Tukiri kwamba katika mfumo wa muungano uliopo, inawezekana raisi kutoka Zanzibar akafanya kazi kwa maslahi ya Zanzibar zaidi ya bara au ya muungano

Ni kweli ila Kuna kitu mfano huko nyuma kulikuwa na Tuhuma kuwa Tanganyika inaimeza Zanzibar akishika mzaznzibar uraisi wa muungano ndie huongoza kuhakikisha Zanzibar inamezwa na utamaduni wa mzaznzibar unaharibiwa Kwa sera kama za Ajira.Mfano Sasa hivi wako wazanzibari kibao wamepewa ajira bara matokeo Sasa muda mfupi tu wameshaharibika walikuja na hijabu Toka Zanzibar Sasa hivi kutembea vifua wazi na kuvaa vimini Wala hawaoni shida sababu wamekuja kwenye Jamii huru isiyowadhibiti uvaaji au tabia sababu huku Kuna utamaduni wa mtanganyika sio mzaznzibari ajira vyeo nk wanapewa lakini at the expense ya maadili ya kizanzibari na hawana mpango wa kurudi Zanzibar

Huku wanajisikia huru sana wakilewa hakuna wa kuwafokea,Wakifanya umalaya hayuko wa kuwafokea kama kwao Zanzibar

Nafikiri kuua uzanzibari wazanzibari waendelee kupewa nafasi zaidi kwenye muungano waje Tanzania bara kiwanda Cha kuua maadili na utamaduni wa mzaznzibari Wapewe na nafasi ndio namna Bora ya kuimeza Zanzibar.Kupitia kuua maadili na utamaduni wa mzanzibar mlipe vizuri afanye kazi ofisi moja na Wala kitimoto na walevi na wavaa wapendavyo na wajirusha viwannja halafu uone baada ya miaka mitano huyo mzànzibari Aliyekuja kufanya kazi kwenye taasisi za muungano kama ndie yule yule uashangaa ajira aliyopewa imezalisha shetani ambaye Zanzibar hatakiwi na yeye hataki Hana mpango wa kurudi Zanzibar
I beg to differ !
 
Hili ni jambo ambalo wenye hekima wanalielewa siku nyingi, na labda wengine wengi sasa wameanza kulielewa, kwamba kutokuwepo kwa usimamizi wa kiserikali wa upande wa bara kunatokeza nafasi kwa raisi akitoka Zanzibar kuwa na uwezekano wa kufanya mambo kwa namna ambayo inatoa maslahi makubwa upande wa Zanzibar kuliko upande wa bara au wa muungano kwa ujumla.

Lakini sio rahisi kwa raisi wa Tanzania atokaye bara kufanya kazi kwa maslahi ya bara zaidi kuliko visiwani, kwa kuwa Zanzibar ina serikali yake tayari ambayo inasimamia maslahi ya visiwani, na inajumuishwa katika serikali ya muungano.

Kuna mambo kadhaa yamekuwa yakijadiliwa ambayo nitayaainisha hapa chini. Haya ni maoni toka wadau mbalimbali na nayaweka hapa ili kutoa wigo wa kuyajadili, sio kama shutuma.

Maoni mojawapo ni kwamba udhaifu wa kutoa maslahi upande wa visiwani raisi akitoka visiwani unajitokeza hasa ukizingatia kwamba katiba ya Tanzania inampa raisi mamlaka makubwa ya kuamua mambo bila hata kujadiliana na viongozi wengine au kuwa na kikao rasmi kitakachowakilisha maoni ya upande wa bara. Rais kutoka visiwani ana uwezo wa kupanga baraza la mawaziri kimkakati ili kuinufaisha Zanzibar, na hakuna namna ya kuweza kumzuia. Labda mfano mzuri katika suala hili ni suala la DP World na bandari, ambapo Zanzibar waliikataa DP World kwa sababu wana uwakilishi wao wa kiserikali, tofauti na bara. Sasa inakuwa kama raisi wa kutoka visiwani aliiamulia Tanzania bara kuwa na DP World. Je kungekuwa na serikali ya Tanzania bara, hili lingekubalika?

Na pia kuna maoni kwamba kila inapotokea raisi akitokea Zanzibar, ule msukumo wa kutoka Zanzibar kutaka muungano urekebishwe au uvunjwe unakwisha. Swali ni kwa nini? Je, ni kwa sababu katika hivyo vipindi upande wa visiwani unaona kuwa unafaidika zaidi na uwepo wa raisi kutoka visiwani? Wengine wamedokeza kwamba wakati wa raisi Magufuli uchumi wa Tanzania ulionyesha kukua zaidi ya uchumi wa Zanzibar, lakini kwa sasa uchumi wa Zanzibar unakuwa kwa kasi zaidi ya ule wa Tanzania, kuonyesha kwamba upande wa bara kuna kushuka kwa kasi ya kukua kwa uchumi. Na wengi wanaona hili linaweza kuwa linachochewa na maslahi mengi ya kitaifa kuelekezwa upande wa visiwani kwa kuwa kuna raisi toka visiwani.

Labda lililo kubwa zaidi ni maoni kwamba ikiwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar uko katika hatari ya kuvunjika, au kwamba watu wa upande wa visiwani hawautaki japo hawasemi hivyo hadharani, hatuoni kwamba tunaweza kumpata raisi kutoka visiwani ambae hana imani na muungano, japo anadai kuutetea, na akafanya mambo kwa namna ambayo kama muungano ukivunjika basi awe amewanufaisha upande wa visiwani kwa namna ya kutosha, yaani akatumia fursa ya uraisi wake kuimarisha upande wa visiwani akijua muungano unaweza kuvunjika wakati wowote?

Mfano umetolewa kwamba wakati Jumuiya ya Afrika Mashariki ikikaribia kuvunjia miaka ya 1977, Wakenya wakijua hili kwamba walitaka kuivunja jumuia, walifanya mkakati wa mali za jumuiya ya mashariki kuhodhiwa upande wa Kenya. Siku jumuiya ya mashariki ilipovunjika Tanzania na Uganda walikuja kugundua kwamba Kenya walikuwa na mkakati huu siku nyingi na walitenda mambo wakijua hilo linakuja! Je philosophy hii inawezekana pia katika suala la muungano, kwa kuwa upande wa bara hakuna serikali itakayokuwa macho kusimamia maslahi ya bara?

Sasa haya ni mambo yanajadilika na ni muhimuhimu kuyatafakari katika suala la muungano. Ndio maana basi, tukiri kwamba katika mfumo wa muungano uliopo, inawezekana kabisa raisi kutoka Zanzibar akafanya kazi ya uraisi kwa maslahi ya Zanzibar zaidi ya bara au ya muungano. Kujifanya kama hilo haliwezekani ni kujidanganya, na haya mambo yasipojadiliwa, yanaweza kuleta madhara na chuki zisizostahili. Na lazima pia tukiri ni mambo kama haya ambayo yamekuwa yakichochea madai ya kuwapo na serikali ya kusimamia maslahi ya upande wa bara, kama ilivyo kwa upande wa visiwani.

Nini maoni yako?
Upuuzi mtupu uliouandika jambo tunalolipata ni Ile asilimia 4 yetu ambayo mlitunyonya miakaa yote hiyo sitini ya muungano ambayo ilikuwamo katika makubaliano yetu ya muungano.
 
Hiyo ni wazi kabisa kwa kuwa anakuwa hana maslahi na cho chote cha Tanganyika. Suluhisho hapa ni kuwa na serikali tatu.

Serikali ya Muungano itashughulikia masuala ya ulinzi wa Taifa na ya kimataifa tu wakati kila nchi itashughulikia masuala yake ya ndani.
Best option ni kuvunja muungano,huu ndo muungano wa hovyo duniani
 
Upuuzi mtupu uliouandika jambo tunalolipata ni Ile asilimia 4 yetu ambayo mlitunyonya miakaa yote hiyo sitini ya muungano ambayo ilikuwamo katika makubaliano yetu ya muungano.
Kuwa na dhana kwamba Tanzania bara inainyonya Tanzania visiwani ni sawa na kusema ndama ananyonyesha mama yake. Haiwezekani hata ungejaribu vipi.
 
Inshort tanganyika tume pigwa..na ni makosa Rais wa Tanzania awe kutoka Zanzibar ni uwendawazimu
 
Umewahi kujiuliza ni Watanganyika wangapi wanautaka muungano? Usije ukafanya kosa kudhani maoni ya viongozi wa serikali ni maoni ya wananchi, japo viongozi wa serikali wanasema wanachaguliwa na wananchi. Ingekuwa hilo ni kweli DP World ingekufa kifo cha ghafla.

Jiulize, kwa nini serikali haitaki kufanyike referandum for or against muungano?
Inajua ndo itakuwa mwisho wa muungano,maana wananchi wengi kwa pande mbili za muungano hawautaki huu muungano wa kulazimishana unaolindwa na dola kwa amri ya viongoz wachache,but l have a dream kwamba sku moja tusioijua muungano huu utakufa naTanganyika itaibuka tena,kila jambo lina mwisho
 
Kweli kabisa. Kulikuwa na sababu za msingi enzi za Nyerere kuifanya Zanzibar kuwa sehemu ya Tanzania kwa kuwa Tanzania ilijihusisha sana na masuala ya kupigania uhuru wa nchi za kusini mwa Afrika. Wakati huo makaburu wangeweza kuichukua Zanzibar kimabavu na kuikalia, na hili lingehatarisha usalama wa Tanganyika. Lakini katika dunia ya sasa Zanzibar haina tena strategic security significance kwa Tanganyika. Hatuna geopolitical enemies tena. Muungano ukivunjika ni sawa tu, na Zanzibar wakitaka wawe sehemu ya Oman ni sawa pia, haituhusu.
Sio kweli ht kdg,kama walikuwa na lengo hilo kwann hawakuichukua comoro ambayo ni kisiwa kipo krb na Tz?
 
Inajua ndo itakuwa mwisho wa muungano,maana wananchi wengi kwa pande mbili za muungano hawautaki huu muungano wa kulazimishana unaolindwa na dola kwa amri ya viongoz wachache,but l have a dream kwamba sku moja tusioijua muungano huu utakufa naTanganyika itaibuka tena,kila jambo lina mwisho
Hamna mtu mwenye akili anataka huu muungano kwa sababu una masumbufu mengi mno na chokochoko za watu wasiostaarabika. Kuna wengine hatuzitaki kabisa. Wakae na utumbatu yao. Tuseme ukweli, mtu kama mimi, common man on the street huku bara, muungano unanisaidia nini? Mtu yeyote wa bara, muungano unamsaidia nini? Halafu kila siku wale wanaonufaika zaidi na muungano ndio walalamishi wakubwa. Nyerere aliwaambia mnakuwa kama mtoto mchanga, mnajinyea, halafu tukitaka kuwatawaza msinuke nyie ndio mnalia, bado hawakuelewa.
 
Malalamiko ya muungano yapo toka G55, lakini walioshikilia nchi hawataki mabadiliko yoyote, Wana nguvu na watu wa kutetea muungano vyovyote ulivyo, matumaini ni kidogo, labda Mungu mwenyezi aingilie Kati, bila shaka mama anajua hizi fursa huwa hazijirudii, hawezi fanya makosa, ni zamu yao zenji, na ni zamu yao kwelikweli
 
Sio kweli ht kdg,kama walikuwa na lengo hilo kwann hawakuichukua comoro ambayo ni kisiwa kipo krb na Tz?
Comoro hatukuungana nayo lakini ilikuwa chini ya control ya Tanzania. Kuna wakati hata jeshi letu lilikuwa pale na kata kuna mapinduzi ya kijeshi yalizimwa na Tanzania. Hivyo tulikuwa na makubaliano ambayo yalifafanya tuwe salama. Nyerere hakuwa mtu mdogo bwana, alikuwa ligi kubwa yule sio mtu wa kusimamia mambo ya vijiweni kama raisi

Hata hapa juzi tu tulienda huko. Wanaongea kiswahili pia na vitu vyao vingi vinatoka Tanzania

On March 25, 2008, military forces of the Union of the Comoros, supported by African Union (AU) troops from Tanzania, Sudan and Senegal, landed on the Comorian island of Anjouan. They met little resistance and took control of the island quickly in order to topple the regime of renegade Anjouan strongman Mohammed Bacar. He had ruled Anjouan legally and illegally, initially coming to power in an island coup in 2001, then being elected Anjouan’s president in 2002, and since 2007 refusing to step down with the expiration of his five-year mandate.
 
Hili ni jambo ambalo wenye hekima wanalielewa siku nyingi, na labda wengine wengi sasa wameanza kulielewa, kwamba kutokuwepo kwa usimamizi wa kiserikali wa upande wa bara kunatokeza nafasi kwa raisi akitoka Zanzibar kuwa na uwezekano wa kufanya mambo kwa namna ambayo inatoa maslahi makubwa upande wa Zanzibar kuliko upande wa bara au wa muungano kwa ujumla.
Wa kulaumiwa ni jiwe. Jiwe ndiye muasisi wa upuuzi huu wa kuipendelea kwao na wa kwao..

Mama Samia anafuata nyayo ,za dikteta.
 
Comoro hatukuungana nayo lakini ilikuwa chini ya control ya Tanzania. Kuna wakati hata jeshi letu lilikuwa pale na kata kuna mapinduzi ya kijeshi yalizimwa na Tanzania.
Acha uwongo. Comoro haijawahi kuwa chini ya control ya Tanzania. Jaribio la Mapinduzi ya kijeshi nchini humo kuzimwa na JWTZ ilikuwa ni maombi maalumu kama ilivyokuwa kwa Uganda chini ya Obote
 
Wa kulaumiwa ni jiwe. Jiwe ndiye muasisi wa upuuzi huu wa kuipendelea kwao na wa kwao..

Mama Samia anafuata nyayo ,za dikteta.
Unajua uko very right. Lakini kama raisi Samia anapendelea Zanzibar, anapaswa kuwa na busara ya kuelewa kwamba mazingira ya Magufuli kupendelea Chato ni tofauti sana na mazingira ya Samia kama raisi kupendelea Zanzibar. Asipoelewa hilo basi tuna tatizo kubwa kuliko tunavyodhani.
 
Acha uwongo. Comoro haijawahi kuwa chini ya control ya Tanzania. Jaribio la Mapinduzi ya kijeshi nchini humo kuzimwa na JWTZ ilikuwa ni maombi maalumu kama ilivyokuwa kwa Uganda chini ya Obote
Sawa, Comorro haijawahi kuwa chini ya control ya Tanzania. Officially. Wewe ulitaka tuitangazie dunia, jamani eeh, Comoro iko chini ya control yetu.

Unapopinduliwa, na kurudishwa madarakani na raisi wa nchi nyingine, unafikiri hutakuwa chini ya control yake?

Au Uganda ya Lule, Binaisa, haikuwa chini ya control ya Tanzania? Ongeza elimu uelewe siasa zinavyoenda
 
Hili ni jambo ambalo wenye hekima wanalielewa siku nyingi, na labda wengine wengi sasa wameanza kulielewa, kwamba kutokuwepo kwa usimamizi wa kiserikali wa upande wa bara kunatokeza nafasi kwa raisi akitoka Zanzibar kuwa na uwezekano wa kufanya mambo kwa namna ambayo inatoa maslahi makubwa upande wa Zanzibar kuliko upande wa bara au wa muungano kwa ujumla.

Lakini sio rahisi kwa raisi wa Tanzania atokaye bara kufanya kazi kwa maslahi ya bara zaidi kuliko visiwani, kwa kuwa Zanzibar ina serikali yake tayari ambayo inasimamia maslahi ya visiwani, na inajumuishwa katika serikali ya muungano.

Kuna mambo kadhaa yamekuwa yakijadiliwa ambayo nitayaainisha hapa chini. Haya ni maoni toka wadau mbalimbali na nayaweka hapa ili kutoa wigo wa kuyajadili, sio kama shutuma.

Maoni mojawapo ni kwamba udhaifu wa kutoa maslahi upande wa visiwani raisi akitoka visiwani unajitokeza hasa ukizingatia kwamba katiba ya Tanzania inampa raisi mamlaka makubwa ya kuamua mambo bila hata kujadiliana na viongozi wengine au kuwa na kikao rasmi kitakachowakilisha maoni ya upande wa bara. Rais kutoka visiwani ana uwezo wa kupanga baraza la mawaziri kimkakati ili kuinufaisha Zanzibar, na hakuna namna ya kuweza kumzuia. Labda mfano mzuri katika suala hili ni suala la DP World na bandari, ambapo Zanzibar waliikataa DP World kwa sababu wana uwakilishi wao wa kiserikali, tofauti na bara. Sasa inakuwa kama raisi wa kutoka visiwani aliiamulia Tanzania bara kuwa na DP World. Je kungekuwa na serikali ya Tanzania bara, hili lingekubalika?

Na pia kuna maoni kwamba kila inapotokea raisi akitokea Zanzibar, ule msukumo wa kutoka Zanzibar kutaka muungano urekebishwe au uvunjwe unakwisha. Swali ni kwa nini? Je, ni kwa sababu katika hivyo vipindi upande wa visiwani unaona kuwa unafaidika zaidi na uwepo wa raisi kutoka visiwani? Wengine wamedokeza kwamba wakati wa raisi Magufuli uchumi wa Tanzania ulionyesha kukua zaidi ya uchumi wa Zanzibar, lakini kwa sasa uchumi wa Zanzibar unakuwa kwa kasi zaidi ya ule wa Tanzania, kuonyesha kwamba upande wa bara kuna kushuka kwa kasi ya kukua kwa uchumi. Na wengi wanaona hili linaweza kuwa linachochewa na maslahi mengi ya kitaifa kuelekezwa upande wa visiwani kwa kuwa kuna raisi toka visiwani.

Labda lililo kubwa zaidi ni maoni kwamba ikiwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar uko katika hatari ya kuvunjika, au kwamba watu wa upande wa visiwani hawautaki japo hawasemi hivyo hadharani, hatuoni kwamba tunaweza kumpata raisi kutoka visiwani ambae hana imani na muungano, japo anadai kuutetea, na akafanya mambo kwa namna ambayo kama muungano ukivunjika basi awe amewanufaisha upande wa visiwani kwa namna ya kutosha, yaani akatumia fursa ya uraisi wake kuimarisha upande wa visiwani akijua muungano unaweza kuvunjika wakati wowote?

Mfano umetolewa kwamba wakati Jumuiya ya Afrika Mashariki ikikaribia kuvunjia miaka ya 1977, Wakenya wakijua hili kwamba walitaka kuivunja jumuia, walifanya mkakati wa mali za jumuiya ya mashariki kuhodhiwa upande wa Kenya. Siku jumuiya ya mashariki ilipovunjika Tanzania na Uganda walikuja kugundua kwamba Kenya walikuwa na mkakati huu siku nyingi na walitenda mambo wakijua hilo linakuja! Je philosophy hii inawezekana pia katika suala la muungano, kwa kuwa upande wa bara hakuna serikali itakayokuwa macho kusimamia maslahi ya bara?

Sasa haya ni mambo yanajadilika na ni muhimuhimu kuyatafakari katika suala la muungano. Ndio maana basi, tukiri kwamba katika mfumo wa muungano uliopo, inawezekana kabisa raisi kutoka Zanzibar akafanya kazi ya uraisi kwa maslahi ya Zanzibar zaidi ya bara au ya muungano. Kujifanya kama hilo haliwezekani ni kujidanganya, na haya mambo yasipojadiliwa, yanaweza kuleta madhara na chuki zisizostahili. Na lazima pia tukiri ni mambo kama haya ambayo yamekuwa yakichochea madai ya kuwapo na serikali ya kusimamia maslahi ya upande wa bara, kama ilivyo kwa upande wa visiwani.

Nini maoni yako?
Tuna muungano wa kinyonyaji na usio na usawa. Katika hili waasisi walitukosea sana. Ni wakati muafaka wa kuupitia upya muundo wa muungano na ikiwezekana kuuvunja kabisa. Tanganyika inahitaji mtetezi.
 
Malalamiko ya muungano yapo toka G55, lakini walioshikilia nchi hawataki mabadiliko yoyote, Wana nguvu na watu wa kutetea muungano vyovyote ulivyo, matumaini ni kidogo, labda Mungu mwenyezi aingilie Kati, bila shaka mama anajua hizi fursa huwa hazijirudii, hawezi fanya makosa, ni zamu yao zenji, na ni zamu yao kwelikweli
Na hapo ndipo raisi Samia anatakiwa kuwa mwangalifu sana. Hii kufanya mambo kwa kuifanya Zanzibar iwe zamu yao kwelikweli ndio kutaharibu mambo vibaya sana, labda kama mission yake ndio hiyo, huwezi kujua. Kuna watu wanamwangalia tu, hawasemi kitu ila wanaona, na wana uwezo wa kufanya kitu.
 
Kwanza hawezi maana Urais ni taasisi

Pili Tanzania Bara Tanganyika wanachukua pesa ya Zanzibar zaidi ya bil.400 Kila mwaka.
Eti Urais ni taasisi! Kichekesho hiki. Maana katiba inampa Rais umungu mtu, hapo taasisi inakuja vipi!?
 
U Mungu mtu wa kufanyaje? Tuna Rais wa kutoa Zanzibar miaka 3 Sasa,huo u Mungu mtu wa kupendelea kwao uko wapi? Thibitisha
 
Back
Top Bottom