusike na tukio hili la Ethiopia kwani Ubalozi wa TZ haukusaidia lolote kifedha katika jambo hi la Marehemu.

Isije ikatumwa Invoice ya kuonesha kuwa Ubalozi ulitumia fedha,itakuwa ni Upigaji wa fedha za serikali.

Nawakilisha.
Poleni kwa kupotelewa na mpendwa wenu.Ila hapo ngoja niwatetee hao wa ubalozi,si dhani kama ni kazi ya ubalozi kusafirisha miili ya watanzania ,ila ninacho kijua ni kwamba wanaweza kufanya coordination na mawasiliano.Ila cost zote zibalipwa na ndugu.ubalozi hawana vifungu vya hivyo.nadhani walikwambia kweli kwamba hakuna hela.
 
Huyu Mtanzania alikuwa safarini peke yake, Ethiopia haikuwa destination yake , alishushwa kwa dharura ya kuumwa ghafla na umauti ukamfika huko.Sisi hatuna familia wala jamaa kule.
Kama balozi yupo ,unadhani nanai awajibike kutowa msaada?
kama hawalipi gharama zote , hata kuchangia sehemu ya Gharama ubalozi hauwezi ?
Pole sana ndugu yangu kwa msiba uliokufika
Lakini sichelei kukuambia kuwa wewe ni kiazi, unataka balozi igharamie kwani Serikali ndio iliyompeleka/mtuma ndugu yenu huko nchi za nje? Au ni mfanyakazi wa Serikali?
 
Sijazungumzia watu wote warudishwe kama unavyozungumza wewe Nchi inayojali raia wao naona kabisa hata wanapozungumzia maendeleo yanaonekana kama hujali raia wako utaendelea kuwa hapo hapo tuu wapo wengine wenye uwezo wanajigharamia wenyewe ni vile tupo katika Nchi ambazo ufisadi umechukua nafasi kubwa sana nakumbuka huko ubalozini kuna dili za kifisadi sana sijui ile kesi ya ukarabati na ununuzi wa ubalozi wa Tanzania huko iliishaje...
Sasa wewe ukitaka privilege hii kwa ndugu yako kwa nini wengine wote wasidai hivyo hivyo?

Wewe una u specil gani kuzidi wengine?
 
Huyu Mtanzania alikuwa safarini peke yake, Ethiopia haikuwa destination yake , alishushwa kwa dharura ya kuumwa ghafla na umauti ukamfika huko.Sisi hatuna familia wala jamaa kule.
Kama balozi yupo ,unadhani nanai awajibike kutowa msaada?
kama hawalipi gharama zote , hata kuchangia sehemu ya Gharama ubalozi hauwezi ?
Brother yaache tu hayo hapa utakereka tu, mbona tunaona wana andaa chakula kwenye mahotel na timu za mpira ila kumsadia mtu alie pata matatizo inakua shida hiyo Tanzania na watanzania
 
Mimi nisamehewe bure.

Ila sionagi umuhimu wa kusafirisha maiti sehemu moja kwenda nyingine, haina mantiki (kwangu mimi) ni kuongeza gharama kwa jambo lisilo na tija.

Unakuta mtu wakati anaumwa huoni michango au juhudi za kuchangia pesa nyingi huyu ili mtu apate matibabu bora apone, ila akifa sasa mapesa mengi huchangwa sijui kusafirisha sijui kuweka mashughuli, baada ya mazishi familia inaendelea na msoto.

Ukifia england zikwa hukohuko
Ukifia masasi kwenu upareni zikwa hukohuko

Hata ukizikwa kwenu hamna faida yoyote itapatikana kwa kuzikwa kwako nyumbani kwako.
Mimi nilishaacha maagizo, sitaki kusafirishwa kurudi Tanzania.

Pia sitaki kuzikwa nitachomwa moto na majivu yangu kurushwa baharini.

Kila mtu akitaka kuzikwa baada ya miaka 1,000 sehemu kubwa sana itakuwa makaburi mpaka kujenga mambo ya maendeleo itakuwa shida.

Wakati barabara ya Maliki kutoka East Upanga kwenda juu Muhimbili West Upanga inajengwa, serikali ilipata tabu sana, kwa sababu barabara ilikuwa inakatisha kwenye makaburi ya Tambaza yaliyokuwepo pale miaka mingi sana.

Ilibidi makaburi yahamishwe ili barabara ijengwe.

Sitaki kuvipa tabu vizazi vya baadaye.
 
Pole...
Ticket yoyote ya ndege ina insurance nyingi ikiwamo matibabu mambo ambayo hatujuwi ama hatuisomi.

Jamaa yangu aliwahi kumsafirisha baba yake kumpeleka US na kule akatibiwa kwa ticket ya ndege.. am not sure how inafanyika ila ni ticket ya kawaida (bila additional insurance) imefaa atibiwe

Am sure hizi ni gharama za shirika la ndege hivyo fuatilia kwa wanasheria wanaojua mambo ya aviation ama wanasheria wa kimataifa unaweza kuli sue shirika la ndege ukapigwa check nene...

Wazo tu ila sio mwanasheria ama mjuaji..
Wengi watashangazwa na na mada ya hapo juu.

Taratibu fuatilia

Tare 21/04/2021 siku ya juma tano, Dada yangu Fatma Said alifariki dunia Nchini Ethiopia akitokea Dubai kuja Zanzibar (Tanzania).
Akiwa ndani ya ndege 'Fly Dubai' aliumwa ghafla na kuilazimisha ndege hiyo kutua kwa dharura nchini Ethiopia ikiwa nio kiwanja cha karibu kwa walipokuwa.

Tukio hili la kumshusha pale ni sehemu ya taibu za ndege inapotiokea dharura. Mgonwa alipelekwa Hospitali na Kufarikiduni muda mchache baada ya kufika hospitali.

Yamkini serikali ya Ethiopia iliarifu ofisi ya Kibalozi ya TANZANIA kwa hatua stahiki.

Wana familia nao tulipopata habari tuliwasiliana na Balozi ili kujua hatua gani zifanywe ili Mwili wa marehemu urejeshwe Nyumbani kwa mazishi. Balozi wa Tanzania alianza kutudanganya na kutupiga danadana eti akidai kuwa hana FUND za kugharamia matukio ya aina hii.

Hatimae ilitubidi wanafamilia tulipishwe Gharama za Hospitali, Kusafirisha mwili na kila kilichohusu kusafirishwa kwa mwili husika.

Mwili ulifika jana tarehe 27/04/2021 kwa ndege ya Cargo ya Ethiopia Air Line.

Nilianza kujiuliza NINI FAIDA YA KUWA NA BALOZI NCHINI ETHIOPIA? Lakini mara nikakumbuka kuwa kama Zanzibar ingelikuwa na Ubalozi wake kule tungelipata matokeo tofauti?

Ilishawahi kutokea wanafunzi wa Tanzania walioko nje nchi fulani(siitaji) walipungukiwa na Masurufu ya matumizi, Wale wa Zanzibar wakatumiwa na SMZ fedha za kujikimu na wale wa Bara wakalazimika kurudi au familia zao kutuma fedha.

Nimeyasema haya nikiwa na Uchungu mkubwa wa kuona kuwa MUUNGANO WETU umekuwa kikwazo kwa raia wa Zanzibar .HILI NALO NI MOJA YA CHANGAMOTO ZA MUUNGANO kwenye mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa. We are not treted equaly.

Namuoba Waziri wa mambo ya nje Ahusike na tukio hili la Ethiopia kwani Ubalozi wa TZ haukusaidia lolote kifedha katika jambo hi la Marehemu.

Isije ikatumwa Invoice ya kuonesha kuwa Ubalozi ulitumia fedha,itakuwa ni Upigaji wa fedha za serikali.

Nawakilisha.
 
Sasa wewe ukitaka privilege hii kwa ndugu yako kwa nini wengine wote wasidai hivyo hivyo?

Wewe una u specil gani kuzidi wengine?
Mkuu nadhani unajichanganya nazungumzia kwa wahitaji mimi sihitaji kitu chochote kutoka ubalozi wa Tanzania na pia kuchangia kwa wahitaji sio kwamba mimi nahitaji mimi huko nilishatoka kitambo namshukuru Mungu...
 
Brother yaache tu hayo hapa utakereka tu, mbona tunaona wana andaa chakula kwenye mahotel na timu za mpira ila kumsadia mtu alie pata matatizo inakua shida hiyo Tanzania na watanzania
Watanzania wengi wanapenda sana kusaidiwa na serikali.

Halafu wengi wanaona kila msaada ni haki yao hata kama hakuna hiyo haki.

Na wengi ni watu wa kupenda kusaidiwa wao, kwenye kusaidia hawapo na wala hawajali wengine.

Mtu anaweza kulalamika ubalozi umrudishie maiti ya ndugu yake Tanzania, wakati hajui hata bajeti ya ubalozi ni kiasi gani, gharama za kurudisha maiti ni kiasi gani, na kuna Watanzania wangapi wanakufa kila mwaka.

Ni ulalamishi fulani wa kijingajinga usiokwenda na data wala kufikiria wengine.

Ni aina fulani ya ubinafsi wa kujiweka wewe mbele bila kufikiria wengine na nchi.

Zaidi, ni tabia mbaya sana ya kukosa kujitegemea.
 
Suala si ukoefu wa Fund , bali Nchi yetu ina Policy mbaya kwa raia wake.
Iliwahikutokea miakaya nyuma Pale Thailand , Wageni walikamatwa kutoka nchimbali mbali wakiwa hawana documents za kusafiria.
Serikali ya Thailand ikazishauri Balozi za nchi husika ziwapatie Raia wao Traveling Documents na wao watawaruhusu waishi na kufanya kazi bila kuwarudisha..
Mataifa yote yaliwapa raia wao Passport na kuwaacha wafanye kazi Thailand ,lakini TZ waliwarudisha Nyumbani bila huruma.
Balozi kule alikuwa Mapuri kama sikosei
November 14, 2006Omar Ramadhan Mapuri

Mimi huwa naona mabalozi wetu wanaenda kutalii nje huku tukitumia kodi zetu kufadhili huu utalii
 
Hakuna sehemu inaonesha mabalozi wa Tz huko nje wanatoka Tanganyika tu. Inawezekana huyo balozi pia ni mzanzibar ila hakukuwa na fedha za dharura Kama hiyo. Mwisho mabalozi huwa ni wanadiplomasia wanaotoka kwenye sehemu zote mbili za muungano.
 
Pole...
Ticket yoyote ya ndege ina insurance nyingi ikiwamo matibabu mambo ambayo hatujuwi ama hatuisomi.

Jamaa yangu aliwahi kumsafirisha baba yake kumpeleka US na kule akatibiwa kwa ticket ya ndege.. am not sure how inafanyika ila ni ticket ya kawaida (bila additional insurance) imefaa atibiwe

Am sure hizi ni gharama za shirika la ndege hivyo fuatilia kwa wanasheria wanaojua mambo ya aviation ama wanasheria wa kimataifa unaweza kuli sue shirika la ndege ukapigwa check nene...

Wazo tu ila sio mwanasheria ama mjuaji..
Haya mambo ni complex halafu huwa yanabadilika nchi kwa nchi, unaweza kwenda kwenye nchi yenye huduma za afya nzuri wakakupa urahisi wa kupata huduma.Ukaenda kwenye nchi zina huduma za afya mbaya ukakosa.

Sasa hapa mtu anaweza kuja akalaumu tu bila kufuatilia kwa ukaribu.

Inawezekana Ethiopia kuna vita huko, Ubalozi una mambo kemkem ya kufuatilia kwenye vita.

Mtu anataka ubalozi ugharamike kwa kumrudisha ndugu yao.Kwani wameshindwa kuweka kikao cha ndugu na kumchangia hela za kufidia gharama?

Mimi naweza kuilaumu serikali kwa kuwa na nchi yenye familia nyingi masikini, serikali imeshindwa kukuza uchumi.

Lakini siwezi kuulaumu ubalozi kwa kukosa bajeti ya kurudisha mwili Tanzania.
 
Mimi huwa naona mabalozi wetu wanaenda kutalii nje huku tukitumia kodi zetu kufadhili huu utalii
Yani hata kama kweli wanaenda kutalii, jukumu la kusafirisha maiti ni la familia, si la ubalozi.

Ubalozi unaweza kusaidia tu ku coordinate mambo.

Na hili si kwa nchi masikini tu, hata nchi tajiri kama Mrekani, mwili wa mtu kusafirishwa labda awe mwanajeshi au special situation mtu alikuwa hostage huko.

Vinginevyo watu wanaweza kukusaidia kwa jinsi msaada wa kibinadamu unavyowezekana, lakini ukisaidiwa usione haki yako, ni msaada tu, na msaada unaweza kupata au kukosa.

Sasa wabongo wengine wanataka kulazimisha msaada uwe haki yao.
 
Mkuu nadhani unajichanganya nazungumzia kwa wahitaji mimi sihitaji kitu chochote kutoka ubalozi wa Tanzania na pia kuchangia kwa wahitaji sio kwamba mimi nahitaji mimi huko nilishatoka kitambo namshukuru Mungu...
Nimetumia "wewe" kama mfano tu.

Hiyo iko applicable kwa yeyote.

Nakuuliza hivi.

Sasa mtu mmoja akitaka privilege hii kwa ndugu yake kwa nini wengine wote wasidai hivyo hivyo?

Huyo mtu mmoja ana u specil gani kuzidi wengine?
 
Pole...
Ticket yoyote ya ndege ina insurance nyingi ikiwamo matibabu mambo ambayo hatujuwi ama hatuisomi.

Jamaa yangu aliwahi kumsafirisha baba yake kumpeleka US na kule akatibiwa kwa ticket ya ndege.. am not sure how inafanyika ila ni ticket ya kawaida (bila additional insurance) imefaa atibiwe

Am sure hizi ni gharama za shirika la ndege hivyo fuatilia kwa wanasheria wanaojua mambo ya aviation ama wanasheria wa kimataifa unaweza kuli sue shirika la ndege ukapigwa check nene...

Wazo tu ila sio mwanasheria ama mjuaji..

Mkuu insurance yeyote ambayo unaweka kwenye ticket ya ndege ni add-on yani additional cost. Mtu una uamuzi wa kuongeza bima kwenye ticket au lah.

Tukiuliza kwanini mwendazake hakuwajibika kwa kuongeza insurance kwenye ticket yake au kuwa na bima nchi aliyotoka tunaonekana wakora.
 
Nimetumia "wewe" kama mfano tu.

Hiyo iko applicable kwa yeyote.

Nakuuliza hivi.

Sasa mtu mmoja akitaka privilege hii kwa ndugu yake kwa nini wengine wote wasidai hivyo hivyo?

Huyo mtu mmoja ana u specil gani kuzidi wengine?
Swala la kujali raia wako ni kipengele ila kutokana na makuzi ya Watanzania wengi hasa waliofanikiwa hawawezi kufikiri kuweka mazingira mazuri kwa wahitaji ndio maana hapa utaona hata wewe unaona ni kitu kisichowezekana...
 
Si suala la kutowezekana.

Kuna nchi zina uwezo mkubwa lakini hazirudishi maiti za raia wao nyumbani, unless wawe wafanyakazi wa serikali kama wanajeshi.

Kwa sababu raia inawabidi wawe na "personal responsibility".

Ukianza kupeleka hela za kurudisha raia ubalozini ndiyo mwanzo wa kuleta mzozo wa pesa kuliwa, kama zimeliwa kweli au kwa figisu tu za kusingiziana.

Ndiyo maana wenzetu wananunua bima, wanasoma small prints za tiketi, wanajiwekea akiba za dharula.

Sisi tunataka kila kitu ifanye serikali, hatuna personal responsibility.

Marekani ni nchi yenye utajiri mkubwa sana. Lakini ukiacha wafanyakazi wa serikali kama wanajeshi, raia wa kawaida akifariki nje ni jukumu la familia kusafirisha mwili. Si jukumu la serikali.

Serikali ilishaweka mifumo huko.Ilishaweka mifumo ya bima, ilishaweka mifumo ya atu kuwa na ajira na biashara.

Kwa kweli Wamarekani wengi ukiwambia mwili usafirishwe na serikali wanaweza kuona ni jambo la aibu.Mwili usafirishwe na serikali kwani huyu mtu hana ndugu? Yani wanaona hata kama huduma ya serikali ipo, hawaiamini, wanaona wao ndio wanaweza kupanga vizuri kumrudisha ndugu yao. Wtapanga kwa mapenzi ya ndugu, ndugu yao kurudishwa na serikali ni kama kazikwa na serikali, bila mapenzi ya ndugu.

Sasa sisi wengi tunapenda dezo.

Mimi nitailaumuserikali kwa kutoweka misingi ya uchumi mzuri.Wtu wamepigika, mpaka familia zinashindwa kujipanga kumrudisha ndugu yao.

Hapo nitailaumu serikali sana tu.

Lakini, kwenye gharama za kurudisha maiti, ni jambo la aibu maiti ya mtu ambayesi mfanyakazi a serikali kurudishwa na serikali. Pia ni jambo ambalo serikali yetu haiwezi kumudu.

Tujifunze kujitegemea, kukata bima, kuweka akiba, kuwa na emergency funds, sio kuishia kuitegemea serikali tu.
 
Back
Top Bottom