Swala la kujali raia wako ni kipengele ila kutokana na makuzi ya Watanzania wengi hasa waliofanikiwa hawawezi kufikiri kuweka mazingira mazuri kwa wahitaji ndio maana hapa utaona hata wewe unaona ni kitu kisichowezekana...
Si suala la kutowezekana.
Kuna nchi zina uwezo mkubwa lakini hazirudishi maiti za raia wao nyumbani, unless wawe wafanyakazi wa serikali kama wanajeshi.
Kwa sababu raia inawabidi wawe na "personal responsibility".
Ukianza kupeleka hela za kurudisha raia ubalozini ndiyo mwanzo wa kuleta mzozo wa pesa kuliwa, kama zimeliwa kweli au kwa figisu tu za kusingiziana.
Ndiyo maana wenzetu wananunua bima, wanasoma small prints za tiketi, wanajiwekea akiba za dharula.
Sisi tunataka kila kitu ifanye serikali, hatuna personal responsibility.
Marekani ni nchi yenye utajiri mkubwa sana. Lakini ukiacha wafanyakazi wa serikali kama wanajeshi, raia wa kawaida akifariki nje ni jukumu la familia kusafirisha mwili. Si jukumu la serikali.
Serikali ilishaweka mifumo huko.Ilishaweka mifumo ya bima, ilishaweka mifumo ya atu kuwa na ajira na biashara.
Kwa kweli Wamarekani wengi ukiwambia mwili usafirishwe na serikali wanaweza kuona ni jambo la aibu.Mwili usafirishwe na serikali kwani huyu mtu hana ndugu? Yani wanaona hata kama huduma ya serikali ipo, hawaiamini, wanaona wao ndio wanaweza kupanga vizuri kumrudisha ndugu yao. Wtapanga kwa mapenzi ya ndugu, ndugu yao kurudishwa na serikali ni kama kazikwa na serikali, bila mapenzi ya ndugu.
Sasa sisi wengi tunapenda dezo.
Mimi nitailaumuserikali kwa kutoweka misingi ya uchumi mzuri.Wtu wamepigika, mpaka familia zinashindwa kujipanga kumrudisha ndugu yao.
Hapo nitailaumu serikali sana tu.
Lakini, kwenye gharama za kurudisha maiti, ni jambo la aibu maiti ya mtu ambayesi mfanyakazi a serikali kurudishwa na serikali. Pia ni jambo ambalo serikali yetu haiwezi kumudu.
Tujifunze kujitegemea, kukata bima, kuweka akiba, kuwa na emergency funds, sio kuishia kuitegemea serikali tu.