Tukipika kuku nyumbani, mimi nalishwa vipapatio, vitoto vyangu vya umri wa miaka 5 na 8 ndio vinalishwa mapaja. Je, hii ni sahihi wakuu?

Mambo ya kushindana na watoto na mapaja ya kuku ni utoto! Waache wale
Halafu mwanaume unakujaje nyumbani haujapitia mahali ukala kitu yako maana wewe ndio jembe la kazi
Unakuja uko NUSU tumbo ukija home unagusagusa tu kilichobaki unawajazia
 
Kyagata umeshinda kwenye ajira saiv mapenzi tena mkuu
 
Suala la mgawanyo wa ulaji wa kuku kwa familia yenye baba itifaki lazima izingatiwe mdau yupo sahihi

Kwa mfano sisi baba yetu anapewa hayo mapaja lakin yeye hashobokei sana mamisosi anatuita anatugea lakini mama haachi kumpa hiyo mipaja na firigisi kwani ndio kawaida

Hata mm nimeoa napewa hvohvo ila nagusa tu nawapa madg kwa sababu sio mpenzi sana wa minyama
 
Nikiwa na mwanangu toka alipoanza kujua kula mpaka leo ana miaka 17 mimi namuachiaga ale mapaja ya kuku tena Yale yanaitwa robo kuku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…